zawadi za ze fulanzzz za globu ya jamii zimeandalkiwa kwa washindi watano wa kwanza wataoweza kutaja hapa ni wapi katika jiji la dar. unasamehewa kutaja jina kama hulijui ila angalau eleza hii ni sehemu gani na hiyo barabara ya vumbi inatoka wapi kuelekea wapi. mdau yeyote popote alipo ruksa. mwisho wa chemsha bongo hii ni jumapili saa sita usiku kwa saa za bongo. usipoleta anuani yako utakuwa umejitoa mwenyewe...
angalizo: wadau mliojishindia ze fulanazzz katika lile ingizo la mdau wa milioni 8 tunaomba mfanye subira kwani ze fulanazzz zimechelewa kutoka airport kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu. juhudi zinafanywa zipatikane wiki hii na kuanza kutumwa. anuani zote zimehifadhiwa, msikonde.
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Sasa we Mithupu mimi naishi Arusha nitajuaje sehemu hiyo ua jiji?? au zawadi ni special kwa watu wa Dar tu.. tuwekee za Arusha uone tutakavyozipatia

    ReplyDelete
  2. nazani hapo ni mbezi beach

    ReplyDelete
  3. MICHUZI HAPO NI UNAPINDA KUELEKEA MSASANI SLIPWAY, YANI NIKIANZIA KILIMA NYEGE UNASHUKA KONA YA KWANZA KUSHOTO MPAKA UNAKUTANA NA KONA YA KWANZA UNAIWACHA SABABU UNASHUKIA MSASANI KIMWERI ROAD KWAHIYO UNAPIGA KONA YA PILI KUSHOTO UNAKUJA NAYO NDIO UNAINGIA KULIA KWAUTIZAMO WA PICHA HAPA NI MKONO WANGU WA KULIA KWENDA SLIPWAY AU NDIO HOTEL YENU MPYA SIJUI TREE NINI. PAZI HIZO NYUMBA SI ZILIKUWA ZA SHIRIKA LA NDEGE? PAZI. HIYO NI MSASANI SI OYSTERBAY WALA MASAKI WANAVYOSEMA PAZI.

    ReplyDelete
  4. HAPO KIBANDA HICHO UNAINGIA KUCHUKUWA CHETI CHAKO CHA TB HAHAHAHAA KWA WALE WANAOTAKA KWENDA UENGEREZA LAZIMA WAPAJUE HAPO. MBEBA BOX. JAMES

    ReplyDelete
  5. MBEZI BEACH NJIA INAYOENDA GOBA
    ALIYEPIGA PICHA ALIKUWA MASANA HOSPITAL
    MDAU UK READING

    ReplyDelete
  6. kwa kuangalia fasta fasta hapo nafikiri ni maeneo ya Tabata Mawenzi (kimanga)hiyo barabara ya vumbi inatokea Tabata bima, hili eneo lipo karibu na kanisa la parokia ya Tabata Mawenzi (kimanga). Thats it, hope am right!!!

    ReplyDelete
  7. michuzi unajua bongo kwakweli imebadilika na inabadilika kila siku. hapo labda ni changanyikeni au mbweni ah. ila pnavutia sana kwakweli na inaonekana ni sehemu yenye viwanja ghali!!
    sasa kaka mimi hata kama nimekosea jibu naomba tu na mimi unitumie tisheti kaka. mimi ni mdau wa pajazzzz naomba kaka kama umekubali nikupe address yangu unitumie niwakilishe huku manake nilipo hapa mbongo peke yangu tu.email yangu ni mdauwapajazzznatitizzz@googlemail.com kama umekubali niambie tu hapahapa kwa kutumia comment then mi ntakuemail kukupa full address yangu ya hapa nlipo.
    mwisho kabisa nlikuwa nauliza vipi libeneke siku hizi mbona liko biased sana?? limenitenga sana nakuwa kama mkiwa kaka ,sasahivi stock nliyonayo ni ileile ya zamani kwahiyo unakuta narudiarudia mboga hebu fanya updatings kaka!!!
    ahsenti!!!

    Mdau wa Pajazzz na Titizzz.

    ReplyDelete
  8. MAENEO YA MSASANI. PICHA YA NYUMA NI KUSINI KWA JIJI LA DAR, KUSHOTO MBALI KWENE PICHA NI MAGHOROFA YANAYOJENGWA MASAKI MADUKANI. 0787747450

    ReplyDelete
  9. hapa masaki

    ReplyDelete
  10. Manzese Uwanja wa Fisi Hapo.

    ReplyDelete
  11. TEGETA KILIMAHEWA!!! pkipokola@yahoo.com, andaa ze fulanazzz hiyo haraka!!!

    ReplyDelete
  12. hapo ni maeneo ya msasani kushoto hvi ni kwenda slipway na ilo ni ileo hotel mpya cjui na hapo jengo kulia ni IOM

    ReplyDelete
  13. Hapo ni Masasani karibu na slipway, hapo kwa upande wa kulia ni office za IOM International organization for migration na pia Medical screening zinafanyika hapo especially TB screen kwa wanaonda kufanya UK visa application

    ReplyDelete
  14. Wanaojuwa wamepatia kusema Msasani yani watu wengi husema Slipway Masaki au Hizo Nyumba hapo Masaki si masaki, Masaki ni kule inakotokea hiyo barabara na wala Sea cliff si Masaki ni Msasani. tizameni hata Adress zao utaona Msasani.

    ReplyDelete
  15. hapo bila kukosea ni kwa MTOGOLE njia hiyo ya vumbi ukiifuata unatokea kwa kwa kina Mwajuma Kigoli na huyo aliye piga alikuwa Tandale..pale karibu na kibanda cha pombe yaaani kwa mama mwagamwaga

    ReplyDelete
  16. hapo n njia ya kwenda slipway kushoto kulia unaenda msasani kwenye mbyu ulokatika karibu na fitness center au msikiti wa zamani mdogo ulokua karibu na beach na ninjia utakayotokea tido. ally67@yahoo.co.uk. london

    ReplyDelete
  17. WOTE MMECHEMSHA. HAPO NI MBAGALA KIBONDEMAJI JAMANI. KARIBU NA KWA MZEE PAZI

    ReplyDelete
  18. Michuzi hapo ni Tegeta Kilimahewa. Ni kama kilimoeter 2 hivi kutoka tegeta stand kuelekea Kaskazini magaharibi mwa hiyo stand kuu ya tegeta. Hiyo barabara ya vumbi inaenda Kilimahewa.

    Tuma hiyo ze fulana ankal fastafasta.

    Mdau.
    USA/ex-tegeta tenant.

    ReplyDelete
  19. hapo arusha kwa loning'o.

    ReplyDelete
  20. Hahah hi si ni nyumba yangu wazee..!!!.Hii No. itakuwa ni ya dalali tu, ngoja nisuburi ataye tia timu hapa.

    ReplyDelete
  21. Hiyo picha kaka ni pale masaki kuelekea Slip Way, unakula kulia kama unatokea nyuma ya picha, kushoto ndio wanakotolea vyeti vya TB kwa wanaokuja kwa mama. Aliyepiga picha nahisi alikua kwenye gorofa lilikua linajengwa inawezekana limeshaisha, na usawa wa kati ya hizo gari mbili nyeupe kwenye kona kuna kiosk mi nishakula mtindi na keki hapo .
    This my email jhpkaloki@hotmail.com

    ReplyDelete
  22. Hapo ni Tegeta Kilimahewa.ckessy@hotmail.com

    ReplyDelete
  23. Hiyo picha imepigwa kutoka ghorofa moja iliyopakana na Slipway. Ukiwa umekaa hivyo Slipway inakuwa Kushoto kwako. Nyuma yako ni Bahari ya Hindi. Ukienda moja kwa moja na hiyo barabara ya vumbi unakutana na mkeka wa Chole Road.

    inof@allied.co.tz

    ReplyDelete
  24. Hapo wote mmechemsha hapo ni sumbuwanga mkoani rukwa karibu na kanisa la ruthelani church.

    Mzee kwa kweli unatembea hadi sumbawanga?

    ReplyDelete
  25. hapo ni Mchambawima

    ReplyDelete
  26. Hapa ni kigamboni kuna project moja inaendelea kule

    ReplyDelete
  27. Hapo Ankal ni barabara ya kuelekea Msasani slipway ambayo inaenda kushoto kwa hii picha na hiyo ya vumbi inatokea kuungana na barabara ya Chole.

    Fulanaaaaaaaaaaaaaazzzz

    areacode741@hotmail.com

    ReplyDelete
  28. jamani hapo ni Keko Juu kona ya mafleti.

    ReplyDelete
  29. barabara ya vumbi inatoka chole road kwenda slipway

    ReplyDelete
  30. Hapo ni maeneo ya Mgeni Nani Mbagala Kibonde Maji kuelekea kwa MchambaWima.

    ReplyDelete
  31. Hiyo barabara ya vumbi inatokea choleroad inakuja moja kwa moja ukikata kulia kwako ni slipway na kushoto unaelekea msasani na mbele ya hiyo barabara kuna double Tree hotel.Hope picha umepigia double tree hotel.Wait for fulanazi contact P.o.box 22657,Dar Phone 754 086683

    ReplyDelete
  32. *Mdau wa Masaki*March 23, 2010

    Jina kamili la hoteli ambapo picha hiyo ilipopigwa ni "DoubleTree by Hilton ". Na ipo jirani tu na Slipway jijini Dar. Ingawa bado kufunguliwa rasmi, lakini huduma zimeshaanza kutolewa.

    ReplyDelete
  33. Woote mmechemsha, hapo ni mbagala Kiburugwa, kibanda ni kwa mzee kinyogoli na njia ya kulia ni kwenda kwa mganga maarufu wa maruhani bibi machapati

    ReplyDelete
  34. YAANI WOTE MMEKOSEA KABISAAA, HAPO NI MLIMA KILIMANJARO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...