wa zahanati ya Kitunda,wilayani Sikonge
JK akipampu maji kutoka katika kisima kilichonjengwa nawananchi chini mradi unaoratibiwa na shirika la maendelo la umoja wa Mataifa UNDP, katika Kijiji cha Mbola, Wilaynai Uyui, mkoa wa Tabora jana. Anayeangalia ni Mama Salma Kikwete na Mwakilishi MkazI wa UNDP Bwana Aberic Kacou
JK akikagua shamba la mahindi lililolimwa kwa ubora na mkulima Bwana Abdallah Sebitango Balakekenwa katika kijiji cha Mbola kata ya Ilolangulu, Wilayani Uyui, mkoa wa Tabora.Mkulima huyo mwenye kumiliki shamba la ekari 25 ana wake wawili na JK aliahidi kumnunulia ng’ombe wa kulimia ambapo ahadi hiyo ilitimizwa hapo hapo.
Mwanafunzi wa Mwaka wa pili katika chuo cha ufundi VETA Tabora Bwana Mandago Pascal Mandago anayesomea fani ya umeme wa majumbani akielezea zoezi lake muda mfupi baada ya JK kuzindua Rasmi Chuo hicho jana mjini Tabora.Pembeni ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA Prof.Zebadia Moshi.
JK akisalimiana na baadhi ya wafanayakazi wa chuo cha ufundi Tabora muda mfupi baada ya kuzindua chuo hicho kilichofanyiwa ukarabati mkubwa jana mchana
Bibi aliyejitambulisha kwa jina la Zubeti Kungi akisalimiana na Mama Salma Kikwete pamoja na JK muda mfupi kabla ya Rais kuhutubia mkutano wa hadhara, katika eneo la Kitunda, Wilayani Sikonge.Bi Kungi alisema kuwa amezaliwa mwaka 1936 na kuwa alifurahi sana kumuona na kusalimiana na Rais Kikwete pamoja na mkewe.
JK akisalimiana na mfugaji Bw. Shadima Nuru Misso wa kijiji cha Ipole, Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora.Mfugaji anayehamahama na mifugo yake ipatayo ng’ombe zaidi ya 200 alimlalamikia Rais kukosa eneo rasmi la malisho yake.Kwa upande wake Rais Kikwete ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Sikonge kumtafutia mfugaji huyo eneo la kufuga na kuahidi kuleta wataalamu ili kumuwezesha mfugaji huyo kupanda majani yanayofaa kwa mifugo yake hiyo na hivyo kuwa mfano bora kwa wenzake.
Home
Unlabelled
JK ziarani Tabora
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


huwa nawaza Mhe.Raisi anajisikiaje anapokutana na raia wake maskini lakini bado wanafuraha kumuona na kuongea nae,hivi kweli anatapa usingizi? huku mafisadi wanakula hazina na nchi na ndio wakwanza kumpiga vita. Natamani ningependa nafasi ya kumuuliza hilo swali....
ReplyDeletepicha ya tatu, kulikuwa na haja gani ya kutwambia mkulima abdallah ana wake wawili?
ReplyDeletesasa chuo ndio kinafunguliwa rasmi lakin tayari kina wanafunzi wa mwaka wa pili, hii imekaaje?
ReplyDeleteMbona waziri mkuu nae alikuwa huko huko tabora hata wiki 2 hazijapita? What is so special that requires attention of the two(Prez,PM)? How about its finacial implications?
ReplyDeleteNapenda kuuliza kama uwanja gani wa ndege ulitumika kurushia ndege ya rais maana uwanja wa Tabora unahitaji ukarabati wa hali ya juu. Unatia aibu. Mvua ikinyesha sana ndege haitui kabisa. Kwakweli uwezo upo wa kuukarabati uwanja. Ndiyo hayo sina la zaidi.
ReplyDelete