
Habari za leo.
Nawaandikieni kuwakumbusha tu kwamba. sherehe mnaziadhimisha hazihusiani na jamii yetu ya kiafrika.
Nawaandikieni kuwakumbusha tu kwamba. sherehe mnaziadhimisha hazihusiani na jamii yetu ya kiafrika.
Naongelea kushabikia sherehe za VALENTINO, na kwamba kuna sherehe mbali mbali (muafaka)zinaendelea mngeweza kujumuika nazo na kutozama kwenye MKUMBO. Kunakosababishwa na watangazaji(UCHWARA) wa redio wa siku hizi.
MAKUMBUSHO ni taasisi yenye hadhi ya kitaifa na ni urithi na hazina ya taifa letu. Fanyeni utafiti kujua hata hii mnayodhania kuwa ni sikukuu mjue imetokanaje kabla ya kuzama kwenye dimbwi la kudidimia kitamaduni.
Kwa taarifa tu Hiyo sherehe hata huko nchi za magharibi haichukuliwi kwa dhati sana zaidi ya wenye biashara kuitumia tu kwa kuhamasisha watu kununua vitu sio siku inotambuliwa kitaifa mahala kokote. Waswahili tumeanza kuwa na hulka kama zile za kucheza kabla hata ngoma haijapigwa.
Ningependa kushauri tu kama kunahitajika sherehe za ziada basi mwezi huu wa pili unaweza kutumika kama MWEZI WA UKOMBOZI WA MWAFRIKA.
Ndugu zetu walioko Ughaibuni hutumia mwezi huo kukumbuka na kufanya sherehe mbali mbali kujiimarisha kitamaduni. Huu ni mwezi wa kukumbuka kuwa MAAFA yaliyomkuta Mwafrika (nyumbani na walio ughaibuni) yanahitaji kufanyiwa mikakati maalumu kuponya athari zake.
Nataraji taasisi yetu hii adhimu itapokea ushauri wangu na kuangalia nasaha hizi kama za kujenga na wala sio kukashifu. Huyo anayeitwa Valentino hakuwa na sifa yoyote ya UPENDO tena kihistoria anahusishwa na kashfa za udhalilishaji kijinsia na ni muendekeza mfumo DUME.
Nataraji taasisi yetu hii adhimu itapokea ushauri wangu na kuangalia nasaha hizi kama za kujenga na wala sio kukashifu. Huyo anayeitwa Valentino hakuwa na sifa yoyote ya UPENDO tena kihistoria anahusishwa na kashfa za udhalilishaji kijinsia na ni muendekeza mfumo DUME.
Utafiti mfupi tu utakupa icha halisi ya chimbuko hili la mila za KIPAGANI (mila za ulaya). Nashauri tuangalie hapa hapa nyumbani kuona mila na tamaduni zipi zinaweza kutengezewa sherehe na taasisi ya Makumbusho iwe kinara wa kuenzi na kuhamasisha sherehe hizo hadi zikubalike. Naamini hilo lipo ndani ya uwezo.
Mfano mzuri ni ndugu zetu visiwani walivyoamsha tena vuguvugu la mila za KOGA MWAKA japo kuna athari za lenga watu wa magharibi na kupoteza lengo lake asilia (KIROHO), na ngono kupata kipaumbele..Lakini hayo yanaweza kurekebishwa.
Hapa Tanzania kuna mila na desturi nyingi mno zinohitaji kuamshwa upya. Tuanzeni sasa. Kama Mwalimu aliposema enzi zake."WAKATI NI HUU"
Asanteni,
wenu katika kujenga taifa.
Zavara Mponjika
Zavara Mponjika
Mimi naanza kupendekeza tuwe na siku ya kumkumbuka 'mzee ele-ktronish!' yaani afande Kova jana maana alivyounga kesi na alivyotamka hicho kisawe du mpaka mtuhumiwa wake wa Utapeli ghafla ilibidi ainame!
ReplyDeletehahahahahahahahah, duuuuuuuuuuuuuu
ReplyDeletebora mie nisiye na VALENTINO! UJINGA MTUPU...............
Zafara,
ReplyDeleteWatanzania tumepoteza desturi ya kujisomea ndio maana wengi wanafuata mkumbo wa tamaduni kwa sababu tu tumeona kwenye tv au kusikia redioni.
Juhudi zako kama hizi zinasaidia kubadili huo mwelekeo potofu.
BTW, Good job kwenye WAPI events..keep up Bro.
Network Engineer (NE),
Reading, UK
Ni kweli Zavara, sisi kama waafrika tunasahau roots zetu kwa kiasi kikubwa na matokeo yake tunaiga culture za kigeni zilizo/zinazo tuweka utumwani kiakili, kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi. Ila campaign za kuelimisha hiki kizazi zinahitajika kwa kiasi kikubwa kutoa historia sahihi (sio ile tulioandikiwa na mkoloni) itakayofungua akili kwa jamii yote. Long Live Alkebu-lan (Afrika) and its People.
ReplyDeletemwafrika ni mtu wa kipekee sana duniani. mataifa mengine yote yanatushangaa. Mwafrika ukimpa achague kati ya uhuru au utumwa kwa wazungu basi atachagua utumwa kwa wazungu.
ReplyDeleteNduguyangu nashukuru sana kuongea hili jambo. Mimi ninakubariana na wewe kabisa! Kwa kifupi ninaishi hapa ulaya. nimesomea hapa na ninafanya kazi hapa. Ila kumbuka kuwa mimi mbali na kukaa hapa, lakini nyumbani Tanzania pana priority zaidi kuliko hapa. Ndio maana sikosi kuwa nyumbani mala mbili kwa mwaka. Na nikifika Tanzania sio kuzamia Dar kwenye mahoteli ya kifahari bali ni kwenda moja kwa moja kijijini kwa babu zangu! Sasa basi sisi waafrika (Watanzania) ni kweli imekuwa aina fulani ya tabia kucheza ngoma kabla ya kupigwa! Au ni kweli tumeisha kata tamaa na maisha yetu? Hivi unaonaje badala ya ujinga huu wa kujibandikiza (valentine), ingekuwa vizuri kila mmoja wetu akafikiria hata kuwakumbuka ndugu zake ambao labda walishakufa! Mimi ninashangaa kuona watu wanakuwa na akiri za ajabu kwa kila kitu kinachofanywa na ndugu zetu WAZUNGU! KWA NINI HAWA WATU WASIIGE KWETU NI SISI TUIGE HATA WANAVYO LALA JAMANI! SISI TUMEKUWA OVYO SANA NDIO MAANA TUNAUZA MADINI YETU ILI TUPATE CHANDARUA ZA KUZUIA MIBU. HUYU NI MTANZANIA AMBAYE ANAJIITA DR. WA SHERIA AU UCHUMI!
ReplyDeleteFUNGUA MACHO, TUJIVUNIE MAMBO YETU HATA YAONEKANE SI MUHIMU KWA WATU WA NJE CHA MUHIMU NI KUDUMISHA MILA ZETU NA DESTURI AMBAZO ZINAENDANA NA KARNE HII YA 21.
NINAKUSHUKURU WEWE MTOA HIYO HOJA.
Hongera Mkuu
ReplyDeleteSidhani kama kuna Muafrika yoyote atakae kupinga kwa hili. Wakati ni huu mwafrika ajiringie na adhamini utamaduni wake
Mdau hoja yako imepita. Atakayeipinga ujue uyo ajitambui.
ReplyDeleteHongera Sana ndugu SAVARA, wewe ni mfano wa kuigwa. Ni kweli watu tumekua tunakurupuka na kufanya mambo bila kujua yametoka wapi, ili mradi wengi wanafanya.
ReplyDeleteKwanini binadamu tumekua tunafanya mambo bila kutafakari? nauliza swali hili kwa kua mimi naishi hapa Europe, hata hao wazungu wengi wanasherehekea sikuku hii bila kujua mwanzo wake umetoka wapi.
Ni kweli jamii inabidi ielimishwe, watu tusome na kutafuta mwanzo wa mambo bila kukurupuka kwa kua TV imeonyesha. "Most of the time" tuvionavyo kwenye TV ni matakwa ya wamiliki wa TV. NI HAYO TU
Sidhani kama kulikuwa na haja ya kusema watangazaji ni uchwara nk.
ReplyDeleteMila zetu ni zipi?
- Elimu ramsi ya shule si yetu
- Dini Mbili kubwa (uislam na Ukristo) si zetu (ingawa wengi ni waamini wazuri tu)
- Teknolojia nyingi tunazotumia si zetu (Magari, Kompyuta nk)
Lakini licha ya yote hayo, bado WaTanzania tunajaribu kuishi kwa furaha na upendo.
Watu tunatofautiana, na kama kuna watu wameamua kusheherekea Valentine, waache washeherekee, kama hutaki si lazima.
Hoja yangu ni rahisi, mtu atakuwa na tabia kutokana na vile alivyokuwa na vile anavyopenda.
Kama una mpenzi, na unaona tarehe 14 Feb inafaa kusheherekea, fanya hivyo, haijalishi kama unajua maana yake ama la.
Siku hizi sikuu nyingi ni alama tu, mfano Xmas, Nk. Ni maamuzi binafsi ya mtu.
Sifurahii mtu anaposema hiki na hiki si utamaduni wetu
Iga iga 100% ndio jina letu cha mzungu bora japo mwenyewe hakijali. Hivi kwanini hatufanyi sherehe kukumbuka vitu kama vita vya maji maji kila mwaka, tukawaelezea watoto wetu nini umuhimu wa hiyo siku kwetu? Hata mambomengine ndani ya makabila na koo zetu kuliko kukumbuka na kusherehea vitu visivyo tuhusu. utakuta mpaka kuna misa eti ya valentino, wenye sikukuu yao wala kwenye nyumba za ibada hawaendi!
ReplyDeleteIga iga 100% ndio jina letu cha mzungu bora japo mwenyewe hakijali. Hivi kwanini hatufanyi sherehe kukumbuka vitu kama vita vya maji maji kila mwaka, tukawaelezea watoto wetu nini umuhimu wa hiyo siku kwetu? Hata mambomengine ndani ya makabila na koo zetu kuliko kukumbuka na kusherehea vitu visivyo tuhusu. utakuta mpaka kuna misa eti ya valentino, wenye sikukuu yao wala kwenye nyumba za ibada hawaendi!
ReplyDeleteKwa watanzania wengi valentine day ni siku ya KUAMBUKIZANA UKIMWI. Kwa sababu ni siku ambayo vijana wengi wadogo hasa watoto wa shule wanarubuniwa kufanya mapenzi. Vile vile wakubwa zao ni siku ya kustarehe na mahawara zao, wenyewe hawajaoa ni siku ya kulala na girlfriends wake wote kuonyesha anawapenda kumbe unafiki mtupu/
ReplyDeleteIngekuwa siku ya maana sana kama wasichana wangetumia hiyo siku kuwa ni takatifu na wakaacha kutoa uroda hovyo! Ingepunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya ukimwi. Ingetumika pia kuwakumbuka ndugu na jamaa zetu waliokufa kwa ukimwi.
Zavara asante kwa mada hii muhimu. Lakini ni mada tata sana ukizingatia ukweli wa dhana ya utandawazi. utandawazi ni hali ya kweli tunayoishuhudia kila siku na hii valentino ni mojawapo ya ushahidi. utandawazi ni koti jipya la kile kilichoanza kama ukoloni na baadaye kikavaa koti la ukoloni mamboleo. ili ukoloni mamboleo au tuiite hilo jina linalovutia, utandawazi, uweze kufanya kazi au kufanikiwa kuchuma walichokusudia ni lazime wawafanye wahusika watumwa wa kiakili kama ulivyoeleza vizuri sana. Vyombo vya habari hususan redio na tv ni mawakala wakubwa sana katika crusade hii. hapa mbepari anachojali si kwamba kweli alikuwepo binadamu kama Valentino au Yesu bali ni kuwafanya watu waamini hivyo ili auze kadi zake, maua yake, nguo zake, mapambo yake na vikolombwezo ambavyo 'walevi wa kasumba hiyo' wameaminishwa kuwa ndio 'kwenda na wakati'. na mbaya zaidi ni pale inapohusu kushibisha kiu au njaa ya kiROHO au ya kiNGONO ambayo ni mojawapo ya mahitaji makuu ya kibinadamu. Sijui ni kwa kiasi gani tunaweza kukabiliana na kani za kiutandawazi!
ReplyDeleteMdau umeongea pointi sana. Watu wa magharibi wanajitahidi kubrainwash watu ili wafanye biashara. Kama unampenda mwenzi wako huna haja ya kusubiri mwezi wa pili kumwonyesha upendo au mapenzi yako kwake.
ReplyDeleteTwo wrongs don't make one right. Tulishafanya makosa kukubali Ukristo na Uislamu na imani nyinginezo za ughaibuni. Tusikubali kulishwa kila kitu.
habari kwa wote? mimimnipo na wewe bwana ZAVARA kwa 100% kwa nini tuwe watu wa kuiga au kufuata vitu ambavyo hatujui faida zake?kuna mtu ame mentio magari,technology na TV naomba kuuliza kwani hajui faida yake? haya atupe faida ya huyo saint valentine,tujaribu kuangalia vitu vanavyoweza kutangaza culcture zetu na sisi tuache ulimbukeni kwa yule atakaye penda.
ReplyDeleteValentine Ni Sikukuu Ya Kikristo Ya Mt Valentino Haina Uhusiano Wowote Na Ngono Na Starehe Zinazofanywa Siku Hiyo. Sisi Wakristo Wakatoliki Ni Siku Muhimu Kwetu Ya Kukumbuka Matendo Mema Ya Mt Valentino Mpaka Alinyongwa Kwa Kufingisha Watu Ndoa Kipindi Ambacho Mfalme Alikataza Watu Wasipendane Ili Apate Vijana Wa kupeleka Vitani/Jeshini.
ReplyDeleteKwa Hiyo Hili Si Swala La Kuiga Ni Swala La Imani Yetu Sisi Wakristo Wakatoliki. Nasisitiza Sikukuu Hii Haina Uhusiano Wowote Na Matendo Yanayofanyika Hivi Sasa Na Watu.
Tukianza kutilia maanani hayo yote basi hata Zavafarai hizo locks(kipilipili) aka Rasta itabidi tukate maana ni za waJamaika...muafrika akiwa na hizo nywele basi kidogo akaunti yake ubongoni imepugua salio... yapo mengi yakurekebisha katika kuutafuta muundo mzima wakiafrika usio ingiliana wala kufungamana na upande wowote.. safari bado ni ndefu na shukrani kwenu nyie mnaoanza kuyaona mapungufu hayo.
ReplyDeletezavara...(sp) you copy what you like best, whether its your own downfall or not, i for one, wont visit makumbusho village simply because i need to be re-connected with my cultural heritage..heck NO ! am not a fan of such stuff, i am not a fan of uzungu either, i am just doing what makes me and my family happy, and if it means me and my husband going out for diner at a nice cozy place with candlelight then be it ! for those who likes to keep it down with culture they are free to do so, if TV has made me forget my culture, i dont blame anybody, i am just doing what makes me happy and that's what's up...do i hear someone calling me a copy cat ? so BE IT
ReplyDeleteNadhani Mjadala Uliopo Ni Sisi Waafrika Tunaiga Mambo, Na Kuwa Tumeiga Sikukuu Ya Valentine, Ukweli Ni Kuwa Sikukuu Hii Ni Ya Kiimani Kwetu Sisi Wakristo Wa Madhehebu Ya Kikatoliki. Sasa Kama Tunazungumzia Kuiga Tu, Tutoe Mifano Mingine Si Kuingilia Imani Za Watu. Maana Tutasema Pia Sikukuu Ya Waislamu Ya Eid Tumeiga Sisi Waafrika. Hoja Hizo Si Nzuri Maana Ni Za Kiimani, Kuingilia Imani Ya Mtu Si Jambo Jema. Si Vema Kusema Sikukuu Ya Mtakatifu Velentine Ni Waafrika Kuiga. Je Sikuu Za Dini Zingine Waafrika Wanaiga? Kwa Maoni Yangu Tuzungumzie Mambo Ya Kuiga Bila Kuingia Kwenye Mambo Ya Imani Yapo Mengi Ya Kuzungumza Yasiyo Ya Imani. Wanaofanya Ufuska Siku Hiyo, Hao Ni Wazinifu Na Ufanya Hivyo Wakati Wote Bila Kujali Sikuukuu Yoyote.
ReplyDeleteVALENTINE'S DAY..
ReplyDeleteHII CKU HUWA INANIFURAHISHA SANA,!
SIJAIELEWA MAANA YAKE HALISI NI NINI? NGONO DAY AU?
MAANA JARIBU KUFANYA RESEARCH CKU HII UTAONA MAAJABU..NYUMBA ZOTE ZA WAGENI ZIMEJAA KUANZIA ASUBUHI,KAMA KUNA MGENI ANATAKA KUJA KUFIKIA HOTELINI DAR CKU HII HAKIKA ATALALA NJE,VYUMBA NEHI KABISA,NA HII INAONYESHA WENGI WAO HAWAKO NA WAPENZI HALALI AU WANA NDOA..
KM KWELI MTU NI MKAZI WA DAR NA YUPO NA MPENZ WAKE HALALI WA KILA SIKU AU MKE/MUME NINI KINAWAPELEKA G.HOUSE AU HOTELINI,SI WANGEFANYIA MAJUMBANI MWAO?
TENA HUWA NACHEKA SANA KUONA KILA NYUMBA YA WAGENI MLANGONI KUNA KIBAO
1.NAFASI HAKUNA
2.VUMBA VIMEJAA
HAHAHAAAAAAAAAA VALENTINOOO