Asalaam aleykum Bwana Issa Michuzi na wadau wote wa blogu ya jamii.

Kwa niaba ya wadau wote wa familia yetu natoa shukrani kamili kwa wadau wote waliotoa ushirikiano ufaao wakati wa mkasa wa barabarani uliompata ndugu yetu aliyekuwa anaendesha toyota corolla.Ushirikiano ulikuwa ni mkubwa sana kuanzia kwa dereva wa Fuso aliyeamua kusimamisha gari yake baada kuona matatizo yaliyojitokeza kwa dereva wa Corolla.

Baada ya tukio raia wema kwa ushirikiano na askari wa JWTZ-Lugalo waliwahi kutoa msaada wa awali na kuhakikisha usalama wa gari na mali zote na majeruhi alifikishwa hospitali kwa wakati ufaao na kupokea huduma maridhawa kutoka kwa madaktari na wauguzi.

Ndugu,jamaa na marafiki kutoka pembe zote za jiji walianza kumiminika wakiwa na salaam za pole na maneno mazuri ya faraja pale hospitalini na nyumbani bila kusahau simu na sms.

Kwa kuwa katika lugha ya Kiswahili hakuna fungu la maneno wala sentensi ya kuonyesha hisia za shukrani kutoka katika papachi za moyo zaidi ya kusema asante,naona fahari kusema ASANTE SANA.

Wenu kwa staha;
Ray Ephraim Ndewingiya Njau
Dar es salaam Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Tanzania si tunaendesha upande wa kushoto ama?sijaelewa vizuri hii ajali ilivyotokea.anyway,poleni wahanga.

    ReplyDelete
  2. Lakini na wewe upande huo wa lori ulikuwa unafuata nini? Ajali zingine zinazuilika. Tuwe waangalifu barabarani.

    ReplyDelete
  3. Ndugu Njau ni furaha kubwa kusikia kuwa ndugu yenu aliweza kupona katika ajali hii na umeonyesha uungwana kutoa shukrani kwa wote waliosaidia na kuwajulia hali. Swali dogo: je unafikiri kuna lo lote zuri tumejifunza kutokana na tukio hili baya ambalo unaweza ku-share na wanajamii?

    ReplyDelete
  4. Badala ya kushukuru tu, tafadhali apologise kwa mwenye lori kwa kumfuata huko, kumwaribia lori lake na kumpotezea muda wake.

    Tatizo la Tz ndo hili, unawezakuwa wewe ni dereva mzuri kabisa, unafuata sheria za barabarani vizuri, uko upande wako wa barabara lakini atakufuata kichaa mmoja huko huko na kukuua. Kwa kweli hivi tunavyopumua muda huu basi tu Mungu anatusaidia. Ni wengi mno hawakuwa na kosa barabarani lakini walifuatwa tu na kuchinjwa na walevi wa aina hii.

    Maisha ni muhimu jamani. Uhai hauji mara mbili. Ni mara moja tu. Ukimuua baba au mama au dada au kaka au mtoto unaiachia familia machungu makubwa. Kuna watu wanashindwa kuendelea na shule kwa sababu baba au mama kachinjwa kwa stahili hii. Maisha yao yanakuwa yameharibika kabisa kwa sababu ya kichaa chako barabarani. Ukiwa barabarani hebu fikiria madhara ya uendeshaji wako mbaya. Tujirekebishe.

    ReplyDelete
  5. wakati mwengine watu msiwe mnalaumu tu barabara zetu za bongo wote tunazijua kuwa ni oneway na isitoshe pia ni nyembamba so mtu ukiwa una-overtake ni lazima utanue kulia inawezekana mwenye corola pia alifatwa huko kushoto kwake ktk jitihada za kujitetea akakimbilia kulia..mimi sikukuwepo kwenye hio ajali na wala simtetei mwenye corola lkn tusikimbilie kuwahukumu kwanza watu

    ReplyDelete
  6. si vibaya pia ndugu njau akatueleza kwa maneno yake, kuliko kuendelea kubuni maelezo, ilikuwaje? yawezekana alikuwa anataka kujitoa mhanga mabomu yakakataa kulipuka,

    ReplyDelete
  7. Ku-overtake kunafanyika pale tu kunapokuwa na usalama. Tusihalalishe uhuni unaoendelea kwenye barabara zetu. Km hujakaa nje utafikiri nchi nyingine zina barabara pana tu. La hasha! Hata Ulaya kuna barabara finyu lkn watu wanafuata sheria. Tena kwenye barabara finyu ndio unatakiwa uwe mwangalifu zaidi kuliko kwenye pana. Wee vipi bwana. Nyie ndo mnawafuata wenzenu kwenye sight zao halafu mnawawashia taa kana kwamba ni haki yenu mpishwe.

    ReplyDelete
  8. HUO NI UZEMBE NA KUTOKUWA MAKINI...ULIKUWA UNAKIMBILIA NINI? WATU KAMA HAWA TUNAO WENGI SANA HAPA DAR NA WANABOA ILE MBAYA. POLE TUNAKUPA LAKINI LAZIMA TUKUCHANE KIDOGO....KUAMBIANA UKWELI NDIO BUSARA.....

    ReplyDelete
  9. Wanopita wenzao kwa kuovertake na kuwawashia taa kisha kuchomeka wanakera mno, Huyu Njau na wengine wneye tabia kama hii hasa vijana wenye age za 20-40 vigali vyenyewe vya wadada zao vya mkopo wajuaji na ni wajinga sana wataanza kukutukana wakati yeye ndo anamakosa atakunyoshea kidole kimoja cha kati ukimbania kana kwamba hajafanya lolote baya. Ahcheni tabia zenu chafu bwana. Kuweni wastaarabu ukiona umechelewa kubali tu laa utabaniwa kama alivyo baniwa Njau mfe pungue wapumbafu nyie.

    XYZ

    ReplyDelete
  10. yani mdau kalikali na xyz
    hahahahahaaa,,,ni tabia ya kinyani sana kumbe tuko wengi tunaiochukia
    me sielewagi kabisaaa

    ReplyDelete
  11. Kwa ujumla kakangu alipata matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wake wakati akiwa kwenye anaendesha gari yake.Namshukuru sana dereva wa fuso kwa kuonyesha ushirikiano ufaao na familia yetu wakati wote wa matatizo.Siwezi kulaumu mchango wowote wa mawazo ila nashukuru sana kwa maneno mazuri ya faraja kutoka wanajamii.Kumbukeni hakuna uzembe wowote wala makusudi ndani ya aksidenti hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...