Habari ya kazi Ankal,
Pole na majukumu mazito ya kutuhabarisha ndugu zako watanzania tuishio kila pembe ya ulimwengu huu.Mimi ni mfuatiliaji sana wa globu yako, imenihabarisha mambo mengi ajabu..
Siku za hivi karibuni nimepata kuona ukitangaza majumba na mali kadhaa zinazouzwa, ningependa kuwataarifu watanzania kupitia blogu yako kuwa mimi na vijana wenzangu tumeamua kuanzisha tovuti mahususi kwa ajili ya kuzitangaza nyumba, majumba, viwanja, mashamba na maghala ili kurahisisha mfumo soko wa bidhaa na huduma zake.
Ndugu Michuzi naomba kupitia Blogu ya Jamii kuutaarifu umma juu ya huduma zetu.Tovuti yenyewe ni.
Pia kumbusha umma yakuwa vigezo na masharti vitazingatiwa wakati wakutumia tovuti.. rejea kichwa cha habari "terms of use"
Natanguliza shukrani za dhati kabisa.
Michael Francis(muanzilishi wa tovuti tajwa)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Joni mashaka najua kasoma hii kacheka.....

    ReplyDelete
  2. nimeitembelea hii web,mwanzo inaonekana inavutia,lakini haina info za kutosha,
    mi nawaona wezi tu hawa jamaa,inakuwaje wanatuonyeshea majengo kwa nje tu,si watuonyeshee na ndani.
    Mdau Cologne,Germany

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. ovyoooo! nothing is in there, i saw one plot fro sale USA 150,000 on your dreams

    ReplyDelete
  5. Are u charging 1% to list a house? That is $10,000 on a $1m home, naona kama $10K ni ghali kulinganisha na options nyingine za magazeti yenye good circulation.

    Kama nimetafsiri vibaya nisahihishe.

    (US Bloger)

    ReplyDelete
  6. "TUENDELEZE JAMII/TUVIPENDE VYA KWETU"

    THAMANI YA NYUMBA $400,000.00

    1)UMEME/MAJI WA MGAO (GHARAMA YA GENERETOR/KISIMA)

    2)MAJAMBAZI/VIBAKA/WEZI/MATAPELI (WANASAIDIWA NA POLISI WASIOTHAMINI KAZI/KIAPO CHAO)

    3)FOLENI(UNAAMKA/ENDESHA KUANZIA SAA KUMI USIKU ILI KUWAHI KAZINI SAA MBILI ASUBUHI MAILI "20-40 KWENDA KAZINI").

    4)VIWANGO/UBORA WA VILIVYOTUMIKA KATIKA KUJENGA/UJENZI WA JENGO

    5)MOTO/AJALI (INSURANCE)MNUNUZI ANALINDWA/THAMANI YA ALICHONUNUA.

    6)TATHMINI/THAMANI YA KWELI YA NYUMBA.

    ReplyDelete
  7. Ukiingia kwenye hiyo website kuna link inayosomeka Nabaki Tanzania or whatever.. hii link ina trojan tafadhali jihadhari nayo....!!!!

    ReplyDelete
  8. Bwana mdogo nimekutembelea huko kwako a good start lakini unahitaji ufanye maboresho makubwa.

    So do that and then come back us. We will give it another go.

    Goodluck!

    ReplyDelete
  9. be careful virus detected!February 04, 2010

    mdau hapo juu, mimi nilicheki hii web site mchana shortly after nikakuta laptop yangu inafurumuka na kusema kuna virus wamekuwa detected, na nakumbuka neno trojan! sikuelewa imekuwaje, nikazima, then nikawasha tena, nikaendelea kutumia, so jamani vipi mnatuwekea kitu chenye virus? Michuzi kuwa mwangalifu sana watu wanakupa linki zao hakikikisha wanakuhakikishia ziko salama, hii imenishtua sana hivi ntapeleka ikachekiwe, its not fair kama ndo kufanyiana kihivo.! jihadharini ambao hamjapita huko, this is serious!

    ReplyDelete
  10. HII NYUMBA YA $2,500 INAUZWA UA INAPANGISHWA AU GHARAMA ZA UDALALI?

    ReplyDelete
  11. Hiyo Plot ya Bilioni MOJA KAriakoo mmeiona wadau. Je ni TSHS ama ZDollar. Ama Kweli Bongo yaenda mbele.

    ReplyDelete
  12. kumbe wanaweza. leo nimetembelea huko, nimekuwa nikiwafuatilia. kumbe wanaweza jamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...