Chef Issa (kulia) akipozi na mshindi wa kwanza toka Uswisi
Mshindi wa kwanza toka Uswisi akipozi na mshindi wa pili toka Urusi Chocolate ya Mshindi wa Kwanza toka Uswisi
Chocolate ya mshindi wa pili toka Urusi
Chocolate ya Chef Issa iliyoshika nafasi ya tatu
Hii ilikuwa ni mashindano kwa ajili ya Junior Chefs (wa umri wa miaka 20-40) ya kutengeneza sanamu za chocolate yaliyofanyika katika Mji wa Intarlaken uliopo huko Switzerland katika kiwanda maarufu na kikongwe dunia katika utengenezaji wa chocolate bora kinaitwa Schuh ambacho kilianza utengenezaji huo toka mwaka 1818 kwenye milima ambayo haikauki barafu mwaka mzima na ndio kitovu cha bara la ulaya. Kiwanda hicho ni wakongwe na wanatisha na ni mabingwa duniani
ambapo wanafundisha kozi yao kwa miaka 4 ili uwe bingwa wa kutengeneza
chocolate aina zote.

Katika mpambano huo Chef Issa aliibuka kuwa mshindi wa tatu baada, akiwafuatia kinadada 2 mmoja ni raia wa Uswiss alieshika nafasi ya kwanza na mwingine ni raia wa Russia alieshika nafasi ya pili. Ukizingatia historia inaonyesha warusi ndio walikua wa kwanza kuanzisha taaluma hii ya utengenezaji chocolate kisha waswiss wakaiba utaalamu na kua mabingwa mpaka leo na wanakula chocolate si mchezo.

Washindi walizawadiwa vikombe na vyeti pia vya ushiriki na walikua jumla washiriki 50 toka pande zote za dunia. Chef Issa alipambana na kubahatika nafasi ya tatu ila anasema mhhh...hao kinadada kiboko.

Chef Issa anatoa wito kwa wazazi wawasomeshe watoto wao fani hii ya upishi akisema ni safi sana na inalipa kwa njia zote kujiajiri na kuajiliwa. Anasisitiza mtoto anapoonesha nia ya kujiendeleza kimasomo katika fani hii apewe kipaumbele ili tupate wataalamu wengi zaidi kwani hapa nyumbani nafasi nzuri zote zinashikwa na wageni ijapokua nasi tukisoma vizuri tunaweza zaidi yao.
Kufatilia mfululizo wa mafunzo safi ya
mpishi toka kwa Chef Issa nenda:
www.activechef.blogspot.com





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. hongera sana chef uko makini safi sana ila hiyo ya mshindi wa kwanza ipo kama shetani lol hata kula yataka moyo labda ulie gizani hongera manangu

    ReplyDelete
  2. Hongera sana kaka, Zidisha marogo utafika zaidi ya hapo.
    Kazi zako nazikubali na nafanyia vitendo nyumbani, sifa kibao chakula kikifika mezani.


    disminder.

    ReplyDelete
  3. hongera,lakini tunaomba utuoneshe hiyo award certificate inayo onyesha kwamba amekuwa mshindi wa tatu

    ReplyDelete
  4. mdau wa 1:17pm naona una roho ya kwanini bila sababu.sasa kama sio mshindi wa tatu wewe utapungukiwa na nini?

    ReplyDelete
  5. ISSA keki mbwa! astaghfilulaah!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...