Tangu kuripotiwa kwa taarifa kuwa mwandishi Jerry Muro amekamatwa kwa muda na kuwekwa chini ya ulinzi kwa 'tuhuma' za kupokea rushwa ya shilingi za Kitanzania milioni 10, kisha taarifa kubadilishwa kuwa anatuhimiwa kwa kukutwa na pingu (nyara za Serikali), na baada ya kumsikia mwenyewe akizungumza, nimetafakari na kujiweka katika nafasi yake kwa sasa na kujiona nipo katika hali ya wasiwasi, woga na kukosa imani na hata usalama wa uhai wangu kuwa hatarini.

Nafahamu fikakuwa ni mapema kuzungumza kuhusu suala hili, lakini wakati mwingine mambo huhitaji uharaka kuliko kusubiri hadi yakaharibika kabisa. Inabidi kulizungumzia ili kutoa ushauri kwa marafiki wa kweli wa karibu, ndugu na jamaa wa Jerry katika kufikisha mawazo binafsi.

Jerry anahitaji kupata mapumziko: Kikazi, anahitaji kutuliza akili ili aweze kuwa na ufanisi. Kimwili, anahitaji kutulia ili kupevusha fikra ili kujiepusha na mkanganyiko wa mawazo (frustration) unaoweza kusababishwa na kuwaza mambo mengi na mazito kwa mkupuo.

Jerry anahitaji marafiki jasiri: Anahitaji marafiki jasiri na walio tayari kupambana wakati wowote, hasa kwa wakati huu kuliko wakati mwingine wowote. Amekuwa na maadui wengi kuliko marafiki kutokana na kazi yake.

Jerry anahitaji washauri wachache makini: Washauri wanapokuwa wengi, ni vigumu kutilia maanani na kufuata ushauri unaotolewa, hivyo watu wachache wenye ufahamu au katika fani ya ushauri wanaweza kumwelewesha umuhimu wa kutulia, kupumzika na kujipanga upya.

Jerry anahitaji kuwa mkimya kwa sasa: Si vyema kwake kuendelea kuongelea suala hili hasa baada ya kuwa limeshafikishwa katika vyombo vya sheria ili kuchukua mkondo wake. Ni kweli kuwa mambo ya kusingizia yanaudhi na hayavumiliki lakini vile vile upande wa mashtaka unaweza kuwa na sababu ya kuuthibitishia umma au kuufanya umma uamini kuwa Jerry alitenda uhalifu. Mambo haya yanahitaji wahusika wa kitaalamu zaidi, ni vyema Jerry akawapata wataalam wa nje na ndani kwa ajili ya kupambana na suala hili.

Jerry anahitaji kusafiri: Asafiri si tu nje ya mkoa wa Dar Es Salaam, bali nje kabisa ya nchi. (Hii itategemea kama ana ruhusa ya kufanya hivyo kutokana na yanayomsibu). Anahitaji kupata muda wa kutosha wa kumwezesha kufikiri vyema namna ya kukabiliana na tuhuma zinazomhusu kwa mujibu wa sheria na haki.

Sipo tayari kusema kuwa Jerry apunguze kasi ya mapambano aliyoianza, la hasha, nadhani kama amejitoa muhanga kwa kazi hii ili kuendeleza mapambabo, basi atakuwa tayari kwa lolote ila kama ilivyo vita nyingine yoyote, lazima upange mashambulizi kwa makini ukiwasoma wapinzani wako mbinu zao na jinsi ya kuzishinda. Ndiyo maana bado ninasisitiza kuwa, Jerry anahitaji mapumziko.
Kwa muda mfupi ameonyesha ukomavu na kutoa mwanga katika uandishi tafiti (investigavite journalism), ila nipo tayari kusema kuwa Jerry anahitaji kufahamu kuwa maji aliyoyavulia nguo kuyaoga ni ya kina kirefu, yenye mawimbi makali ndani ya ziwa pana sana.
Ndani ya ziwa hilo wapo wanaofurahi kuogelea na Jerry lakini katika hao pia wamo wanaomvizia ili kumsokomeza kichwa katika maji marefu ili azame, akose pumzi na ikibidi afilie mbali.
Jerry ameonesha mfano mzuri sana kwa kufichua maovu kwani ndicho tunahochitaji sana nchini Tanzania ili kuweza kumulika wala rushwa, wabadhirifu wa mali ya umma na wakandamizaji wa raia.

Huu nimtizamo binafsi na ambao ningeutumia au ningemshauri mtu yeyote aliyekumbwa na hali kama hii.

Nimeandika haya kufuatia video niliyoiona hivi punde kuhusu Jerry alivyozungumzia kadhia aliyokumbana nayo akiwa mikononi mwa polisi. Video yenyewe ipo hapa (bofya hapa) katika ukurasa wa Video.
Subi/www.wavuti.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. HII INATHIBITISHA FIKA KUWA WAKUBWA WANAHUSIKA KATIKA KUHUJUMU WANANCHI WA KAWAIDAKWA MTINDO WA EUSHWA KWA UROHO WA PESA NA MAENDELEO BINAFSI, KWA NINI WACHUKUWA HATUWA YA KUMFANYIA HIVYO JERRY? HAINGII AKILINI HATA KWA MTU AMAYE NI TAHIRA. WANAMKAMATA BAADA YA YEYE KUTOWA ADHARANI VITENDO VYAO VYA RUSHWA NA UOZO NA KUSHINDWA KWA LEADERSHIP. KWA NINI HAWAKUFANYA HIVYO KABLA? HII INAONYESHA JINSI GANI NCHI ZETU ZA AFRICA KAMWE HAZITALETA MAENDELEO KWA WATU WOTE KWA KASI MPYA, NI MAENDELEO KWA WAO WACHACHE KWA KASI MPYA YA KUWAIBIA WANANCHI WA KAWAIDA KWA MTINDO WA RUSHWA, WABUNGE TUMEWACHAGUWENI KUTUNGA SHERIA ZETU NA KUTUTETEA SISI WANANCHI WA KAWAIDA WALALA HOI TUNAWAOMBENI MLIKEMEE HILI HASA WALE WA UPINZANI NAJUWA WA CCM HAWATALIONGELEA HII KWA KUWA NAO WAMO PIA KATIKA MTANDAO HUU WA KUJILETEA MAENDELEO BINFSI NA SI YA WOTE, HII NI AIBU AND SHAME ON YOU POLICE, ACHENI KUONEA WATU WA KAWAIDA NI AIBU INAYONUKA KABISA.

    ReplyDelete
  2. Tatizooo polisi wetu wamejaaaa elimu duni ambayoooo wanashindwa kufanya maamuziii ambayooo yana mpangilio wa ukweli..polisi wa kitanzania sheria hawajui kabisa mimi ni mojawapo wa victim ambayee nilikumbwa na tatizoo la mapolisi .Mafundishoo yanahitajika ya mara kwa mara kwa polisi ya sheria ili raia wawe na haki na polisi kuongezewa mishahara ili walizike na wanachokipata ..wapi Adam mwaibabile nyota yake walishaizima siku nyingi..Said Mwema huko wapi?iyooo ndioo kasumba ya polisii iliyopo tangia utawala wa Mwinyii mpaka sasa kuhusu rushwaa ndio msingi wa maendeleo kwao

    ReplyDelete
  3. Swali kubwa ni kwamba vijana watashirikije katika kujenga taifa hili. Vijana wenye maarifa ndiyo mstakabali wa taifa lolote duniani. Kazi za kukimbiza mwenge na kuandaa matembezi ya mshikamano,kusifia viongozi sifa ambazo hazina kichwa wala miguu hazitainua taifa. Serikali zetu zinadidimiza vijana huku zikilaumu wazungu kuwa ndiyo sababu ya umasikini wetu. Vijana waliosoma wanapigwa na wasiosoma wanapigwa mitaani na askari wa jiji.
    Hii inasikitisha sana. Serikali iepuke Kunyanyasa watu wake kwa misingi ya udini na ukabila. Hili litaangamiza umoja wetu.

    ReplyDelete
  4. mi nahisi jery anahitaji kugombea urais sasa au ubunge atapata tu,Lakini mh! inawezekana kuwa mtego tu umefeli lakini alikua kwelia akale Rushwa kwani Pingu kazipata wapi?.na kwa sheria gani na huyo mtu alijuaje kama kuna pingu Kwa jerry au walifatilia wakajua anatembea nazo SASA SI ANGEOMBA TU KAZI OFISI YA TAKUTURU SIJUI NDIO KATUKURU AH ! WATAJUA WENYEWE

    ReplyDelete
  5. Subi unajishusha kwakuwa nakujua na nakuheshimu sana.
    Acheni kutoa hukumu hata kama umesikia maelezo yake mwenyewe. Ungetegemea angekili alichofanya?
    Jifunzeni kwa Mrema alivyovuma kumbe alikuwa anapokea pia.
    Mkapa pia alikemea rushwa kumbe mla rushwa mkubwa.
    Wage is a millionare. Hakuna taasisi yoyote ya kumpa vijipesa atengeneze mtego.
    Bongo kila mtu mla rushwa. Na waandishi msijifanye mnajua kuteteana. Tunajua kuwa mnatisha watu kupata rushwa.
    Pia hamuwaandiki hata mastaa wa bongo flavor hadi aawape pesa.
    Bongo inanuka
    Nawewe unatetea rushwa
    Waandishi wanaleta majungu kwenye ukweli
    TAnzania inanuka hadi sisi tulioko nje HATUTAKI KURUDI BONGO INANUKA
    No matter nani anasema nn
    Wage alimfanya the same afisa wa PCB kule Iringa
    He is a strong guy
    Keep it up Wage no matter wat
    NOBODY IS ABOVE THE LAW
    Funga waaandishi hao

    ReplyDelete
  6. Mnageuza ukweli kuwa majungu
    Sweka rimande hao
    wanapoteza disiplini ya taifa
    Kila mtu mla rushwa
    The country is stinking

    ReplyDelete
  7. Kaazi kweli kweli!

    Ukifuatilia kwa makini na undani utaelewa kabisa Jerry ni mtu wa system (Usalama wa Taifa au Takukuru), angalia hata maneno ya Kova mara mwanasheria wa Serikali kafanya nini, na ndo maana anajenga hoja ya kuwa kwa usalama wake Jerry asiseme kitu. Pia angalia Jerry alivyosema kwa kujiamini kabisa kuwa kumiliki kwake silaha huu ni mwaka wa nne na hajaanza leo, na pia kwa kusema Kova sio Polisi akimaanisha kabisa kuwa kama kweli Kova angekuwa ameiva katika hilo basi angeweza kumtambua Jerry mapema kabisa bila hata ya kukurupuka na kuutangazia umma kuwa anamiliki silaha na pingu kwa maneno hayo kwa mtu muelewa utajua tu kuwa kova yanamgonga muda huu! Na ndo maana Kova amechemka kwa kutomgundua mapema kuwa Jerry inawezekana akawa mtu wa system. Kwa upande wa Kova yeye kama kiongozi hapaswi au hawezi kuita Press Conference kwa taarifa za juu juu (anatakiwa apate full information na ndio aseme kitu kilicho kuwa kimekamilika) na ndo maana siku ya pili akakosa la kuongea kuhusu rushwa ambayo siku ya kwanza aliita waandishi wa habari ila siku ya pili case ikabadilishwa na kuwa anamiliki Bastola na Pingu. Lakini katika hili maelezo ya Muro hayapo ila yapo ya upande mmoja tu , na ndo maana narejea tena mtazamo wangu wa mwanzo kuwa Kova amestuka na kuona huyu kijana ni wa system.
    Sasa kwa hili la kuita Press Conference inawezakana Kova alitegewa mtego au bomu na vijana wake bila yeye Kova kuliewa na kuliingia kichwa kichwa na kuitisha Press Conference, si unajua tena vijana wa siku hizi, inawezakana Kova anawabana vijana wakajipanga, sasa usije ukashangaa hii issue ikamgeukia Kova mwenyewe na vijana wake wakaonekana washindi! Ni mtazamo tu.
    Kitu cha pili ambacho ni cha muhimu zaidi, mawasiliano yote yaliyofanyika yapo kwenye makampuni yanayotoa huduma za simu kwa hiyo mwisho wa siku hayo yote yaliyosemwa na Jerry alipigiwa simu na huyo mtu hapo City Garden yatajulikana na hayo ya Kova ya kusema kuwa kuna sehemu ambayo hawezi kuitaja nayo yatajulikana. Ila hii ngoma itakuwa ngumu kwa Kova mtaniambia wadau! Jerry atawashinda na wala msihofu kwa hilo.
    Ankal comments zangu unazibania sana, hii inakatisha tama tunapochangia na kuona comments chache zenye mtazamo chanya ndio zinazoonekana. Naomba usibanie.
    Pia ankal email address yako hatuifahamu tunakuwa na matukio mengi tu ila jinsi ya kuyatuma, ni vyema ikajulikana Ankal.

    Mdau, Kichali

    ReplyDelete
  8. Jerry anachohitaji ni kuwa mkweli kwasababu story yake inaacha maswali zaidi kuliko majibu. Ushauri wa kunyamaza sio ushauri wa busara kwenye jambo lenye public interest kama hili. Anyamaze ili iwe nini? Anachotakiwa ni kusema ukweli kama ulivyo. Kwenye video hii anaonekana kama msanii tu, anaonekana ana-act sana. Jerry pia tunamjua tangu chuoni. Alikuwa yuko tayari kusingizia kifo cha ndugu yake ili kukwepa responsibility pale chuoni. Maisha haya ya umaarufu feki ambao hauna misingi ya kweli huu ndio mwisho wake.

    Mimi nina maswali kadhaa kwako Jerry:

    1. Unasema “kuna mtu kanipigia simu kuna press conference”. Mtu huyo ni nani? Je, press conference wanapigiwa waandishi moja kwa moja au inapigiwa taasisi ndipo inatuma mwandishi? Utaendaje kwenye press conference bila kujua imeitishwa na nani?

    2. Unalielezeaje suala la vitu vya huyo mzee wa Bagamoyo (miwani) kukutwa kwenye gari lako?

    2.Jerry, wewe ni mwandishi mzoefu. Hebu niambie press conference hata moja katika historia ya nchi hii iliyofanyika kwenye hoteli ya City Garden? Na hata ukienda kwenye press conference, inakuwaje unabaki kwenye gari eti unamtafuta kwa simu “mtu” aliyeitisha press conference. Si unaingia ukumbini na kuwakuta waandishi wenzako?

    3. TBC kwa kawaida kwenye matukio inatuma cameraman na mwandishi. Kama ni press conference, mbona hukwenda na cameraman? Je, wakubwa wako TBC walikuwa wanajua hiyo press conference uliyoitwa?

    4. Ukiangalia video ya maelezo yake kuanzia mwanzo hadi dakika 0:58, Jerry unasema hujui kwanini gari lako limezungukwa na polisi. Ghafla, kwenye dakika 0:59, unasema “siwaelewi, rushwa ya milioni 10?”. Sasa hapo unatuchanganya, utawaulizaje hilo swali wakati hadi dakika hiyo ulikuwa hujui kwanini polisi wamekuzunguka? Halafu baadaye, kwenye dakika 1:31, ndio unawauliza “nielezeni mlichonifuatia hapa”. Kama ulikuwa hujui, mbona kitu cha kwanza ulichowauliza ilikuwa “rushwa ya milioni kumi?”

    5. Lakini pia, baadaye, kwenye dakika 5:47 unabadilisha sequence ya story na kusema polisi walivyozunguka gari lako wakamwita mzee na kukwambia kwamba huyu mzee anasema umemwomba rushwa. Sasa hivyo ndio ilivyotokea swali lao kwako kwamba “nielezeni mlichonifuatia hapa” linatokea wapi?

    6.Pingu unayotembea nayo kwenye gari ni ya kazi gani?

    7.Huyo “Mzee wa Bagamoyo” (Mhasibu) ulishapata kumuona au ndio ulimuona kwa mara ya kwanza pale City Garden? Ulipata kuwasiliana naye au hapana?

    8. Kuna tatizo gani Kova kusoma vifungu vya sheria?

    ReplyDelete
  9. Nakubaliana na ushauri huu kwa Bw. Muro,
    Bw Muro ni mtuhumiwa mpaka sasa. hajathibitika kutenda hilo kosa. Anayohaki ya kuwa kimya hadi atakapotoa ushuhuda wake mahakamani. Kuongea hovyohovyo kutampeleka pabaya..thats a free advise. Kaa kimya tafuta mwanasheria then akutetee kisha ukishinda kesi unadai fidia kibao.Kesi za dizaini hii ni deal sometimes.mahakama tu ndo itathibitisha ukweli au uongo wa tuhuma.
    Nadhani kaka Muro kama ni mwandishi ajuaye sheria atafunga mdomo na si vyema kulumbana/kumshutumu hata Kamanda wa Polisi...yeye kama mtumishi wa Umma kumshambulia mtumishi mwingine wa Umma pia si sahihi

    ReplyDelete
  10. Huu ndio wakati muafaka wa JK kujizolea umaarufu. Rudi toka kwenye kikao cha AU halafu timua akina Kova na vigogo wote walio nyuma ya hili sakata la Muro. akiweza hilo, atakuwa amefunika vibaya.

    ReplyDelete
  11. Kwa aliyetowa ushauri wa bure kwa Jerry, first and for all, Jerry has not committed any felony, there will be no DA that would prosecute this embarrassing and stupid case. The DA will be out of his mind to do that, and should loose his Job - Just as the commissioner of Police here needs to resign. So, stop scaring the shit out of this guy, this shows how Tanzanians can easily be frightened to fight for their rights. Tanzania needs to get rid of having police prosecuting cases; they are ignorant of the law period. How do you hire a form six lever and put him to prosecute cases? It is just hard to believe what a stinky justice system we have.

    ReplyDelete
  12. Waswahili huwa ni wepesi sana kudanganywa Duniani. Ati kwa sababu ni maarufu ndiyo mnamwona hawezi kuwa mualifu! Waalifu wote huwa ni wa namna hiyo siku zote. Ngoja muone mambo sasa

    ReplyDelete
  13. Jamani nimesikiliza maelezo ya Kova kwenye TV na nimesikia maelezo ya Jerry vile vile kwenye TV. Picha nilioipata ni kama ifuatavyo:1. Ama Kova kadanganywa na makachero wake au naye ni sehemu ya njama ya kumdhuru Jerry. 2. Ama Jerry katunga uwongo wa kujitetea au anasema kweli.
    Conclusion: Polisi wameamua kumnyanyasa Jerry. Kesi ya rushwa iweje wao waifuatilie ilihali TAKUKURU ipo lakini isihusishwe? Hapo pana hila. La pili, kwa nini kesi iende kwa DPP wakati kesi nyingine nyingi tu haziendagi huko? Kova anajitia kuijifanya kuwa anafuata sheria na anatka haki itendeke kumbe ni mwongo. Anajua fika DPP hawezi kuikubali hiyo kesi. Lakini lengo lao watakuwa nao wamemdhalilisha Jerry mbele ya jamii. Ukitazama body language ya Kova ni ya kilaghai. Du. Mwongo mwongo!! Huo ndio mchezo wao polisi.Ninamshauri Waziri Masha aifuatilie hii kesi la sivyo IGP na timu yake wawajibishwe. Shame on You Kova! SHame on IGP and Shame on YOU Tanzania Police. Media Council of Tanzania wekeni wakili wa maana kumtetea Jerry. Lo aibu sana.

    ReplyDelete
  14. Jmani tuwe wakweli na wawazi. hasa kwa wanahabari wenzie. kuna mtu asiyemjua jerry Muro na utaratibu wake wa kulazimisha mishiko? mi nimewahi kufany akazi nae na nimeshuhudia alipokuwa analazimisha mtu atoe mshiko amasivyo habari yake haitatoka au ataigeuza iwe mbaya(negative) katika hili nachelea kusema tusiseme sana tukajikuta tunaumbuka. jerry si safi kihivyo. tuwe makini

    ReplyDelete
  15. Da'Subi umlichonena ni cha msingi na tena kilichoainishwa kwa umakini na upendo kwa kijana alieshafanya kazi stamilivu na ya ushupavu kama Jerry, anahitaji sana kufata hayo uliyosema ili asije kuishia kupata msongo wa mawazo na kupoteza dira njema na mwelekeo thabiti ambao nadhani wengi wetu tunaukubali kwa kazi zake sadifu na yakinifu ambazo ameshazifanya mpaka sasa,
    Labda ni vigumu kuhukumu moja kwa moja mpaka sasa lakini swala kubwa lisilofichika ni maelezo ya kujikanganya mno ya jeshi letu husika ambayo kwa hakika yanaacha maswali mengi pasi majibu na hasa pale tunapoona mtu akizungumzia swala hili nyeti akiwa na bashasha tele kana kwamba ni neema iliyokuwa ikisubiriwa,

    Kwa hakika maji uliyoyavulia nguo ni kina zaidi ya kile labda uluichokifikiri, fuata ushauri maridhawa kama ulivyoainishwa na Da'Subi, kutolizungumzia suala hili kwa sasa ni uamuzi sahihi ili kutojiingiza kwenye mtego wowote,

    Vita hii ni ngumu labda tena sana lakini kujipanga ipasavyo na kujua mbinu za upambanao si tu jawabu bali hatua stahilivu,

    Tanzania bila uonevu kwa hakika INAWEZEKANA

    Matukio OleAfrika Aranyande Chuma

    ReplyDelete
  16. JERRY NI SAWA NA WATANZANIA WENGINE KAZI YAKE HIMFANYI AKAWA SI MHALIFU WALA HASHAWISHIKI, JERRY KWA BAHATI NZURI HAKUWA PEKEE WAKATI KOSA TENDWA LILIPOFANYIKA WAPO WANGINE NAO WAMEKAMATWA HIVYO SI SAHIHI KUJARIBU KUMSAFISHA JERRY NA KUWAACHA WENZAKE KWA SABABU TU HATUWAJUI NA HATUJUI KAZI ZAO, MAHAKAMA PEKEE NDIYO ITAKAYOMSAFISHA JERRY NA SI VYOMBO VYA HABARI NA MAGAZETI HUU NDIO UTAWALA WA SHERIA.

    ReplyDelete
  17. Itabidi minimum entry of police officers wawe na B.Sc. Political Science au Sociology au LL.B. Polisi wa bongo kweli hawajui kupanga madili kama ya Maiko Skofild wa Prison Break

    ReplyDelete
  18. Acheni jazba, muulizeni pisto mchana ya nini; pingu na uandishi wapi na wapi. Acheni jazba wandugu.

    ReplyDelete
  19. Mimi ninaomba mnaomtetea Jerry na sisi tusiokuwa na majina tunapokamatwa muwe mnatutetea hivyo na MCT iwatetee wananchi ambao ni wajasiriamali wenu kwani ndio wanaosoma magazeti yenu, wakifungwa basi hamtakuwa na wasomaji na wasikilizaji na watazamaji wa vyombo vya habari. Lakini pia MCT mjue Jerry si mwandishi wa kwanza kudai au kutuhumiwa kwa kosa hilo na pia mnaotaka tuwe nyuma yenu kuwaunga mkono baadhi yetu tumewahi kudaiwa rushwa kwa vitisho vya kuandikwa vibaya.

    ReplyDelete
  20. Mimi napinga wanaosema kuwa watanzania wote wala Rushwa. Wanaotoa hoja hiyo wanautaarifa umma kuwa nao ni wala Rushwa na kama ilivyo kila mwizi anafikiri kila mtu mwizi. Na inaonekana wengi wanaosema hivi ni mapolisi. Inasikitisha kuona watanzania walio wengi hawana dhamiri (conscience). Hata wanapoona uonevu wanashirikiana ili kupinga ukweli. Ni dhahiri kabisa Jerry anafanyiwa mchezo mchafu. Tukiendelea hivi hukumu kwa Tanzania iko njiani! Mashuhuda mnaoshuhudia uongo hamuitakii mema nchi yetu!Mwogopeni Mungu watanzania!

    ReplyDelete
  21. Mimi napinga wanaosema kuwa watanzania wote wala Rushwa. Wanaotoa hoja hiyo wanautaarifa umma kuwa nao ni wala Rushwa na kama ilivyo kila mwizi anafikiri kila mtu mwizi. Na inaonekana wengi wanaosema hivi ni mapolisi. Inasikitisha kuona watanzania walio wengi hawana dhamiri (conscience). Hata wanapoona uonevu wanashirikiana ili kupinga ukweli. Ni dhahiri kabisa Jerry anafanyiwa mchezo mchafu. Tukiendelea hivi hukumu kwa Tanzania iko njiani! Mashuhuda mnaoshuhudia uongo hamuitakii mema nchi yetu!Mwogopeni Mungu watanzania!

    ReplyDelete
  22. jamani hapa nazani tusubiri mahakama.unaweza mtetea jerry kwa jambo usilolijua,kwa kweli mimi nilipoona pingu kwenye gari lake nguvu zote ziliniishia.bongo kwa sasa kumeshamili mitendo vya utapeli kutumia uandishi wa habari,inawezekana watoto wa mjini walimshilikisha wajameni
    michu na wewe una pingu

    ReplyDelete
  23. WEWE UNAYELEZEA MAELEZO YA JERRY KWENYE VIDEO HAYO MAELEZO HAYAKO KWENYE MTIRIRIKO WA TUKIO KWA VILE HAYO MAELEZO YAMETOLEWA BAADAYE NA JERRY ALIPOENDAGLOBAL PUBLISHER SI WAKATI WA TUKIO.

    PINGU NA BUNDUKI SI MALI YA SERIKALI WALA POLISI NINA MAANA POLISI WA TANZANIA HAWANA HAKI MILIKI YA VITU HIVYO MTU YOYOTE ANAWEZA KUWA NAVYO TU, KITU HATARI SANA HAPO NI BOSTOLA AMBAYO TANZANIA INASHERIA ZAKE ILI KUIMILIKI, NAHISI JERRY ALIFUATA UTARATIBU WA KUMILIKI BASTOLA, PINGU HAINA UTATATIBU WOWOTE ILI MTU AMILIKI KISU NI HATARI KULIKU PINGU LAKINI TANZANIA KISU MTU YOYOTE ANAWEZA KWENDA DUKANI AKANUNUWA NA KUTEMBEA NACHO OVYO NA ASIULIZWE NA MAMLAKA HUSIKA KAMA NCHI ZA WENZETU KUTEMBEA NA KISU HADHARANI NI KOSA LA KUFUNGWA JELA, KUHUSU MIWANI PIA HIYO NI HOJA NDOGO SANA KIWANDA KINACHOTENGENEZA MIWANI HIYO HAKIKUTNGENEZA MIWANI YA HUYU MZEE PEKE YAKE KILITENGENEZA MIWANI KIBAO HATA JERRY ANAWEZA KUNUNUWA, NA NI KAMA YA HUYO MZEE KWA NINI ALIACHA KWENYE GARI YA JERRY, BASI HII INATHIBITISHA WAZI KUWA KESI NI YA KUPIKWA, ALIPANGA NA POLISI AKAACHA MIWANI HUMO ILI IWE KUJA USHAHIDI, HIZO KESI ZA HAINA HIYO NI ZA MWAKA 47

    ReplyDelete
  24. Brother Michuzi mimi ninavyoona kwa mtazamo wangu ni kwamba ni mapema mno kuanza kulalamikia vyombo vya dola na serikali kwa ujumla,cha msingi ni wananchi tuwe watulivu mpaka hapo ukweli utakapojulikana maana kesi yenyewe ndio kwanza imeanza kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele ndipo tutakapojua ukweli zaidi kama ni kweli Jerry kaonewa basi atendewe haki la kama tuhuma dhidi yake ni za kweli basi sheria ifate mkondo wake kwa sababu huyo Jerry yeye si malaika ni binaadam kama walivyo binaadam wengine na makosa kwa binaadam ni vitu vya kawaida.
    Jambo lingine ni kwamba Jerry anaongea sana mpaka anapitiliza hiyo haiwezi kumsaidia sana sana inaweza kuwa ndio inazidi kumuharibia na kumuweka mahali pabaya zaidi mfano mzuri ni pale aliposema"Kova anasema amekuta pingu na bastola mbona hasemi mambo mengine aliyoyakuta!!!!????" hebu atufafanulie Kova alikuta mambo gani menfine?inaonekana kuna usiri mkubwa sana katika hii kesi. Wacha polisi wafanye kazi zao tusipende kulaumu kila kitu ina maana hao polisi hakuna jema hata maja wanalolifanya katika kazi zao???Anasema hawezi kumtapeli mfu milioni kumi,ina maana hao anaowaona yeye kwamba ni wazima anawatapeli zaidi ya hizo milioni kumi anazotuhumiwa nazo!!! Kijana kuwa makini katika maongezi yako jazba haziwezi kukusaidia.

    ReplyDelete
  25. hahaah huyo aliyeuliza kama michuzi ana pingu?kanichekesha hahaah

    ReplyDelete
  26. JAMANI MBONA TUNACHEKESHA?

    1) WEWE DA-SUBI, KAMA UNAFEELING KUHUSU JUSTICE, KWANINI USIMTUMIE UJUMBE HUO JERRY MWENYEWE, NA UKAULETA HAPA. ARE YOU SEEKING PUBLIC SUPPORT OVER MURO'S ISSUE, WHEN NO ONE OF US HAS EVIDENCE WHATSOEVER, ON WHO IS WRONG, AND WHO IS RIGHT?

    2) WHAT IF JERRY'S ALLEGATIONS ARE TRUE IN THE END OF THIS WHOLE DRAMA? ARE YOU GOING TO WRITE ON THIS BLOG TO APOLOGIZE FOR MANIPULATING US (PUBLIC)?

    3) KWA MAWAZO YANGU, HATA KAMA JERRY HAJAHUSIKA KWA HILI, BASI KUNA JAMBO KUBWA SANA ANALOHUSIKA NALO. LAKINI AMETAJWA KWENYE ISSUE AMBAYO USHAHIDI SIYO WA WAZI.

    HAMNA MTU MSAFI AKAANZWA TU HIVIHIVI NA JESHI LA POLISI, HASA HAWA WAFANYAKAZI ZA 'BLUE COLOR JOBS". VIBAKA NDIO HUONEWA MARA NYINGI.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...