Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. ndio mwalimu alifanikiwa katika rushwa lakini tusisahau yeye pia ndo chanzo cha umasikini wa leo kwa watanzania,maana sera zake za ujamaa ziliudidimiza uchumi wa nchi,ameondoka madarakani watanzania wako hoi,hali ilikuwa mbaya mno,vitu vya kawaida vilikuwa kama anasa,na baadae akaja kutuchagulia mkapa kwa lazima ambaye ndo aliirudishwa rushwa kwa kiasi kikubwa.

    ReplyDelete
  2. hii longo longo yote hapa anampigia kampeni mkapa,ambaye ndio baba wa rushwa nchi hii,mwalimu ungekuwa kweli mwerevu ungemjua mkapa mapema,maana alikuwa mwanafunzi wako.kaila nchi yote

    ReplyDelete
  3. kila rais wa tz,ana mazuri na mapungufu yake,kwa nyerere rushwa na umoja aliweza kuzitekeleza kwa uzallendo kabisa,kwa hilo hatutakusahau baba,kwa uchumi mzee ulikuwa zero,mzee ruksa aliweza kuubadilisha uchumi wa nchi hii kwa muda mfupi sana,na alifanikiwa kuimarisha democrasia ya tz,lakini kipindi chake ndo rushwa ilianza polepole,mkapa yeye aliujenga uchumi vizuri pamoja na mipango mizuri,sema alifanya ufisadi wa kutisha,kubinafsisha mashirika ya umma kwa bei ya kutupwa,madini,nyumba za serikali na mabenki,JK mpaka sasa anaendeleza mipango mizuri pamoja na uchumi unaokuwa,sera safi,mfumo wa sheria na haki,pia ajira zinazidi kwa tz walio wengi,tatizo ushkaj.

    ReplyDelete
  4. NYERERE NDIO KAITENGENEZA RUSHWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA. NDIO MSINGI WAKE ULIKUWA MKAPA.

    ReplyDelete
  5. What a legend...

    ReplyDelete
  6. Kimsingi ukikubali kununuliwa wewe zuzu, huna tofauti na mnyama asiyefikilia!!

    ReplyDelete
  7. Wakati wako hodari sana wa kupinga Rushwa na Riba,ila Ubabe wa kuchagua unaowataka uliweka mbele,Ulimkataa MADEVU PIA NA JK,Mwinyi kiboko ila matabaka yaliinuka MASKINI AKAWA MASKINI KABISA NA TAJIRI AKAWAPITA WENZAKE KWA MBALI KABISA,MZEE MKAPA ALIKUA VITISHO TU KWA WAPINZANI UFISADI NA KILA BALAA LA RUSHWA,JK POA KIDOGO KUPAMBANA NA ALOYALETA MKAPA ILA NA YEYE SAFARI ZA NJE ZIMEZIDI MI NAHISI NI RAISI WA KIMATAIFA NA SIO WA BONGO,TATIZO LA TZ KILA KIONGOZI ANAKUJA KUFUTA UCHAFU WA ALOMTANGULIA NA ANAANDAA UCHAFU WAKE KWA ANAEKUJA AUFUTE ALETE WAKE.MI NAHISI JK AKIMALIZA MUDA WAKE APEWE TENA WAZIRI WA MAMBO YA NJE( NURAMO )

    ReplyDelete
  8. JAMANI, WEKENI KWA WINGI HIZI HOTUBA PALE YOUTUBE.COM

    ReplyDelete
  9. nyerere hata TV ilikuwa anasa, ukiwa nayo u, we mnyonyaji, kabaila, mirija ikatwe etc, sasa hata hii video leo hii tungeiona kweli mzee wetu?

    ReplyDelete
  10. Nyerere ni alikua na mapenzi makubwa na nchi yake. Kama binadamu yeyote, kila mtu anakosea pahali fulani.
    Nyerere ameangushwa au alizungukwa na wanafik, kitandawili kinasem; "KIKULCHO KINGUONI MWAKO", ndio walimzunguka, si wote lakini.
    Nyerere alikua ni msema ukweli, si mwizi, na wala si mnafik kama tunavyo yaona leo.
    Kuna viongozi ambao hakuwataka, kwa sababu alijua ni majambazi, lakini baadaye waka tawal tu, KWA NINI???
    Umoja wa akili ni nguvu jamani, pande zote. Kwa mazuri ni nguvu, huleta maendeleo, kwa mabaya, ni nguvu vilevile, huleta umasikini mkubwa, tukumbuke.
    Umoja wetu leo uko wapi?? Jibu lake ni UTAJIRI KWA WACHACHE TU.
    Naishia hapo

    ReplyDelete
  11. Zaidi ya kuangalia Habari za dunia, na habari chache za maana, TV imejaa UPUUZI na kusabisha vijana wetu Kupumbaa na kuiga mambo yasiyo ya kiasili. Hao Mawaziri wenye majumba kila mahali, na mahospitali na mashule, ndio wanao ua nchi zaidi. Je ni sawa hiyo, kwa nchi ya kimaskini??? Kama alivyo nena Baba wataifa, hizo hela wamezipata wapi???

    Nyerere alijua hiyo. Asili ya kiTanzania inatoweka kwa kuwa watu hawana maarifa ya kuchagua zuri na lisilo. Huku hatuko, na Kule ni Hola vilevile.

    Mwacheni mzee wa watu alijitahidi sana. Ndio maana wachache tumebakia na UTU na heshima aliotufundisha.

    ReplyDelete
  12. Duh...Kumbe Nyerere alikuwa camedian? Clips za Baba wa Taifa zote ni nzuri na zinachekesha unaona ata raha uzidi kuckiriza. Kwa mtaji huu nasema Nyerere na Ze Camedi, Nyerere zaidi afu ndo wanakuja ze camedi..From Mshangiliajio wa Drajani

    ReplyDelete
  13. TV kujaa UPUUZI ni tatizo la watayarishaji, siyo tatizo la TV yenyewe. sasa unataka kusema hata hii video ya mwl nyerere akiongelea rushwa nayo ni UPUUZI?? ikiwa wamiliki wa vituo vya matangazo hawataki kutuonesha asili ya kiTanzania, wanatuwekea vikaragosi vya kichina na wapi sijui, wee unategemea nini? TV ni sawa na hiyo computer uliyotumia kuandikia ujumbe weko anony, ukitaka kuona UPUUZI ndani ya mtandao po kinao sana, lakini ukitaka kunufaika kwa kufanya mambo makubwa hilo nalo linawezekana. sawa mzee alijitahidi sana lakini kuna mapungufu kibao alitukwamisha, hasa kwenye sekta ya habari

    ReplyDelete
  14. Ankal Michuzi naomba hotuba nzima ya mwl. nyerere alipokuwa mbeya mei mosi.

    Niwekee link ni download.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...