Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo (kulia) akipokea msaada jana mjini Dar es salaam wa magodoro 2000 na blanketi 2000 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Kilosa waliokubwa na mafuriko ambayo yaliwasababishai kupoteza mali zao zote. Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 75 umetolewa na Mwenyekiti wa Karimjee Jivanjee Family Bw. Hatim Karimjee (kushoto) kwa niaba ya wenzake.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mhn...wahindi bwana!

    ReplyDelete
  2. MUNGU awabariki wote wanaojitolea, msaada ni wa kutia moyo sana. Sio wengine kampuni inaingiza mabilioni ya fedha kwa mwaka halafu wanatoa hela ya siku moja.

    Ni hayo tu wadau.

    ReplyDelete
  3. Bro michu,
    Napenda kuchukua fursa hii kuwarekebisha wale wote ambao wanadhani wahindi wote ni wabaguzi. Ni lazima tuelewe wenzangu kwamba we cannot paint all Indians with the same brush.Tunajua kwamba wapo wahindi ambao wanaishi vizuri nasi na wanasaidia sana katika jamii.Ninaelewa kwamba watu wengi wamekasirika kutokana na vituko vilivyotokea huko India kuhusu ubaguzi unaofanywa na wahindi.But again,lazima tuelewe kwamba kwanza kabisa,kuna tofauti kati ya wahindi wa India na wenzetu wa Tanzania.Pili, there is blackship in every community.Kwa hiyo wenzangu lazima tufikiri mara mbili kabla ya kuongea chochote.

    Mdau wa antartica.

    ReplyDelete
  4. safi sana ndugu zetu watanzania wenye asili ya asia kwa kweli wanaongoza katika kulipiga tafu taifa lao

    wana jamii mnapoongelea swala la ndugu zetu kule india ni kweli wanapata mateso lakini msijenge chuki kwa hawa waliopo nchini

    hawa ni wananchi na wana umoja katika mambo ya taifa bega kwa bega na hawana roho mbovu kama za wale walioko huko india.

    ReplyDelete
  5. WATANZANIA TUONYESHE UMOJA, NA UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO UNALETA UDHAIFU, WANAFUNZI WA VYUO HAPO TANZANIA VYUO VYOTE ANDAMANENI NENDENI UBALOZI WA INDIA MKATOWE LLALAMIKO NA KILIO CHENU JUU YA WANAVYOFANYIWA WATANZANIA WANAFUNZI INDIA, HILO NI JUKUMULENU WALE NI WENZENU PIA, SERIKALI YA INDIA INATAKIWA KUKUMBUSHWA JUU YA UTU NA DEMOCRACY, KWENDA KUSOMA KWAO SI KOSA. IS NOT A CRIMINAL ACT KWENDA KUSOMA INDIA. BALOZI WA INDIA TANZANIA LAZIMA ATOWE TAMKO JUU YA HALI ILVYO HUKO INDIA YA WATANZANIA WANAOSOMA HUKO.

    ReplyDelete
  6. Ni matarajio yangu kuwa wapiga kura wa Kilosa watampigia kura tena mbunge wao Mkulo. Amefanya kazi nzuri ya kutawatafutia misaada.

    ReplyDelete
  7. yaliyomo yamo.March 18, 2010

    hawa jamaa wa karimjee jivanjee nawapa big up sana. siyo kwa magodoro na mablanketi, bali kwa namna wanavyojua kusimamia biashara!

    big-up men!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...