Mkurugenzi wa Mtendaji wa Global Publishers Erick Shigongo(kushoto) akiwa ameshikilia moja ya zawadi aliyempatia Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru mara baada ya kutembelea ofisi zao na kuwahabarisha kuhusu “habari ndiyo hii”ambapo mtandao wao ulivyoshusha gharama ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, wachapaji wa magazeti mashuhuru ya Ijumaa, Uwazi, Risasi, Amani na mengineyo, Bw. Eric Shigongo (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Bw. Ephrahim Mafuru mchana. Leo ilikuwa zamu ya kampuni ya habari ya Global Publishers kutembelewa na kampuni ya simu ya VODACOM Tanzania ili kunadi HABARI NDIYO HII, ikiwa ni kampeni mpya kabisa iliyoanzishwa kupitia vyumba vya wanahabari jijini Dar es salaam. Katika kampeni hiyo, watumiaji wa mtandao huo sasa wataweza kuongea kwa shilingi moja tu kwa sekunde kwa watumiaji wa Vodacom kwenda Vodacom. Eric Shigongo akisalimiana na Necta Pendaeli Foya, huku Mkurugenzi wa Mahusiano na Mkurugenzi wa Masoko Ephraim Mafuru wakijiandaa kuketi.

Eric Shigongo akimuelekeza Ephrahim Mafuru sehemu ya kumwaga wino kwenye kitabu cha wageni, huku Mwamvita Makamba akingoja zamu yake
Mkurugenzi wa Masoko akiongea na wafanyakazi wa
Global Publishers kuhusu HABARI NDIYO HII
Eric Shigingo akiongea wakati wa hafla hiyo
Meneja mkuu wa Global Publishers akikaribisha wageni
Chumba cha habari cha Global Publishers wakati wa hafla hiyo leo











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Ok But Podium mngeifunika walao kwa taulo....! Ni maoni tu.

    ReplyDelete
  2. podium imechoka hiyo!!

    ReplyDelete
  3. nina mawili....moja podium na pili huyu mwamvita vipi mpango wake? au ndio wachafuzi wa bongo kama kawaida?

    ReplyDelete
  4. Kaka huyu Mwamvita hivi vivazi vyake vinatega! Khaa!

    ReplyDelete
  5. SHIGONGO NDUGU HUBADILIKI??..tafuta PAMBA zenye hadhi ya u-MD..hzo nguo za kariakoo-makoba sio mwana...tai RANGI INAWAKA utadhani balbu...NENDA WOOLWORTH Ukanunue nguo za maana BRAZA...!!

    ReplyDelete
  6. yani nakupenda wee eric basi tu,just to embarce you...
    ubarikiwe na Bwana!!

    voda mlishindwa kbs kuwa na press conference???

    ReplyDelete
  7. Hii style ya kutembelea vyombo vya habari waliokuja nayo voda ni nzuri kwa jamii. Kwani hapa tunapata kuona undani wa hivi vyombo ni chombo kipi kina mazingira mazuri ya kazi.
    Press conf za pale maelezo au kwengineko huwa zinatuficha ukweli khs hivi vyombo vyenyewe! Hapa mbabaishaji ataonekana.

    naungana na walionitangulia, Podium ya Global publishers imechoka kusema ukweli.

    Nasihi hata viongozi wa wizara ya habari wajenge utaratibu walau kila baada ya miezi miwili kuvitembelea hivi vyombo na kuongea na wafanyakazi na watendaji wengine. Hii inaweza kusaidia kuleta maboresho ktk upande wa pili wa shilingi.

    Mdau Mmoja hivi

    ReplyDelete
  8. We Shigongo,

    Sio ndo unatoka hapo,,unaanza kuandika hadithi,,kwa kuwaangalia hao mademu..hachelewi huyo kutunga hadithi zake,,the guy is professional...

    ila kumbe handsome

    Lucy

    ReplyDelete
  9. Hongereni voda kwa kufikilia kidogo. Hata hivyo bado sana mngekuwa na akili za kutosha mngeweka shs 1 kwenda mitandao yote hapo mngekuwa mmetuokoa na adhabu ya kutembea na simu nne kisa bei kubwa kati ya mitandao tofauti. Kwa kifupi habari yenu haishtuwi coz tigo wamekuwa na habari hiyo ya sh 1 kwa miaka kadhaa sasa. By Mwanyika

    ReplyDelete
  10. Kuna mambo mawili..voda wameenda kwenye magazeti ya udaku basi tu,,..kwa ajili yanasomwa na market segment ..kati ya wanazokusudia..lakini angalia hata walivyovalia utaona wamekurupuka tofauti walivyotembelea vyombo vya ukweli kama daily news,tbc,itv etc..utaona hata sehemu waliyokaa ilipambwa na bango lao la voda...hapa silioni zaidi ya bango la uwazi na podium iliyonunuliwa kwenye mnada majembe..dizaini ilikuwa ya moja ya hoteli zilizovunjwa kati kati ya mji..like mawenzi hotel etc....

    La pili its like shigongo alienda kulalamika hawajamtembelea ..na akawadaka barabarani....hawajajiandaa wala yeye hajajiandaa....zaidi ya kuandika haraka haraka placard ..."karibu vodacom"....

    kukosekana kwa alama yeyote ya voda ni ishara kuwa voda hawataki kuhusishwa na low class papers za udaku...na walikuwa pale kuwazuga tu...-ANALYST[MCHAMBUZI WA MAMBO]

    ReplyDelete
  11. Watu wengine bwana comments zao utadhani anatokea kwenye mataptap.

    "magazeti ya udaku" au "low class papers za udaku"

    Unajua reach ya haya magazeti? Sasa ulitaka magazeti yote yafanane. Kila mtu ana kundi alilolenga, usiwaponde wenzake.

    ReplyDelete
  12. We shogongo jifunze kusalimia watu kwa heshima kwenye picha ya pili unamsalimia huyo dada huku mkono wako nwa kushoto ukiwa karibu na maeneo ya maangamizi maana yake nini? halafu nyumbani huna kioo wewe? unachanganyaje rangi za mavazi kama vile maputo ya kwenye harusi? mwachie mkeo akuchagulie mavazi MENU yako ya uvaaji ni kama mtu kala kande na pilau-heavy food-tegemea mashuzi tu..na hiyo podium yenu ni inaonyesha jinsi ofisi yeni isivyokuwa makini USAFI UNAFICHA UMASKINI BWANA KAITUPENI KULE YOMBO KILAKALA HARAKA-ORDER,
    MZAZI CHOPANGA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...