watu watatu wanasemekana wamepoteza maisha jana jioni wakati basi hili la shabiby kuvamia lori lililokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara. kwa mujibu wa abiria waliokuwemo ajali hii imetokea baada ya dereva kushindwa kurejesha basi upande salama wakati yakifukuzana na basi lingine. habari kamili mtembelee mwenyekiti wa kijiji Maggid Mjengwa aliyefika muda mfupi baada ya ajali hii kutokea 


Ianzishwe sheria madereva kama hawa wapewe kitanzi...Ukisababisha ajali watu wakaumia adhabu iwe kifungo cha maisha na ukiendesha vibaya ukaua nadereva apigwe kitanzi...
ReplyDeleteinasikitisha sana maana tunapoteza saana maisha ya watu....rest in peace kaka Nsajigwa tokana na ajali hii....Family ya Kina Mwakapala poleni sana...Krom
ReplyDeleteHALAFU NDIO WAMILIKI WA MAMBI WANAKATAA SPEED GAVANA.. WATATUMALIZA SANA. SERIKALI INATAKIWA IWALAZIMISHE. KWANINI WANAKKATAA GAVANA? NIA YAO NDIO HII YA KUFUKUZANA TUU NA KUWAUA RAIA WASIO NA HATIA. INASIKITISHA SANA.
ReplyDeleteRuvu hadi Chalinze, Njia tatu pale Mwidu, mteremko wa Mdaula pembeni ya shamba la katani, Bwawani na Kingolwira, ni maeneo ya ajali. Why?
ReplyDeleteMdau naomba nichangie kwenye ili,jana nilikuwepo wakati ajili hii inatokea,maana sisi tulikuwa kwenye basi la mbele ambalo dereva wa basi lililogonga lori alikuwa anajaribu kuliovertake,alishafanya hivyo kabla baada ya ruvu dereva wa gari nilimokuwa akampisha apite.Sasa mara ya pili alipojaribu tena akachemsha na kuliparamia lori ambalo nalo lilikuwa linatembea kwa busara za dereva wa lori akakata kushoto kutembelea kwenye lane ya pembeni ambayo kawaida yanapita magari yanayopanda polepole.
ReplyDeleteKosa ni ladereva wa basi alilogonga
Jambo lingine wadau ambalo ni muhimu kuweka makakati,ni masuala ya uokoaji,tulimshauri dereva wa basi tulilopanda asimame ili tuwape msaada majeruhi alisimama,kimbembe kilikuwa kuwatoa majeruhi waliokwama/kubanwa na viti na mifuko ya simenti kutoka kwenye lori,vifaa vya kukatia vyuma hakuna,gloves hakuna watu wanaogopa kushika damu,nilishuhudia watu wakiwaangalia majeruhi bila msaada,wengine ulijitahidi,kuwatoa lakini wenye magari wengine waligoma/kataa kutoa lift kupakia majeruhi ambao wangewaishwa wangeweza kupona na sio kupoteza maisha,wengine wamekatika miguu inaning`inia sijawahi kuona lakini hakuna msaada wa maana waliopewa.
Kuna wezi pia,moja ni abiria tuliekuwa nae kwenye basi letu,huyu yeye sio binaadamu maana alishangilia baada ya kusikia kishindo cha ajali,akamwambia dereva twende zetu mchina kajiingiza mwenyewe kwennye lori,nilimshangaa,dereva akawa hajuhi la kufanya ndipo tulipo mshauri asimame,sasa jamaa huy huyu akaiba begi la majeruhi sijuhi marehemu,akawa amalazimisha basi liondoke kumbe watu wamemuona.Kufika moro watu wakawaarifu trafick mara gari limesimamishwa jamaa akakutwa na na begi tena la kike,kuna nguo za kike na hati ya kiwanja,anapesa zaidi ya 1 milioni,akadai ni zake alishahesabu,lkn iligundulika kuwa hata nauli hakuwazo walimpa tiketi ya msaada,balaa tupu.inasikitisha.
Magari yalazimishwe kuwa na gloves,dawa za kuiauvujaji damu, na pia kuwe na ambulance zinaegeshwa kwenye vijiji vya aribu kutoa msaada haraka
UNAONA UJINGA WA MADEREVA WA BONGO? ETI WALIKUWA WANAFUKUZANA WAKATI WAMEBEBA RAIA!INASIKITISHA SANA. NGOJA NISIONGEE MENGI, MANA NENO AJALI LIMEKUWA MAARUFU KULIKO WIMBO WA TAIFA.
ReplyDeleteSerikali, serikali, serikali..... Bunge, Bunge, Bunge.....Hivi haiwezekani kabisa maderva kama hawa kuwaficha jela wakafia huko? Mmoja mmoja mpaka watakwisha tu. Adhabu za sasa za TZS 20,000/= hazina maana yoyote. Kila siku tunasema sheria zimepitwa na wakati, lakini nani anatakiwa kuzi-update? Na ugumu uko wapi? Miaka nenda rudi... Sheria zilitungwa na binadamu na binadamu huyo huyo ana uwezo wa kuzibadilisha.
ReplyDeleteUzembe na Ujinga wetu utatumaliza.Halafu utasikia mijinga inasema ooh Mungu kapenda,Ooh Kazi ya Mungu haina makosa,OOh barabara hii ina majini.Upumbavu mtupu.Hawa madereva na wamiliki wa haya mabasi wanatakiwa wafungwe na wafirisiwe.Wananchi wanatakiwa waelemishwe haki zao ya kwamba wanaweza kuwashitaki hawa wamiliki na madereva wanaosababisha vifo na ulemavu.Ma-lawyer wa TZ wanafanya nini,kwa nini wasielemishe wananchi juu ya jambo hili? Halafu bongo mnataka barabara za juu-juu na madaraja ya nguvu,vitu hivi vikiwepo bongo si kila siku watu watakuwa wanakwisha.
ReplyDeleteMwidu iko Mkoa wa Pwani na sio Morogoro. Mpaka wa mikoa wa Morogoro na Pwani unatenganishwa na mto Ngerengere eneo la Bwawani (Pwani) na Gwata (Morogoro)
ReplyDeleteNchi za wenzetu wanaojali usalama wa abiria ni nadra kusikia ajali ya basi kutokea katika kipindi cha miaka 10-2o. Tanzania tulipokuwa na mabasi ya kamata au ya shirika la reli usalama wa abiria ulipewa kipa umbele. Dereva kabla hajakabidhiwa bus alitakiwa aongozane na dereva mzoefu kwa miezi au miaka kadhaa mpaka awe mahiri.
ReplyDeleteLabda kwa sasa tungerudisha shirika la reli liwe na dhamani ya kusafirisha abiria hata kwa mabasi ili kuokoa maisha ya watu. Kama mabasi yote yanamilikiwa na shirika moja hakuna wa kumwonea wivu mwenzake ili kupata abiria zaidi.
Hata commuter bus zinazomilikiwa na serikali unakaa mtu kwa starehe na kujali ustaarabu wa abiria kuliko hizi za kiswahili kushindana kupata pesa kwa abiria.
Mabasi binafsi kazi kufukuzana kuwahi abiria wa mbele bila kuwa na hisia za usalama wa abiria walio nao ndani ya basi.
HIZI AJALI MPAKA LINI.. NASIKIA LIMEUA GIRLFRIEND WA MSANII WA BONGOFLAVA MADEE.. NIMESIKIA HIZI HABARI LAKINI SINA UHAKIKA ANZO LABDA WADU WAKOMFRIM
ReplyDeleteNasikia mmiliki wa basi hilo ametembeza mshiko ili habari hiyo isirushwe kwenye TV ingawaje inasemekana wanaohusika na kurekodi matukio katika vituo mbalimbali vya TV waliwahi kufika eneo la tukio cha ajabu habari hiyo haijaonyeshwa kwny Tv zaidi ya kwenye magazeti.Lengo ni kuwa eti ajali km hy ikioneshwa kwny TV watu watasusia kupanda basi hilo.
ReplyDeleteMdau