daladala lililogonga kichwa cha treni ya TAZARA leo sehemu za Tandika Yombo jijini Dar na kusababisha kifo cha mtu mmoja (anahofiwa kuwa ndiye dereva) na kuacha majeruhi 26, ambao 21 kati yao wamelazwa hospitali ya Temeke na watano wamekimbizwa Muhimbili kwani majereha yao ni mkakubwa zaidi.
sehemu ilipotokea ajali hiyo leo ambapo daladala likitokea Tandika sokoni liligonga kichwa cha treni ambacho inasemekana dereva hakukiona wakati kinakuja hadi dakika ya mwisho. Hata hivyo sehemu hiyo haina alama yoyote kama kuna reli inakatisha mbele kama ilivyo kawaida.
mmoja wa majeruhi akiuguzwa na nduguye hospitali ya temeke leo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hiyo ndiyo Tanzania...ambapo viongozi wanadhani kutembelea mataifa ya ulaya KUOMBAOMBA ndiyo kutatatua COMMONSENSE problems kama hizi za alama za usalama barabarani, wakati gharama wanazotumia kwenda na kurudi huko ULAYA zingetosha kabisa kuondoa matatizo haya madogomadogo.....

    ReplyDelete
  2. POLENI SANA wafiwa. Nasikitika kuwa nilipanga kuandika juu ya hatari hii mapema lakini imetokea kabla sijafanya hivyo. Juzi Jumamosi asubuhi kama saa tatu hivi nusu kichwa kingine kigonge saloon moja. Mimi nilikuwa kwenye gari lingine kilicho niokoa ni kelele za mshangao wa wananchi. Kwani gari na enjini ya traini zilipishana kwa nusu inchi hivi. Nami nilikuwa kwenye mkumbo. Tatizo hakuna alama na watu wamejenga vibanda hivyo hakuna"visibility" uonekano. Pia niliambiwa kuwa honi ya treni hiyo ni mbovu. Naomba yawekwe matuta kwani kama mtu ni mgeni ni wazi wataumia wengi

    ReplyDelete
  3. POLENI WOTE MLIOKUMBWA NA MKASA HUU.HAYA NDIYO MATATIZO YA KUTOKUWA NA FLY-OVER KATI YA BARABARA NA RELI NA BARABARA MOJA NA NYINGINE.WADAU NAOMBA KUFAHAMU NI KWA NINI VIONGOZI WETU WENGI WANAPENDA KU "PICK NOSE"WANAPOKUWA WAKIONGE,KAMA HUYO AFANDE ALIVYOFANYA,SIYO TU NYUMBANI HATA WANAPOKUWA KWENYE INTERNATIONAL STAGE?JE,HAYA NI MAADILI YA KITANZANIA?

    ReplyDelete
  4. Poleni sana familia na ndugu walioguswa na ajali hiyo

    Mungu awe nanyi

    ReplyDelete
  5. nasikia treni kutokana na uzito wake na na magurudumu ya chuma na barabara ya chuma ule msuguano huwa unatengeneza nguvu ya umeme, sasa kama gari inavuka reli huwa inavutwa(umeme wa gari una kuwa neutral) kwahiyo hapa gari inakosa nguvu/inazimika na ndipo balaa linapotokea mfano yarabi salama dodoma. Hizi ajali zinatokea nyingi sana tz sema huwa hazitiliwi maanani sana, tulioishi maeneo ya reli nadhani tunaelewana
    ushauri=ajali hizi ni ngumu sana kuzizuia,reli zisikatize barabara za watu au magari,pia ni hatari kwa usalama wa treni mfano hujuma nchi nyingi reli huwa imepigwa fensi.

    poleni wahanga

    ReplyDelete
  6. Hivi ni mimi tu peke yangu nimesikia officer wa polisi anasema ajali imetokea saa nne na dakika sitini na tano?

    ReplyDelete
  7. Hao watoto hapo wananitia huruma kwa kweli. Nini future yao, miaka yetu ingekuwa kwanini hawapo shule.

    ReplyDelete
  8. Bongo tambarare kweli
    Ofisa wa polisi hayupo serius kabisa kutoa taarifa, bali yupo busy kuulizia ...”sawa...”? sijui anaulizia usawa wa namna gani badala ya utoa taarifa

    ReplyDelete
  9. tunawaombea mungu majeruhi wote wapone haraka na kumuombea mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi, amin.hivi hakuna maswala zaidi ya kuulizwa huyu muheshimiwa polisi, isipokuwa idadi ya watu, hivi hawa wanahabari wamelewa kama polisi mwenyewe nini?

    ReplyDelete
  10. Wakati mwingine haya mambo yanatokea kwa uzembe. Juzi nilikuwa maeneo ya reli inayokatiza banda la ngozi, along Pugu/Nyerere road. Magari yasiyopungua matano, yote yalikuwa yanapita kasi ili kukiwahi kiberenge kilichokuwa kinakatiza. Kiberenge kilikuwa kinapiga honi za mfululizo kuashiria ujio wake, lakini wenye haraka zao nao walikuwa wanachochea magari yao ili kuwahi kupita! Kwa maoni yangu, huu ni ujinga usio na kipimo.

    All in all, nawatakia uponyaji wa haraka majeruhi wa ajali hii.

    ReplyDelete
  11. heeeee siamini treni na gari?afu izo nyumba apo mbona ziko pembezoni ivo mwa reli?

    dakika 65?saa ya wapi hii

    poleni wahanga wote Mungu awatie nguvu

    ReplyDelete
  12. Dakika 65 hazipo mheshimiwa!!halafu unatoa taalifa utadhani unauliza?duh!!!Eti lakini deleva huyo,,lakini kwenye ajali hiyo! anaongea kitu unafikili hana uhakka,,,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...