washiriki wa kipindi kipya cha muziki kinachotarajiwa kuanza kurushwa na TBC-1 Jumapili hii wakirekodi mchuano wao ambapo nyota wa fani mbalimbali huchuana kwa kucheza na mapatna katika wiki 13 za kipindi hicho watazamaji watakuwa wanawachuja mmoja mmoja hadi mshindi apatikane akiwa yule aliyesalia mwisho. atalamba zawadi ya shilingi milioni 15
Home
Unlabelled
Kipindi cha SELEBUKA kikiandaliwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
utumbo mtupu yani sijawahi kuona wote hawajui kucheza wataishia kutongozana tu lakini ni upuuzi hawajui kucheza wanataka kuiga mambo ya dancing with the stars haya yetu macho kaka michuzi usisahau kutuwekea mambo yanavyoendelea tena kwa video sie wambali tupate kujionea
ReplyDeleteInakuwaje muziki unaotumika ni wa kilatino???? Kwani hatuna muziki wa nyumbani?? Watanzania vichwa maji kweli kweli. Kwa sie tulioa wageni utamwonyeshaje mkeo "dancing with the stars" ya kwetu afu kinapigwa kilatino!!!
ReplyDeleteMdau USA
Kilichobaki sasa, ni mcheze mziki tu sasa.hamna deal la kufanya.
ReplyDeleteOyaa uncle.Najua utanibania kama kawaida yako.Mi sioni mshindi hapo.Hasa huyo jamaa mwenye shati jekundu.Vurugu kwenda mbele.
ReplyDeleteHaya tena Photocopy nyingine hiyoo!! Hivi jamani hata kama tuna copy na ku paste kila kitu cha unyamwezini tuwe tunajaribu kuingiza maadili yetu ili hata Babu na Bibi kule Lukuredi wawe wananufaika!! Kama swala ni mashindano ya kucheza la hao we " celebrities"" kwa nini wasishindanishwe kucheza Lizombe au Kasimbo yeye?? Mimi nadhani kwa kufanya hivyo ingekuwa inaleta maana zaidi kwa jamii yetu ya kitanzania kuliko kucheza Macharanga ambayo hayatuhusu!! Jamani kama ubunifu hatuna kabisa tujaribu KU-COPY, TU_PASTE halafu TU-EDIT kidogo walau tuonekana tunafanya kazi!! Mwe!
ReplyDeleteUTAMADUNI WETU UMETUSHINDA? SIJAONA KUCHEZA NGOMA ZA KWETU ZA MBEYA AU ZA KIZARAMO MDUNDIKO AU ZAKIMAKONDE AU KIDUMBAK CHA PEMBA AU NGOMA ZA BUKOBA TUNARUKIA MA SALSA NA RUMBA? SELEBUKA GANI HII BWANA. TUMEINAMA TUMEINUKA TUMEOKOTA KIDUDE EEEH KIDUDE MAMBO MAMBO KWA SOX EEEH KWA SOX HAKIPENDWI KITU NI POCHI TU.
ReplyDeleteMRISHO MPOTO KASEMA TUNAUTUKUZA UENGEREZA SANA NA MAMBO YA NJE>
KIMARO.
JAMANI VIPI MNANDA,MCHIRIKU,VANGA,MDUNDIKO NA MAGOMA KIBAO YA KIKWETU WASWAHILI;
ReplyDeleteHAO WANANITIA KINYAA TU,
bora kuweka ngoma za asili tu kuliko kuiga kitu tusicho kiweza,
Bwaa....nahisi kutapika.Kibaya zaidi ni kuwa hakuna hata anayejua kucheza aina hiyo ya muziki kati ya hao wote.Naona wanajizungusha tuu.Kwa huku ughaibuni mmoja anakuwa ni mtaalamu wa kucheza na mwingine anakuwa ni mtu maarufu ambapo huyo maarufu anakuwa anafundishwa na huyo mtaalamu.Hapo nimeshindwa kutofautisha...Mvurugano tuu.Bora wangechukuliwa wataalamu wa ngoma za asili kutoka vikundi kibao ambavyo tunavyo hapo Tz.Kama kile cha mzee jangala,Parapanda arts,
ReplyDeleten.k.
Jonaa.
Michuzi nimeona, kwa leo sitacomment chochote, naomba uturushie kadri mashindano yatakavyokuwa yanaendelea.
ReplyDeleteTuombeane uzima.
mimi nampa ushindi mwenye suti nyeusi naona atakuwa Ali Baucha .he is the best
ReplyDeleteWANAZUONI WA BASATA NA BAGAMOYO TUONYESHENI KILICHOPO CHINI YA KAPETI LA MASHINDANO HAYA NA HIYO MANTIKI YA MSHINDI KUONDOKA NA TSHS.15,0000,000.00 BILA KULIPA MAPATO YA SERIKALI.TRA ELEKEZENI MACHONI HUKU KWENYE MAPESA NA MSIONE HAYA KUNYOFOA HALALI YENU.
ReplyDeletemiziki yetu tunaiua wenyewe..jamani tumieni miziki ya kitanzania please! tumechoka utumwa.. tumesoma ili iweje ndugu zangu?
ReplyDeletekamera yenyewe moja na imewekwa sehemu moja utajuaje kama mtu wa upande wa pili anacheza vizuri???