Ankali michuzi japo ni habari iliyopita nimeona niitume maana mie binafsi ilinishangaza sana. Ilitokea pale darajani usiku wa kuamkia jana tarehe 12 feb kama unashuka tokea kwa komba mbezi karibu na njia panda ya kawe na mwenge. Vipi vekesheni huko Ifakara.
Mdau Sam
Sent from my BlackBerry® smartphone from Zain Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Haya kaka kweli chombo chako cha kuwasiliana kiko makini.Smartphone siyo! tulishaipata hii huku ughaibuni but asante kwa kutukumbusha

    ReplyDelete
  2. dah sasa hapo mbele kioo kimetoboka au ndo alipochoropokea dereva?? vipi hali za victims wa hii ajali lakini manake naona haijatulia kiaina.
    @ ankal salamu vipi bado ifakara au tayari ushatimba bongonyoso?? manake hamna pics za mandhari ya ifakara. poa sana mwana nlikuwa nakupa hi tu, kwakweli i can't ask for more for this wkend and probably the coming wk mambo safi kwakweli ya jana bado inakosa upinzani.
    Mdau wa pajazzzz

    ReplyDelete
  3. hii si ya mwaka, ya karne, sipati picha, mungu atunusuru

    ReplyDelete
  4. Hii yote shauri ya speed! Tutaendelea kujiua na kuhatarisha maisha ya wengine mpaka lini? Tunakufa kwa ajali hata kuzidi wanaokufa kwa mabomu ya Pakistan na Afghanistan!! Imeshakuwa kawaida na tumezoea!

    ReplyDelete
  5. Wadau, hivi hii yaweza kuwa imesababishwa na nini? udereva mbaya, dereva bado anajifunza au dereva kuwa ulevi. Siamini macho yangu.

    Kwa mazingira ya pale darajani hii ajali ni ya aina yake utadhani gari kaipachika kwenye mti kwa kutumia crane.

    Jamaa asali sana.

    ReplyDelete
  6. Kama kuna mdau anajua kilichotokea kwa undani mpaka hii gari iko hapo juu naomba atueleze.

    Vipi waliokuwemo wametoka salama?

    ReplyDelete
  7. that is a parking lot. jamaa kafika hapo aka park bila kulipia. pombe siyo chai. Lol

    ReplyDelete
  8. Mhusika wa ajali hafahamiki. Usikute mwizi wa penzi. Likely alikuwa na hawara, kwanini akatoweka?

    ReplyDelete
  9. wadau tuepuke kuendesha kwa kasi, tukishindwa tuwe waangalifu tunapoendesha.

    Pombe na kuendesha ni hatari.



    Mdau Ikumbi

    ReplyDelete
  10. Nadhani hapo alipovunja kioo ndipo alipotokea maana milango yote ilikuwa inaning'inia hewani. Mimi niliikuta ajali hiyo asubuhi ya saa moja na sote tulikuwa tunashangaa huyu jamaa amefika vipi hapa juu.

    Yule askari aliyehojiwa alisema imetokea kwenye saa nane za usiku kwa hivyo kwa asilimia kubwa imesababishwa na ulevi. Nadhani jamaa aliposevu tu alikimbia mpaka nyumbani kwake hata kama ni kilomita kumi.

    ReplyDelete
  11. HII SIYO AJALI BALI NI KAMA PICHA TUNAZO ONA KWENYE SINEMA.

    ReplyDelete
  12. Mpenzi Jini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...