Kwaya ya Gestheman ya Kanisa la Moravian wakiwatumbuiza viongozi wa serikali , dini na wananchi waliokuhudhuria sherehe ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya majengo ya Mahakama Kuu kanda ya Sumbawanga , mkoani Rukwa leo. Sherehe hiyo ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa , Daniel ole Njoolay (hayupo pichani
JK akijadiliana jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Augustino Ramadhani (kushoto) na Spika wa Bunge, Samwel Sitta wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu jiji Dar leo.
Mkuu wa wilaya Kigoma John Mongela (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu wa mkoa Kigoma wakiongozwa na hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa huo Emanuel Mrangu (wa kwanza kushoto) na Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Kigoma, aliyekaa kulia David Ngunyale leo huko Kigoma.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hongereni mahakimu wa Kigoma kwa kuadhimisha Law Day! Nakuona hapo Mheshimiwa Demi Nyakunga mnyalukolo umetoka chicha! All the best! - Mama wa Kimara.

    ReplyDelete
  2. Demi nyakunga kweli kigoma imekupenda mnyalukolo maana naona umechana vibaya mno labda utupe siri ya mafanikio mzee!!!hongereni sana kwa kuendeleza libeneke la sheria mungu awajalie mafanikio mema kwa kazi zenu ngumu mazee!

    ReplyDelete
  3. Jamani, ongezeni basi majudge, pale Mahakama ya kazi. Nchi nzima eti wapo wawili tu. ni aibu. Hivi ankal Michuzi unalijua hilo? Eti nchi nzima majudge 2. Kesi zinakaa pale miaka na miaka. Watu wanakufa hawajalipwa haki zao!!

    ReplyDelete
  4. waheshimiwa mr Devid ngunyali na bwana demi nyakunga punguzeni uzito bwana miili hiyo inahitaji mazoezi angalieni hakim hatakiwi kuwa na kitambi bwana!!mnajitahidi sana kuchapa kazi muendelee kuwa waaminifu hivyohivyo kwa serikali yetu ya jamhuri ya muungano wa tanzania!amen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...