KWA HESHIMA NA TAADHIMA GLOBU YA JAMII INA FURAHA YA KUTANGAZA KWAMBA IMETIMIZA MDAU WA MILIONI 8 MUDA MFUPI ULIOPITA NA KAMA ILIVYOAHIDI KUANZIA SASA HADI MDAU WA 8,000,100 ATAPATA ZAWADI YA ZE FULANAZZZ BURE. UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUTUMA ANUANI YAKO KUPITIA:
ILI ULETEWE ZE FULANAZZZ POPOTE ULIPO ULIMWENGUNI. HAKIKISHA UNATUMA ANUANI YAKO KAMILI NDANI YA MUDA HUO.

TIMU NZIMA YA GLOBU YA JAMII INATOA SHUKRANI ZA UNYENYEKEVU KWA WADAU WOTE KWA KULIENDELEZA LIBENEKE HADI KUFIKIA HAPA. BILA WEWE MDAU HII ISINGEWEZEKANA HIVYO HATA KAMA UTAKOSA ZE FULANAZZZZ KWA KUWA NJE YA WADAU 100 WA KWANZA BAADA YA KUGOTA WA MILIONI 8, JISIKIE KWAMBA HIZI SHUKRANI ZINAKUHUSU WEWE PIA!

ANGALIZO: NI WALE WADAU WATAKAOKUWA NDANI YA MDAU WA MILIONI 8 NDIO WATAONUFAIKA NA HILI. IKISHAPITA 8,000, 100 UJUE BAHATI SI YAKO. ANGALIA KWA MAKINI TARAKIMU ZA MAHESABU CHINI KULIA KWENYE GLOBU HII YA JAMII. ZAWADI ZITATUMWA WIKI MOJA KUANZIA LEO, NA SI VIBAYA UKIUJULISHA UMMA KWAMBA UMEPATA ZAWADI YAKO KWA KUTULETEA TASWIRA UKIWA UMAVAA AMA HATA KWA KUIONESHA TU BILA SURA YAKO KUONEKANA. YOTE SAWA...

ASANTE SANA MDAU KWA KUWA NASI, MOLA AKUJAALIE

-MICHUZI


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nshachelewa naona. Tayari imeshagonga 8,001,057. Hongera!!! Libeneke 1 daima!

    ReplyDelete
  2. mhh anko mbona kiini ,ni wa 8001400 iabidi nipate upendelea maalum

    idumu libeneke

    ReplyDelete
  3. nimekosa T-shirt jamaniiii.. anyways next time nitajitahidi nipate ze fulanaz, anko fanya na vitambaa hata vya ichwani basi.

    Tuko Pamoja, Mama A

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...