Yanga imeaga mashindano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kufungwa goli moja na timu ya FC Lupopo katika mchezo uliochezwa katika jimbo la Katanga nchini DRC.
Goli lilifungwa na mabeki wa Yanga baada ya kubabatizwa na washambuliaji wa FC Lupopo katika Dakika ya 89 ya mchezo hivyo Yanga imetolewa kwa magoli 4-2 ya agrigeti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Tangu lini Yanga ikashinda bila kubebwa na serikali? timu pekee tuliyonayo hapa nchini ya kuwakilisha ni Simba. Na huu siyo utani wa jadi bali ni fact

    ReplyDelete
  2. ndiyo tumefungwa sasa wewe furaha yako nini.. mpaka itwe mdebwedo...mbona na wewe sikuizi habari za livepool umezichunia sikuizi kwa kuona aibu..ukuliona...hilo..Amefungwa chelsee 4 sembuse sisi cha ndimu.....

    ReplyDelete
  3. Historia imeonyesha kwamba Yanga huwa wanapata shida sana kwenye mechi zisizo na marefa wazalendo

    ReplyDelete
  4. halafu mnataka kocha anayeifundisha yanga apewe kufundisha timu ya taifa klabu tu imemshinda anayokaa nayo karibia mwaka ataiweza stars na kumfunga shehata mpaka hapa asiwemo hata katika mchujo ameshashindwa

    ReplyDelete
  5. Ushindi wa Yanga na furaha yao ni pale wanapofanikiwa kutwaa ubingwa wa kiloko na hivyo kuwazuia Simba kushiriki katika mashindano ya kimataifa kuipeperusha bendera ya Bongo.

    Angalia sasa, wakirudi watasema sasa tunakonsentreti kutwaa ubingwa ili kuliwakilisha taifa katika mechi mbili tu hapo mwakani.
    Hawa Yanga hawaaa, ... we acha tu.

    ReplyDelete
  6. hata mimi ni mpenzi wa yanga ukweli utabaki palepale simba ndio club pekee yenye ushindani mzuri na vilabu vya njee lakini sisi wasindikizaji, yanga oyeee

    ReplyDelete
  7. Candid ScopeFebruary 28, 2010

    Timu inapoliwakilisha taifa si tena mwendo wa ushabiki wa kitimu kama hata timu ngeni toka nje hupata mashabiki isivyo kawaida

    Tatizo kubwa ushindani wa soka tanzania ni kuona simba na yanga nani kamfunga mwenzie. Timu nyingine wanachofanyia mazoezi ni kuifunga yanga au simba ndo waonekaba umecheza.

    Wachezaji wa timu nyingine wanachofanya ni kuonekana wachezaji wazuri ili kusajiliwa timu za yangu na simba.

    Wachezaji wa siku hizi ni wale walio wengi waliookotwa mitaani wakichezea mipira ya matambala. Ile michezo ya Umiseta imekufa. Michezo ya shule na vyuo ndo chimbuko la wachezaji wazuri waliokulia mazoezi tangu utotoni. Ndo maana wanaojaribu soka la kulipwa ulaya wanarudi bila kufaulu ni kwa sababu hawafundishiki. Hata ukileta kocha wa timu ya taifa ya ufaranza au uingereza kiwa wachezaji wa bongo kazi bado palepale
    Tukumbuke kocha wa sasa wa taifa anavyokazania kukuza vipaji toka vijana utotoni kwani kishaona tatizo la wachezaji wa kufunza mpira ukubwani hawafundishiki.
    Kwetu simba, yanga ndo soka letu limeishia hapo

    ReplyDelete
  8. Let's blame Maximo. Kosa la Maximo hili!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...