pikipiki 100 ambazo zimeletwa na meya wa jiji la Changzhou huko China walizoletwa kama zawadi kwa halmashauri ya jiji la dar zitazotumika kwa halmashauri za ilala, temeke na kinondoni na pia chache zitapelekwa kituo cha polisi cha Urafiki kusaidia kazi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Wawapatie askari wa jiji ili wamalizwe vizuri na daladala maana wamezidi kuonea walalahoi

    ReplyDelete
  2. ASKARI WA JIJI KWA KUTUMIA VEMA HIZI PIKIPIKI WANAWEZA KUSAIDIANA NA ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KATIKA KUSIMAMIA UEGESHAJI MBOVU WA DALADALA VITUONI NA KUSABABISHA FOLENI HASA KWENYE KITUO CHA POSTA MPYA NA MNAZIMMOJA NA KUZUIA UHALIFU MWINGINE KUTIA NDANI KUONDOA USUMBUFU WA WAPIGA DEBE.ASKARI HAO WANA MCHANGO MKUBWA KATIKA SUALA LA USALAMA WA RAIA JIJINI WAKITUMIWA VEMA.

    ReplyDelete
  3. Wodi ya Toyo Muhimbili lazima iongeze majeruhi wa kikata miguu na mikono.

    ReplyDelete
  4. duh,
    mzigo wa kichina.

    ReplyDelete
  5. tena hao askari wa jiji wanaacha kupambana na vibaka na mateja wanaozurura wanawaandama dada zetu wanaotuletea vyakula vya bei rahisi.
    wananikera kishenzi.

    ReplyDelete
  6. Feki tu hizo......

    ReplyDelete
  7. Mtakoma kwa spea maana nahisi kila week itakuwa ni spea fulani ambayo lazima itoke kule kule China, jamaa wanaona mbali kweli kweli nyinyi mnapongeza!!!

    ReplyDelete
  8. haya sasa wameziponda pikipiki za kichina ( ohh feki zinasababisha ajali , ohh sio imara ) sasa mmepewa bure naona mtabadilisha usemi wenu na mtasema ( ohh ORIGINAL na zinasaidia usafiri ) binadamu bwana mpaka umpe ndio akuthamini , feki nyie mnatengeneza ? hata mashine ya kunyolea hamuwezi kutengeneza then mnasema za wenzenu feki. mdau A.K.A MKEREKETWA WA DSM

    ReplyDelete
  9. Jamani Wachina zisije zikawa pikipiki feki, baada ya mwezi mmoja zinakufa zote

    ReplyDelete
  10. Ankal, nina swali la kizushi!
    Hizo ni orijino ama nakala (feki)?
    Ni kutaka kujua tu!

    ReplyDelete
  11. hapo wazee mnaona mmeletewa bonge la zawadi hayo mapikipiki ya kichina yakianguka yanavunjika vipandevipande kama glass.

    ReplyDelete
  12. Pikipiki za kichina. Mmh, zawadi haikataliwi lakini...

    ReplyDelete
  13. Tutaziona hizi kama vibajaji Vibajaji vililetwa kwajili ya Vilema watolewe kwenye kuombaomba ili wapate kazi ya kujipatia na ndio Serikali ilivyoomba msaada. navipa mwaka vitaanza kuuzwa. USIBANIE HIIIIIIIII. JE Wadau mnaonaje? Juma

    ReplyDelete
  14. Pikipiki feki

    ReplyDelete
  15. aKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE.

    ReplyDelete
  16. florian rweyemamuMarch 24, 2010

    ZA KICHINA. tusubiri zife na tununue spare kwa hao hao wachina kutumia pesa yetu ya kimatumbi. KAZI KWELI KWELI.

    ReplyDelete
  17. Du jamaa wanaakili kweli kweli maana wanawekeza stock yao ya chuma chakavu. pata picha ndani ya miaka 2 tu hizo pikipiki zitakuwa katika hali gani na watakuwepo walemavu na yatima wangapi. Big up wachinaaaa

    ReplyDelete
  18. Mtoto wa CoastMarch 25, 2010

    Si kila kitu cha kichina ni kibövu.
    Tuwe macho na propoganda zinazopikwa na nchi zenye wivu wa kutaka wao tu ndio waonekane kuwa ni mabingwa wa kila kitu.

    Hata kama wengine hawasemi, Mimi huku nikiitafuta mbingu na mikono yangu kifuani, kwa unyenyekevu mkubwa natamka;

    " Rafiki zetu Wachina, asanteni sana kwa msaada huu. Wengine hata mkokoteni wa mbao tu hatuwezi kuumiliki hapa. Mola awazidishie mara dufu bidii ya kazi na uzalishaji wa bidhaa bora na mzidi kuwa na mahusiano mema na nchi nyingine kote duniani. Mnajishusha mtakweza! Wanaojikwezao watashushwa maana Mola wetu ndiye Mpaji mkuu.

    Ee Mola nasi Watanzania, tupe moyo wa kupenda kazi na kujituma na kuthamini michango ya wajuvi mbalimbali tulionao na utupe ushirikiano wa kuendelea kulinda amani yetu.
    Tupe mioyo na akili za kukumbuka kutumia vyombo hivi kwa usalama na kwa ajili ya faida ya Umma wa Watanzania.

    Amelaaniwa yeye atakaye taka kufanya mradi wa ubinafsi na au kujitafutia umaarufu kupitia msaada huu wa rafiki zetu Wachina.

    Amen

    ReplyDelete
  19. Michuzi usisahau kutuwekea picha zitakapoanza kula mizinga ee. Karibu Reading ndugu yangu usiishie tu London.Safari njema.

    ReplyDelete
  20. tunashukuru sana wachina lakini wasiwasi wangu zisije zikawa kama hivyo viatu vyenu vya yebo unanunua leo kesho kimechanika au vifaa vyenu vya electronic unanunua dukani ukifika nyumbani unaweka kwenye soketi kinaungua hapo hapo

    ReplyDelete
  21. Piki piki zenyewe zimepimwa Ubora, isije ikawa kama simu zao line 3 sijui, charging system migogoro!!!!!Zipimwe ubora ndio wapewe watumiaji

    ReplyDelete
  22. wachina tena?pikipiki ziko salama kweli hizi

    aya twawatakia kazi njema

    ReplyDelete
  23. VIMEO VYA KICHINA SALAAALEEEE!!!

    ReplyDelete
  24. Zawaadiii?Hakuna kitu kama hicho siku hizi, yapaswa kujiuliza hizo pikipiki ni exchange ya nini, whether ni leo au miaka kumi ijayo.Kuna kitu inaitwa mutual benefit viongozi wetu hawana uelewa huo,mfano mimi nipo China kwa scholarship za serikali ya China but kwa jinsi nlivo-experience kuna plan ipo in exchange ya hizi scholarship.Wabongo tuamkeni jamani, mtu hawezi akakusalimia ghafla barabari hakujui,si salamu ya bure au zawadi..lazima anataka kukuibia au kukuchulia mkeo!!

    Zhang, China

    ReplyDelete
  25. Tena wachina kiboko, siku hizi pikipiki yao ikikudondosha inasema SORRY, ukiinyanyua tu ukawasha unasikia welcome.....wachina oyeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  26. Wazee wa manisapaa. Labda mungeleta mikokoteni ya kichina ya kubebea taka maana hii serikali ya mtaa inashindwa kazi ya kusomba takataka. Kwa mfano hapa Namanga, kiwanja chetu cha michezo na midahalo wamezilundika, eti dampo. Pia wameanza dampoo jingine mbele ya TIRDO na mengine saba yapo barabara/ mtaa wa 'Maandazi Rodi' Bosi wetu mpya wa kata, hukusanya sadaka ya 2000/ kwa kila mtu aneingia ofisini, na 5000 au 10,000 nyumba zenye geti. Mageti yana mkera!!!

    Tuokoeni jamani na hizi takataka kwa visombea na sio vya-upepo vya kichina.

    ReplyDelete
  27. SASA TUWAOMBE MAGARI NA VIFAA VYA KUZOLEA TAKA KWA KUWA HIZO NDIZO CHANGAMOTO ZETU HAPA JIJINI.

    ReplyDelete
  28. ankal usisahau kufika huku manzese(reading)karibu sana.

    ReplyDelete
  29. duh..misaada mingine tuwe tunakataa tu coz inaongeza matatizo tu.hizi pikipiki zakichina sijui kwanini tbs inakubali ziingizwe nchini..vyuma vinachomelewa kila siku hazina standard yoyote.kwanini tanzania tumekua centre ya vitu feki vyakichina.

    ReplyDelete
  30. Wabongo kwa ubaguaji wa kitoto bwana! Sio kila kitu cha china low quality!

    Hizo iPhone mnazozibabaikia zote zinatengenezwa China.

    Compyuta karibia zote mac/Dell/HP China.

    Tukirudi kwenye maada, "There is no free lunch" kuna strings attached na hizi zawadi!!

    ReplyDelete
  31. eti zinavunjika kama glass,annon wewe?

    mbavu zangu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...