Kamanda Selemani Kova akjionesha wanahabari
pingu ya Mwandishi wa TBC Jerry Muro
stakabadhi ya ununuzi wa pingu za mwandishi wa TBC Jerry Muro
habari kamili


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. KOVA ANAWEZA KURUDI KWENYE PRESS CONFRENCE NA KUWAAMBIA WANANCHI KWAMBA AMEKOSEA KUSEMA KWAMBA RAIA ARUHUSIWI KUWA NA PINGU NA HAMNA DUKA LINALO UZA PINGU NCHINI?


    ANAWEZA KUSEMA KWAMBA WANANCHI TUNARUHUSIWA KUWA NA PINGU?

    INAMANA YEYE ALIKUWA HAJUI SHERIA ZA NCHI?


    NAONA NI BORA AJIUZULU TU MANAKE HATA SHERIA ZA NCHI HAZIJUI NA YEYE NI KAMANDA JE HAO WACHINI YAKE?

    ReplyDelete
  2. Kova sasa sijui atarudi na Ipi siku zile hakusema kuhusu CCTV alipomsoma Jerr muro maongezi yake Mbona hakuna CCTV akaja na kuhusu CCTV, Atakuja na Kuhusu Pingu kama Mdau alivyosema wa Kwanza.

    Kova aKa ELEKTRONIKI aKa We Sogea Huku NJOO HAPA NJOO HAPA aKa Utata Msije kusema Tumecheza Faulo.


    Tambara au Video ay Picha ndio Linaanza kukolea hahahaha. Pazi.

    ReplyDelete
  3. unajuwa watanzania tuna matatizo siamini kama mnaweza tetea tapeli kama jerry wewe unae fungua kinywa mpaka mwisho kumtetea jerry na wewe utakuwa ni tapeli tu kwani sisi wanyonge tunajua jinsigani jerry alivyo tutapeli apo awali ila tukawa atuna chakumfanya kwakuwa yeye anajuwa mamboyake anavyo yaendesha kova tunashukurusana kwa kumtolea aibu kwani mashaidi tupo tunaojuwa ukweli wa jerry katuonea mda mrefu kwa kutuzurumu tunafurai kwa kaziyako kova kamata wote hao kama wakina jerry

    ReplyDelete
  4. Nina mambo mawili juu ya Jerry.
    Moja. Sheria inasemaje? Jerry kama mwandishi na raia wa kawaida anaruhusiwa kuwa na pingu? ni za nini? yeye amekuwa police? Naomba kueleweshwa.
    Mbili. Swala la Jerry kutoa habari za rushwa na hasa polisi kule Iringa isiwe kigezo cha kumsafisha kuwa hausiki kwenye rushwa. Uandishi wake wa habari za uchunguzi siyo kinga. Badala ya kumhukumu Jerry au Kova, tusubiri uchunguzi na mahakama ndivyo vyenye uwezo wa kuonyesha nani yupo sahihi.

    Tuache ushabiki.

    ReplyDelete
  5. Pingu hizi ni za mambo ya chumbani na mpenzi wake ama ni tahadhari ya kujiandaa kuwakamata watu wabaya wenye nia ya kumdhuru?

    ReplyDelete
  6. JOHN MASHAKA MBONA KIMYAAAAAA??? US BLOGGER ANAKUSHINDA BWANA. tunataka kukusikia. Tena sasahivi sio mpaka baadae usiwe kama mganga wa kienyeji.

    Unamwambia Kuku wangu kapotea namtaka arudi unamuuliza aliyeibiwa Kuku kama ana Laki mbili.???????. Kimaro.

    ReplyDelete
  7. michuzi mie ningemshauri jerry atulize mzuka,,,,hv vitu vingefaa vioneshwe mahakamani picha ndio ingekuwa tamu...!
    kucheza na vyombo vya habari vinaweza vikamcost yeye Jerry!
    Ney..

    ReplyDelete
  8. Kwa nini kova ameikamia sana kesi hii? mbona kuna kesi nyingi haitishi press conference? mimi naona kuna jambo. kovu anatumwa na hasira badala ya kutumia maarifa.

    ReplyDelete
  9. Lakini pamoja na yote Muro alikuwa anatumia pingu kwa ajili ya nini?

    ReplyDelete
  10. KWANI TATIZO NI KUWA NA PINGU AU TATIZO UNAITUMIAJE??
    KWANI PINGU NA BASTORA KIPI NI HATARI ZAIDI KWA WATU WENGINE?
    SUMU YA PANYA NI MBAYA KAMA AKIINYWA BINADAMU TUU ILA AKILA PANYA HAINA TATIZO..

    ReplyDelete
  11. Huwezi jua alikuwa anatumia pingu kwa ajili ya nini. Kuna watu wanapendelea kutumia pingu na mijeledi wanapokuwa chumbani katika mambo ya faragha, sio kila siku kifo cha mende.

    ReplyDelete
  12. Eti pingu za nini?anatumia pingu kumkamata anayemtishia maisha.
    Pili, jua kwamba kuwa na pingu sio kosa la sheria. Nenda hilo duka la serikali linauza pingu bwerere-ukitaka hata wewe watakuuzia hauitaji permit, so dont try to change the subject here, the story was Jerry atempted to accept bribery! Unfortunately you can't prove your case, rather you are bringing up some bushit about handcuffs.
    Hao wanaotoa comments praise Kova, ni police wenzie, and all the haters of Jerry.
    I realy dont know how you are having such an ediot as the head of police force.

    ReplyDelete
  13. Waandishi wa Habari na wenyewe ni Wezi na matapeli. Wamezoea kuonea watu na kuwatisha kwa kuwaandika kwenye Magazeti na kuwachafulia majin. Huyo Muro na yeye ni mmoja wa matapeli kama hao Police.

    ReplyDelete
  14. Jamani eh! Pingu ni kwa kizungu kwa kiswahili ni Kamba za kufungia mikono,sasa sifikiri kama kuna kosa kumiliki pingu,especial ukiwa mtu wa mapenzi,ila PINGU PLUS SILAHA hapa kuna jambo,Halafu na huyo Jerry au sijui TOM,kujitia kimbele mbele hadi kumiliki vitu hivi mwache akione sio,ijapokua Kova na yeye Yumo wanajuana hawa wana kesi zao za zamanit u

    ReplyDelete
  15. WADAU MKASOME HAPO PALIPOANDIKWA BOFYA HAPA KWANZA KABLA YA KUCHANGIA MADA!! WAMESEMA PINGU SIO SILAHA!! SASA HAPO HAKUNA KESI, BUNDUKI NI HALALI, RUSHWA HAKUKAMATWA NAYO, PINGU INA RISITI NA SIO KOSA KWA MTANZANIA KUWA NA PINGU. KWA HIYO HAKUNA KESI HAPO!! SASA LABDA TUSUBIRI CCTV AMBAYO HAINA SAUTI NA SASA KOVA UTAKUJA NA USHAHIDI WA ETI "WAHUDUMU WALIOKUWA WANAUDUMIA WALISIKIA WAKISEMA"!!!

    ReplyDelete
  16. Ukitaka kujua kwa nini Kova amekomalia issue hii na kuvuta hisia za watu wote na vyombo vya habari ni kwa ajili ya kupoteza lengo kwa mambo mazito yanayoendelea kujadiliwa huku bungeni hivi sasa. Hii yote ni kuwapumbaza waandishi wote na kuripoti issue ya jerry Muro na kusahau mambo ya Richmond yanayotegemewa kujadiliwa. Jamani kuweni macho na mitego na mchanga wa macho sio mara ya kwanza kwa issue nzito zikiwa zinajadiliwa bungeni zinaibuka issue ya kusahaulisha watu na vyombo vya habari. Mtaniambia hii kesi itakavyoyeyushwa na bunge ndo linaishia hivyo. Kwa kweli nimesoma makala ya Mama Ananilea Nkya, huyu alikuwa na wazo kama langu.
    Kwa undani zaidi bofya hapa:
    http://www.darhotwire.com/home/news/2010/02/04/sakata_la_jerry_na_ccj_ni_mchezo_wa_mafisadi.html

    Mdau Belgium

    ReplyDelete
  17. nyie wote mnaeuliza jerry anatumia pingu ni yanini? dhahiri inaaonyesha kwamba na nyie ni polisi malimbukeni,kwani serikali inauza pingu kihalali kwa nini?jibu nikwamba ukiwa na pingu pamoja na silaha inamaana akitokea adui mfano;jambazi unamuonyeshea silaha akikubali masharti unampiga pingu kwa kifupi pingu ni kama kamba ya kiaina ndio maana ni halali kwa raia kuwa nazo na ughaibuni wanatumia sana kwenye mapenzi sawa afande na wewe kova mwingine unae jiita MWAIPOLO sasa wewe unasema nyie wanyonge mnajua kiasi gani jerry alivyowatapeli,kweli huyo jerry angekuwa ni mtapeli basi atwatapeli hata wanyongee?maana myonge inamaana atakutapeli sh5,000hivi we wacha ulimbukeni rudi huku primary school uje usome kidogo.

    mdau MERU PRIMARY SCHOOL ARUSHA

    ReplyDelete
  18. Mtaongea saana lakini yote tisa Kamanda Kova kachemsha, Mzuka wa nini!!!!! mbona kaikomalia saaaana hii issue alafu cheki anavyoboil sasa sijui atajificha wapi.

    ReplyDelete
  19. KOVA KUBALI KATAA UMECHEMKAAA BABU

    ReplyDelete
  20. jerry muro yeye ni nani make labda ni shushu sasa hizo pingu ni nini kwa mwananchi a kwaida ianmaana kazi yake ya uandishi inaruhusu pingu alafu mbona jerry ana visikendo vingi mno kuanzia alipokuwa ITV

    ReplyDelete
  21. Kununua pinguni kama kununua kofia...... ila kwa watanzania ni mara ya kwanza kuona mtu ana pingu. Pingu ni nzuri sana kama ukimshuku mtu anataka kukudhuru ili asitimke then unamfunga na kuwaita polisi.

    ReplyDelete
  22. Kuna jambo linanitatiza Pingu zimenunuliwa Mizinga Upanga Shop muhuri upo pale chini huku juu tena kuna muhuri Mizinga shop Morogoro imekaaje hiyo au utaratibu uko vipi? KIGMB

    ReplyDelete
  23. Enyi watanzania msiokuwa na akili, ni nani amewalaani?

    Kumiliki pingu ni haki ya mtu yeyote. Ile siyo silaha. Nathubutu kusema kuwa hata mapanga tunayonunua pale kwenye hardware kwa shin 5,000 ni hatari kuliko pingu.

    Kuna watu wanauliza eti "Mwandishi wa habari ana haja gani na pingu?" Hili ni swali la kutapatapa na linaonesha kuwa muulizaji amekosa pa kumpiga Muro. Waingereza wanaita "hanging on to straws". Wewe mtu tayari anamiliki (kihalali) silaha ya hatari kama pistol, halafu unamuuliza eti pingu ya nini?!!! Tumbaf! Bora hata ungeuliza, mwandishi ana kazi gani na pistol? Lakini hauulizi hilo swali kwani unajua utaumbuka hapo hapo.

    Mwisho, Tanzania ina watu Millioni 40. Kila mmoja wao ni complex sana. Kila mmoja anamiliki vitu vyake, vingine ambavyo wewe unaweza usiwe umeona umuhimu wa kuwa navyo. Na wewe pia unavitu ambavyo wenzako hawana. Hatuwezi leo tukaanza kusema tumchunguze kila mtu ana kitu gani nyumbani halafu tukaanza kurukia conclussions kutakana na vitu tunavyokuta huko.

    ReplyDelete
  24. SIONI SABABU YA RAIA WA KAWAIDA KUMILIKI PINGU, BASTOLA NAYO NI QUESTIONABLE, JERRY ANA LAKE JAMBO, ACHENI USHABIKI WA BILA KUFIKIRI.

    ReplyDelete
  25. Kumbe Jerry aliwahi kumtapeli kaka hapo juu aliyetoa comments zake

    Wengine hamjui kitu mnajifanya mnajua sheria kuliko kova

    hamjui ndio maana hata mungu hakuwapa nafasi ya Kova

    Za mwizi ni 40
    Sweka vibaka na wala rushwa wooote

    Nilishawahi kuibiwa kwa mtindo huo japo sio na Muro ila kwa style yake

    Funga manyang'au hayo
    Wanalitia aibu Taifa
    Kama weka ndani woote
    Hata watetezi wake weka ndani
    Ni fibaka tu woote

    ReplyDelete
  26. Matapeli wa bongo wanamiliki mpaka mihuri ya Ikulu,Jerry aangalie asije akajiingiza kwenye kesi nyingine Mhuri wa juu Mzinga Morogoro, chini Mzinga Upanga,halafu kwa asiitoe siku alipozungumza na waandishi?

    ReplyDelete
  27. Ankal wewe pingu yako iko wapi au umeshaitumbukiza chooni?
    Na kigun chako mbona kila siku unawahug watu na ze mikono lakini wala hatukioni au wewe unakiweka kwenye miguu

    Watanzania raha sana ...kuwa na pingu ni kosa???????Jamani kuwa na gun mimi naona ni hatari kuliko pingu...

    Au kwa vile watanzania waogaoga tu wakiona pingu basi wazania mtu police huyo?

    Angekua ana kitambulisho cha police na pingu ningewaza mara mbili mbinu yake ilikua nini lakini kuwa na pingu tu basi kosa la jinai iiiiii???Mhhhhh

    Hivi hata camouflage clothing bado wanakataza tanzania watu kuvaaa? Mhhhh Bongo tambarare

    ReplyDelete
  28. wewe unayeuliza pingu mbona wewe una panga na kisu na sime na mkuki na glass, chupa, misumali, asprin, ddt vya nini na vyote hivyo hujui ni silaha? unaristi ya vyote hivyo? Tatizo watanzania wengi hawajui haki zao ndiyo maana maswali ya kijinga yanaulizwa watanzania wengi hawajui hata kujizuia kwa tahadhari yaani self defense ndiyo maana maaafa yakitokea wana kimbilia kuangalia badala ya kukimbia...shule iliminywa hata walioenda shule wanatumia ujinga wa watanzania wengi kuwafanya wote wajinga... wakati umefika watanzania kujua haki zao...
    xyz

    ReplyDelete
  29. no comment tatizo ni kwamba siku hizi MWENGE hauchomi umekuwa kama joka la kibisa enzi za sokoine na mwalimu hakukuwa na haya

    ReplyDelete
  30. Jerry ulikosea kidogo ungemwambia KOVA katika mgao huo wewe ungempa kama kilo tatau hivi usingepata hayo matatizo yote.Pole sana ila MUOSHA UOSHWA !!!!!
    "dont stop till we get enough".

    ReplyDelete
  31. aisee hii nomaaa...duh

    pingu ni kwa ajili ya mapenzi jaman

    ReplyDelete
  32. jerry angekua my husband wangu ningempiga marfuku hizi kazi za kudhalilishana na MAJARIBU ya kiasi ichi

    jamani my jerry mwaaa

    ReplyDelete
  33. Isei Jerry wewe kuwa kamujanja mie ninakabunduki kangu na pingu pia lakini kwa IQ ya mapolisi wa kibongo hawawezi kuzifahamu Pingu zangu sababu ni CABLETISER mafundi wa it they know what kifaa iam talking about next time uwe na cabletiser kutowa lawama ya polisi wasiojua sheria wako mudau mujanja wa muji

    ReplyDelete
  34. WATANZANIA TUNAPENDA SANA KURUKIA MAMBO. KABLA YA KUJADILI HILI JAMBO JARIBU KUJIULIZA IWAPO UNAFAHAMU YAFUATAYO:
    1. SHERIA.
    2. FACTS ZA KESI YENYEWE.
    3. MTU AITWAYE MURO.
    4. WENZAKE NA MURO.

    SUBIRINI KUSHANGAZWA.

    ReplyDelete
  35. Lakini katika majibu yake Waziri Mkuu Pinda alionyesha ugumu wa swali hilo akisema: "Hili suala lingekwenda mahakamani, jibu lingekuwa rahisi kweli." Akaongeza:"Labda niseme kwanza kwamba, binadamu alivyoumbwa ni kiumbe mwenye mapungufu mengi tu, hata kama angekuwa ana sifa nyingine zote, tukubali tu kwamba atakuwa na mapungufu. Waziri mkuu anayo; Hamad anayo; kwa hiyo na waandishi wa habari vile vile wanayo mapungufu yao kama binadamu." Alisema ndio sababu ziliwekwa sheria, kanuni na taratibu ili kusaidia kufanya mambo kwa kuzingatia sheria na kanuni. "Sasa yaliyompata Jerry... niseme tu kwamba kama binadamu na kama mtumishi mwingine yoyote, ni jambo ambalo linawezekana kabisa. Yale anayotuhumiwa yanawezekana yakawepo, vile vile yasiwepo," alisema Pinda. "Ndiyo maana kwa sababu hiyo inabidi uchunguzi ufanyike, tena wa kina ili kuweza kubaini ukweli wa yale wanayomtuhumu ni kiasi gani na kiasi gani si kweli."

    Hata hivyo alisema tatizo ni namna jambo hilo lilivyoanza kushughulikiwa na vyombo husika vya usalama na Jerry mwenyewe. Alisema wote wamekimbilia kwenye vyombo vya habari na kujenga picha tofauti kwa wananchi. "Tatizo ninalolitapa, Mheshimiwa Hamad, ni pengine namna jambo hili lilivyoanza kushughulikiwa... tumekimbilia kwenye vyombo vya habari sisi tunaochunguza, na yeye kama mtuhumiwa ametafuta vyombo vya habari na kuvitumia. Kwa hiyo sasa ujumbe tunaowapa wananchi kwa ujumla unaweza ukatuchanganya sana. "Kwa hiyo mimi rai yangu ni kuwa uchunguzi fanyeni kama mnavyofanya uchunguzi mwingine wowote. Utakapofikia mwisho, itajulikana kama ni kesi ya kwenda mahakamani au hapana," alisema Pinda.

    ReplyDelete
  36. Samahani, labda sielewi vizuri sheria za Tanzania, lakini hivi kuwa na pingu ni kosa? Nauliza hivi kwa sababu hapa Marekani unaweza kununua madukani, hata zipo za watoto kuchezea. Ila pingu (handcuffs) hapa watu wanazitumia hasa kwa ajili ya vitendo vya mapenzi (Bondage lovemaking). Hebu wasechi hao wazungu wanaotua Bongo si ajabu wengine wanazo.

    ReplyDelete
  37. WATANZANIA - PINGU SIO SILAHA NA HAIPO KATIKA AMUNITION AND FIREARMS ACT YA TANZANIA WALA NCHI NYINGINE

    PINGU SIO SILAHA ILA NI WAZI KUWA SIO KITU CHA KAWAIDA MWANANCHI ASIYE POLISI AU MAGEREZA KUWA NAZO.

    ASKARI WA ULINZI WA BINAFSI WANAZO PINGU.

    SIO KOSA MTU YEYOTE KUMILIKI PINGU KWANI PINGU SIO SILAHA.

    KAMBA YA KAWAIDA INAWEZA KUWA PINGU ILA PINGU ZA MURO ZILIKUWA SPECIAL.

    PINGU PIA HUTUMIWA NA RAIA WA KAWAIDA KATIKA MICHEZO HASA MICHEZO YA KIMAPENZI

    HIVYO KOVA KACHEMSHA NA NDIO MAANA JERRY MURO HAWEZI KUFUNGULIWA MAKOSA YA KUMILIKI PINGU KWANI HAKUNA SHERIA INAYOKATAZA

    KOVA KAUNDA TIMU YA MAPOLISI KUTAFUTA KIPENGELE CHOCHOTE KILE ATAKACHOWEZA KUMBANA NACHO MURO. WATU WANAO JUA SHERIA NI WANASHERIA - KAMA ATTORNEY GENERAL NA SIO MAPOLISI.

    MSHISHANGAE KOVA AKAJA NA MPYA - RISITI YA JERRY NI FAKE? NA MZINGA NAO WAKADHIBITISHA NI FEKI - HII INAWEZA KUSUKWA KWANI MZINGA PIA WANAONA NOMA KWA SUALA HILI. MIMI NADHIBITISHA RISITI YA MZINGA NI HALALI NA JERRY HAWEZI KUTOA RISITI FEKI KWA POLISI WAPELELEZI.

    WATANZANIA PINGU SIO FIREARM. SIO SILAHA NI KAMA KAMBA.

    PINGU SIO SILAHA SIO FIREARM

    ZINDUKENI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...