Askari wa jeshi la Uturuki wakimsindikiza JK kwenda kuweka shada la maua katika kaburi la mpigania uhuru na mwanzilishi wa Taifa la Uturuki na pia Rais wa kwanza wa taifa hilo leo jijini Ankara.Rais Kikwete yupo nchini Uturuki kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Rais Abdullah Gul wa Uturuki.

JK akiweka shada la maua katika kaburi la mpigania uhuru na mwanzilishi wa taifa la Uturuki Mustafa Kemal Ataturk jijini Ankara Uturuki Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akimkaribisha JK ofisini kwake jijini Ankara, Uturuki
JK akiweka saini katika kitabu cha wageni kwenye jumba la makumbusho ya historia ya taifa la Uturuki ambamo amezikwa mpigania uhuru na mwanzilishi wa taifa hilo Mustafa Kamal Ataturk ambaye pia alikuwa Rais wa kwanza wa taifa hilo.
JK akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kitaifa (State Baquet) iliyofanyika katika ikulu ya nchi hiyo jijini Ankara, Uturuki usiku huu. wa tatu kulia ni mwenyeji wake Rais wa Uturuki Abdullah Gul na kushoto mke wa Rais wa Uturuki Hyrunisa Gul.Kulia ni Mama Salma Kikwete.
Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Dr.Mary Nagu na Waziri wa nchi wa Uturuki Bwana Zafer Caglayan wakisaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Uturuki na Tanzania katika hafla iliyofanyika katika ikulu ya nchi hiyo jijijni Ankara Uturuki leo asubuhi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa

    Tanzania machete massacre 'sparked by goat theft'

    Funerals have been held in Tanzania for 17 people hacked to death on Monday night, amid rumours the massacre was sparked by the theft of goats.

    The sister of one of the victims told the BBC she believed the killings were revenge after three suspected goat thieves were chased and killed in 2005.

    The dead were mainly women and children from the northern Mgaranjabo village.

    The BBC's Erick Nampesya says hundreds of grief-stricken mourners attended the burial ceremony.

    One of the mourners, 21-year-old Nyasiden Kawawa, said: "I lost my father, mother my five siblings and a child of my aunty."

    Ms Kawawa, who is married and lives away from her father's home, added: "They called, but when I reached here, I found them hacked to death."

    At the funeral, church elder Gasper Msenya called for tolerance.

    "Mothers, you have a responsibility," he said.

    "These acts are carried out by men - your husbands and your sons. Educate them because such acts anger God."

    ReplyDelete
  2. Nimependezwa na jinsi rangi za blauzi na skafu za Dr. Nagu zilivyomachi na tai ya huyo waziri wa Uturuki.

    ReplyDelete
  3. Yule mpambe wa rais lazima alipigwa kipupwe cha nguvu maana wenzake wote wamevaa makoti makubwa yeye yuko na gwanda lake la jeiwi ambalo halifai kwa mazingira ya baridi.

    ReplyDelete
  4. mdau hapo juu nakubaliana na wewe kabisa huyo bodigadi wa jk alipigwa na kiwinter kisawasawa sometimes awe anavaa kawaida sio kila dakika na migwanda tuuu ebu protokol fanyeni namna huyu mlinzi wa raisi asiwe anavaa migwanda hadi anaboa ah!

    ReplyDelete
  5. MIMI BADO NA HAWA MABODIGADI WA RAIS WETU....HIVI NI LAZIMA KUVAA HAYO MAGWANDA?????????

    NAONA KILA SEHEMU HATA IKIWA SEHEMU YA STAREHE LABDA RAIS KAALIKWA SHEREHE FULANI WATU WOTE WAMEVAA SUTI LAKINI UTAMUONA BODIGADI NA MIGWANDA YAKE

    NAFIKIRI WANGEFANYA KAMA WENZETU WENGINE MAMBO KISASA BODIGADI ANAWEZA KUVAA KAWAIDA TU KAMA SUTI NA SIO LAZIMA AJIWEKE NA MAGWANDA NA AKAKAMAE NYUMA YA RAIS LIKE THAT.....

    kijiushauri changu nawewe ankal nanihii unaweza kuchangia mada hii

    ReplyDelete
  6. tumwambie riziwani akamwambie babake kuwa yule bodigadi wako wananji wasema asiwe anavaa migwanda kila siku anaboa awe anavaa wakati wa sikukuu za kitaifa tu full stop yani hadi rais akisakata rumba na yeye nyuma yake na migwanda hadi hainogi mambo ya kiobama yananoga sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...