


Bwana Michuzi,
Kama mkatoliki, kuna kiongozi wangu ninayemkumbuka sana, ambaye aliijengea heshima kubwa sana kanisa na nchi yetu wakati wa uhai wake. Huyu si mwingine ila Muadhama Laurean Cardinal Rugambwa.
Kama mkatoliki, kuna kiongozi wangu ninayemkumbuka sana, ambaye aliijengea heshima kubwa sana kanisa na nchi yetu wakati wa uhai wake. Huyu si mwingine ila Muadhama Laurean Cardinal Rugambwa.
Ikumbukwe kuwa huyu mzee alikuwa Kardinali wa kwanza mweusi barani Africa, na alifanya kazi kubwa kuweka heshima ya kanisa katoliki ndani ya makao makuu ya kanisa hilo ndani ya Vatican.
Aliishi maisha maadilifu sana. Kwa wadau wanaomkumbuka mzee huyu je wanaweza kuchangia ni jinsi gani sisi kama wakatoliki na watanzania kwa ujumla tunavyopaswa kumuenzi katika nyanja mbalimbali?
Tuweke michango tafadhali.
Mdau DEO MUSHI
Mdau DEO MUSHI
when I visited the my city,I was selected among kids to baptised those in that area,Named after Him!! No wonder I have lived Uprightly to Honor his Name
ReplyDeleteBaba Kardinali Rugambwa anastahili kuanzishiwa mchakato wa kuwa mtakatifu. Hii ni wazi kabisa. alifanya kazi kubwa sana ya kuleta uhai wa kanisa katika Afrika, hadi kufikia hapa tulipo. Yeye pamoja na wamisionari wengine kama vile Hayati Padre Cassian Spiss wametoa mchango mkubwa katika kustawisha kanisa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla
ReplyDeleteUkweli ni kwamba huyu mtumishi wa Mungu muadirifu amesahaurika kabisa ni jambo la kushangaza sana kwa kanisa Katoriki na Taifa la Tanzania kwa ujumla!. Hata wakati wa kufikiria kuwatangaza wenye heri kanisa lilimfikiria kwa haraka Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye naye alimuheshimu sana Muadhama Laurian cardinal Rugambwa.
ReplyDeleteNina uhakika kama Baba wa taifa angekuwa anatakiwa kutangazwa mwenye heri akiwa hai angekataa kufikiriwa yeye badala ya cardinal Rugambwa!
Ndugu Wakristo Wakatoliki kama kweli tunataka kutenda haki kwa Mwenyezi Mungu ebu na tumkumbuke mzee huyu kwa kuadhimisha japo kumbukumbu ya kifo chake au siku ya kuzaliwa kwake jamani ni kweli ametutendea mema mengi wakristo, kanisa na taifa kwa ujumla.
Mwenyezi Mungu akubariki sana wewe uliyeleta mada hii nawe Issa Michuzi uliyekubali kuitangaza kupitia kwenye blog yako kwakuwa hukukataa kwakuwa eti sio dini yako na hivyo sio kiongozi wako, ahsante sana.
Mimi si Mkatoliki na wala si Muislamu lakini huyu jamaa pamoja na Sheikh Mkuu wa wakati wa Mwalimu, Hemed bin Jumaa bin Hemed, nawaheshimu sana wazee hawa. Hawa jamaa walikuwa na busara utafikiri si watu miongoni mwa Watanzania. Hawakuleta kero wala usumbufu, waliheshimiana na serikali vizuri na Watanzania wote tulipendana kwa sababu wao hawakuchokonoa upuuzi. Siku hizi tuna wanasiasa wachafu na viongozi wa dini wababaishaji (mnawajua wote), na matokeo yake watu wanafanya na kusema mambo ya kijinga. Tanzania ya enzi zile ingawa ilikuwa na ulofa lakini ilikuwa imetulia. Safi sana Deo kwa kutukumbusha mambo kama haya.
ReplyDeleteKadinali Rugambwa alikuwa miongoni mwa viongozi wadini wachache sana walio waadilifu waliowahi kutokea katika anga za Tanzania, pamoja na uadikifu wake alikuwa mwenye akili nyingi mno zilizomfanya awe na uwezo wa juu katika masomo pia kusababisha kuwa mwafrika wa kwanza kufuzu "canon law" katika alama za juu kabisa kuliko wakati wowote alipomaliza masters na phd yake katika masomo hayo huko Rome.
ReplyDeleteMnamo mwaka 1962 katika mahojiano na vyombo vya habari Askofu Mkuu Edgar Marantha (mzungu) aliyekuwa askofu mkuu wa jimbo la Dar-es-salaam alisema kuwa hajui kati ya kadinali Rugambwa na Mwalimu Nyerere nani angekuwa kadinali wa kwanza wa Tanzania na Afrika kwa ujumla iwapo Nyerere angeendelea na utashi wake wa kuwa padri ambao ungemfanya asiingie katika ulingo wa siasa na pia hajui nani angekuwa rais wa kwanza wa Tanzania kati ya Mwalimu Nyerere na Kadinali Rugambwa iwapo Kadinali Ruganbwa angeamua kuwa mwanasiasa.
Point ya Askofu Marantha ni kuwa hawa watu wawili walikuwa na upeo wa juu na akili ya juu sana ambazo zilishabihiana kiasi cha kwamba kama wangekutana katika anga moja kwa pamoja ingezua kizazaza.
asante mdau kwa kutukumbusha sehemu ya historia.
ReplyDeleteOh samahani mimi si mkatoliki ila nimeguswa na marehemu Kardinari Rugambwa.Nakumbuka nilihudhuria heshima za mwisho pale Bukoba kanisa kuu pia baba wa Taifa alienda hadi kijijini kwenye mazishi.NASIKITIKA WAKATI HUU WA FISADIS ERA NI NGUMU KUENZI WATU WETU KAMA HAO.
ReplyDeleteHistoria ya watu mashuhuri wa Tanzania inabidi iwe digitalised. Ninamaanisha kuweka habari zao kwenye mtandao, kwani kizazi cha sasa ni IT generation. Wengi wetu hatutapata nafasi kwenda kwenye Makumbusho ya Taifa, kwahiyo kwa kutumia vizuri tovuti kama wikipedia.org tunaweza kutaarifu dunia nzima kuhusu nchi yetu na watu wake mashuhuri. Nimeona kurasa ya Rugambwa kwenye wikipedia umeandikwa vyema, heko kwa aliyehariri.
ReplyDeletehttp://en.wikipedia.org/wiki/Laurean_Rugambwa
wakatoliki, wakatoliki, mie sisemi
ReplyDeleteI totally I agree, he was good person, and a good leader in Catholic church. Ver intelligent
ReplyDeletenakumbuka huyu jamaa alimlambisha nondo ya kipaimara my sister pale pugu pale miaka hiyo...
ReplyDeletewengi wanadhani next black pope atatokea west africa, lakini kuna uwezekano mkubwa sana kiimani atatokea east africa kama ninchi ni nchi gani east africa ni imani yako itakuongoza kuifahamu nchi hiyo itakopokuwa!! ila kama angekuwapo Rugambwa ingekuwa wazi!
ReplyDeleteMdau!
Wapenzi,
ReplyDeletemimi natoka Mwemage parish, Bukoba ambayo mhashamu aliijenga kwa juhudi zake za kutafuta wafadhili. Alijenga hosp. na kuleta waganga toka uholanzi ambao walikuja kuondoka sababu ambazo wana tanu wa wakati wa 72 wanazijua. UBINAFSI. Mhashamu alijenga Mwemage Girls Upper primary school ambayo nilisoma mimi na walionitangulia na kunifuata. Alinipa kipaimara na mama yangu alimpikia mchuzi wa kuku the day before. Nilipopeleka kitoweo nikamsalimia tata olailota akajibu eti ndaile ninkulota. Meaning he was dreaming about me. I was 6. What a shock I could not believe a Saint dreamt about me. I thought I was in heaven! Kama mnataka kujua mengi kuhusu alipofariki kilichotokea, waulize waliokuwa BK siku ya kuzikwa kwake na senene zilizoanguka muda huo!!!
Kama mnatafuta watakatifu Unsung heros ni Kadinari Rugambwa na rafiki mpenzi wake Mwalimu Julius, BASI!
anonymous 12.11.00 am. mada si wakatoliki wala kanisa, mada ni kardinali rugambwa kama mtu binafsi kulingana na maisha yake kama mtawa..ni vyema kama huna la kusema juu yake,..hongera deo kwa kutukumbusha habari za ndugu huyu..ni vyema kanisa likaweka siku moja ya kuadhimisha kuzaliwa (si kufa!)kwake..ili tumuenzi
ReplyDeleteAhsante! sana Deo kwa kunikumbusha mbali.Namkumbuka vizuri marehemu Cardinal Rugambwa kwani mimi ni mmoja kati ya wanafunzi waliosoma katika shule ya msingi Bunena mkoani Kagera kati ya mwaka 1987-1991 na kisha kuhamia Jijini Dar-es-Salaam nilipomalizia elimu yangu ya msingi.Shule ya msingi Bunena ipo jirani kabisa na kanisa Katoliki la Bunena (alimozikwa Rugambwa) ambapo marehemu Rugambwa alipenda kuja na kuwajulia hali walimu na wanafunzi mara kwa mara.Pia wakati mwingine marehemu Rugambwa alikuwa akija shuleni wakati wa mapumziko na kuwakuta wanafunzi wakicheza na yeye kuutumia muda huo kuzungumza nao.Kifo chake kilinishtua sana ambapo wakati huo nilikua kidato cha tano pale St.Anthony's Secondary School Jijini Dar-es-Salaam.Bunena ni shule ambayo inafundishwa pia na masista wa kanisa Katoliki.Marehemu alikuwa ni kipenzi cha watu na ataendelea kukumbukwa daima kwa mema yote aliyoyafanya ndani ya kanisa Katoliki.Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi,Amina.
ReplyDeleteMdau mwanafunzi-India.
Tuchunguze maandiko kitabu cha Daniel na ufunuo wa Yohana juu ya mnyama atawalaye dunia mwenye namba 666...
ReplyDeleteNaomba kuwasilisha...!
Mdau
Mimi namkumbuka sana cardinal Rugambwa katika miaka ya mwanzoni ya 1980-1994 nilikuwa mmoja wa vijana watumishi wa misa katika parokia ya mt.petro-oysterbay.
ReplyDeleteAlikuwa mpole sana na mnyenyekevu. hakuwa msemaji sana. wakati wa sikukuu kama za kipaimara ama pasaka ambazo yeye alikuwa akishiriki alikuwa akituonesha mapenzi ya hari ya juu, akitubaliki na kutuombea.
kwa kweli kuna haja ya kanisa kuweka siku moja kwa ajili ya kumbukumbu yake. pumzika kwa amani baba laurian cardinal Rugambwa.
Namshukuru sana Deo kwa kunikumbusha Cardinal Rugambwa, ni siku nyingi zimepita tangu afariki. Mimi nimesomea primary school Kashozi (Kamukukubwa) kwa wanaolijua jina hilo. Nakumbuka nilipokuwa ndogo miaka ya 1970's alikuwa akija kutembea hapo Kashozi Parish, tulikuwa tunafurahi sana kwa kuimba nyimbo na kucheza ngoma hasa wakati wa kupata Kipaimara maana ndiye alikuwa mtoaji kipaimara kwa wakati huo. Lakini napingana na mtoa mada hapo juu eti Baba wa Taifa alienda kumzika huko kijini kwao na mwingine kasema amezikwa kanisa la Bunena Bukoba mjini, huo ni uongo mpaka sasa Cardinal Rugambwa hajazikwa ila ameifadhiwa katika Kanisa kongwe la Kashozi hata ukienda sasa hivi unaruhusiwa kwenda kumwona alikowekwa kwa kutoa shs. 500/ za kununua umeme maana amezungukwa na taa zinazowaka wakati wote. Mpaka hapo baadaye atazikwa kwenye kanisa lake alilolijenga yeye mwenyewe linaloitwa Cathedral hapo Bukoba mjini ambalo linafanyiwa ukarabati pia na kutengeneza kaburi lake. Ni hayo tu ninayoyajua kwa Cardinal Rugambwa.
ReplyDeleteits about time the government honor this super class individual by returning all the institutions he built to the church...coz all the institutions he established through his hard-work and love to his community are in a very terrible state under the government supervision..those who attended Rugambwa High School knows wot i mean.
ReplyDeletekusahaulika kwa baba kadinali Rugambwa kunatokana na Wakatoliki wenye na asa viongozi ,wabadilike ata wajaribu kuleta siku ya kumkumbuka walau mara moja kwa mwaka ndani ya kanisa.kwani ndiye mweusi kardinali wa kwanza mweusi,yahani mtu mweusi wa kwanza kukubarika kwenye utawala wa juu wakiroho ulimwenguni kwa nini asikumbukwe na wanakumbukwa wale tu waliotwala Tz?Tutumie busala jamani.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu aiweke roho ya kadinali Rugambwa mahali pema peponi,Amina.
Kwanza nimsahihishe Anonymous (09:03:00); Rugambwa hakuzikwa katika Kanisa la Bunena, bali mwili wake ULIHIFADHIWA katika Kanisa la Kashozi, takriban km 15 Kazkazini mwa mjini wa Mji wa Bukoba. Nimetumia neno kuhifadhiwa kwa sababu, ilielezwa wakati huo kuwa atahifadhiwa hapo kwa muda, hadi MAZISHI yake yafanyike katika Kanisa Kuu la Bukoba, alilochagua mwenyewe kuzikwa. Kanisa hili wakati huo lilikuwa linafanyiwa ukarabati, na hadi hii leo halijakamilika. Miaka miwili iliyopita nilizungumza na Uongozi wa Jimbo la Bukoba na kuthibitishiwa kuwa kanisa liko karibuni kukamilika, na MAZISHI ya Rugambwa yatafanyika huko kama alivyoagiza na kama ilivyoahidiwa. Kwa hiyo bado HAJAZIKWA
ReplyDeleteAnony Thu Feb 04, 10:07:00 AM
ReplyDeleteLAbda huyo 666 ni wewe.
Bible imeandikwa juu ya maisha yako na si mtu fulani kama unavyojifanya wajua
mbona hata kwenye hili jema unaingiza mapepo yako
Hata waislamu wameonesha kumtambua na kumfurahia kwani dini ni upendo.
Ulivyo mwanga na mwenye mipepo unatafuta attention kwa kutaja 666
Mimi naona ni wewe mwenyewe ndio anti christ kwakuwa huoneshi kuheshimu amri kuu ya upendo
kamuone daktari akutibu ADD Attention Defficient Disorder
kumbuka mara zote shetani hutujia kwa emotions zetu.
kuna mdau humu anaota kwamba kuna siku atatokea papa muafrika. Inawezekana huyu mdau anajidanganya kwa obama kuwa rais wa marekani.
ReplyDeleteMtawala wa himaya ya warumi kamwe hawezi kutoka afrika.
Ni sawasawa na waislamu waanze kujidanganya kwamba kuna siku imamu wa maka atakuwa mtu mweusi.
ANONY FEB 03, 09.25:25:00 UMENIFURAHISHA SANA NA MAELEZO YAKO NASHUKURU KWA UCHAMBUZI WAKO
ReplyDeleteWe anon wa Feb 04,01;19 pm inaelekea una ugonjwa wa kutojiamini, maka kuna imamu mweusi tayari soma hii habari kwenye hii link,jitahidi uwe unazungumza vitu unavyokuwa na hakika navyo, pili lazima uwe na komfo na rangi yako mambo ya kujidharau kama wewe hayapo tena duniani.
ReplyDeletehttp://www.mujahideenryder.net/2009/04/11/the-saudi-obama-shaykh-adil-kalbani-first-black-imam-of-masjid-al-haram-makkah/
Jamaa ndio alikuwa awe Papa Johni Paul wa II ila jamaa wakamzibia tu. Mwekweni awe mtakatifu basi. Hata alipozikwa haijuikani.
ReplyDeleteHey Michuzi, this made my day today... Thank you :-) There's something amazing about men who live simple lives... I'm a Nyerere fanatic so I feel this. Cheers!
ReplyDeleteHasante sana kwa picha za Mhadhama Kadinari Rugambwa.
ReplyDeleteKAKA DEO ASANTE KWA MADA NZURI.
ReplyDeleteMIE HUWA INANISIKITISHA SANA HASA HAPA KWETU BUKOBA KWA JINSI TULIVYOMSAHAU HUYU MTUMISHI WA MUNGU, KILICHOPO JINA LAKE LIMEBAKI KWENYE MASHULE NA MAJENGO TU. FIKIRI TANGU ATUTOKE ETI KANISA LINAKARABATIWA ILI AZIKWE PALE ALIPOPACHAGUA MPAKA WA LEO BADO, HIVI HUO NI UKARABATI NI WAAJE? NISAIDIE JAMANI!!!
NDUGU YANGU Reggy's KUAMBIWA ETI UKARABATI UNAKAMILIKA HIVI KARIBUNI, TUOMBE UZIMA TUISHI UTANIAMBIA AU UTAONA UKARABATI ULIOAHIDIWA KUKAMILIKA HIVI KARIBUNI.
MSAADA: HIVI NI SAWA NYERERE KUTANGAZWA MWENYE HERI KABLA YA RUGAMBWA?
Mungu ampuzishe kwa amani Rugambwa!!!! Kwa kipindi cha uhai wake katika jiji la DSM, Rugambwa alionekana ni kiongozi wa MAADILI na busara. Na kama angekuwa bado anaishi leo hii, nafikiri kwa BUSARA ZAKE Mafisadi waliozagaa ndani ya nchi wangepewa NENO la Busara na kujirudi!!!!!
ReplyDeleteRugambwa pumzika kwa Amani!!!!
ReplyDeleteTunaomba Ruhusa ya mchakato wa kumtangaza Rugambwa Mtakatifu!!!