Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, niliwahi kusikia kwamba Pofu ana miiko yake kama ukitaka kumuwinda. nadhani kama tungepata wawindaji wangeweza kutuambia. Nilisikia kuwa ukitaka kumuwinda pofu siyo rahisi kihivyo, yaani si kama unavyoweza kuwinda digidigi au nyumbu na wengineo. Kuna ukweli???
Mdau DSM
Mdau DSM
YOU CAN READ EVERYTHING YOU ENQUIRED ON THIS LINK (http://www.safaribwana.com/ANIMALS/animpages/eland.htm)
ReplyDeleteKatika wanyama bora wa kuwindwa, pofu ni namba moja... Yaani hata ukirudi nyumbani na nyama ya pofu, lazima upate heshima nyumbani na mtaani kote..
Watu wengine hufikia stage ya kusema kwamba pofu ana mashetani.. maana matatizo mengi hutokea wakati unamwinda (Eg. Kupata ajali, nk).
Nyie ndo walewale mnaotaka kutumalizia asilimali zetu...sijui watu wengine wakoje badala ya kuuliza ni jinsi gani tutawalinda wanyama wetu unauliza tutawaangamizaje...kha!
ReplyDeleteFikiri kabla ya kutunda..sijui we ni muumini wa dini gani hufuati maandiko...khaa!!
Unataka kumwinda Pofu ili iweje? Wewe lazima utakuwa jangili au mtu ambaye hujali hali ya wanyama hawa. When they all go extinct, that's when you will be happy, uh?
ReplyDeleteWewe jangili usituletee shida.
ReplyDeleteHuyo mnyama anapatikana kwenye hifadhi za taifa au kwa kifupi hizo ni nyala za taifa. Sasa unataka kumuwinda wa nini?
Umemaliza faru sasa unatafuta mbinu za kuwapata pofu, shame on you.
Tatizo lako mto mada hukuweza wazi wewe ulisikia kuwa anawindwaje?. Maana kwa kusema huwindi kama digidigi je anawindwaje?. Kwa mshale, kwa upanga, kwa bunduki, kwa bomu, kwa mitego, kwa nyavu, kwa madawa ya usingizi au vipi?. Elezea kwanza kiufasaha ili mjadala uendelee. Kwa style hii jibu utakalopata ni baadhi ya niliyoyaorodhesa hapo juu.
ReplyDeletesasa wewe unomba ushauri wa kumuwinda pofu ili umfanye nini ao ili iwe nini? kama ni kitoweo kipo butcher ao sokoni. watu wengine bwana? mdau toka bujumbura
ReplyDeleteWhat a magnificent beast
ReplyDeleteIts almost regal in its posture
Nafikiri huyu ni Pofu dume kwa kingereza aitwa eland, yeye na jamaa yake CHOREA ua fringe eared oryx ni baadhi ya protected animals. Basi kabla hujaanza kufikiria kuwawinda afadhali ucheck hiyo lisensi yako.Poaching for bush meat may land you in jail, eating makande.Ikiwa watafuta mishikaki afadhali uwinde mbuzi.
Samahani
Wakatabahu
ukitaka kumpiga risasi ukishalenga inabidi UFUMBE MACHO..
ReplyDeleteSiyo ukweli. Mimi si muindaji ila ninaweza kukuambia kuwa mila ama imani za kiafrika mara nyingi ni za kijinga. Niliwahi kuua chui aliyeingilia mbuzi wa babu yangu kule kwetu kusini (I had mtutu). Baada ya mwaka kupita nikakutana na mtu aliyeniambia kuwa yeye aliua chui na ilibidi aoge dawa kwani ukiua chui, fisi, simba, na wanyama wengine wakali lazima ufanye hivyo kwani wana miiko yao. Nilishangaa sana na nikauliza ni miiko ipi? Jamaa akaniambia kuwa ukiua chui, simba, fisi na wengineo bila kuoga dawa lazima utapatwa na maradhi yasiyotibika ama kufa tu ghafla. Mimi nimeshakuja TZ miaka miwili iliyopita na marafiki zangu wazungu waindaji, tulienda selous kwani kule pofu ni wengi mno, mwenyeji wetu Mze Idrisa (yeye ni gemu pale selous) ndiye aliyekuwa anatuongoza maporini hakutuambia chochote kile kuhusu kuoga dawa wala nini na kama kuna dawa basi alifanya kwa ajili yake bila sisi kujuwa. Wale marafiki zangu walibahatika kuua pofu mmoja kwa ajili ya trophy na swala wawili. Tukampa Mze Idrisa na wenziwe swala mmoja na nyama ya pofu ikagawiwa kwa baadhi ya wana vijiji pale kijijini, hatukuoga dawa na isitoshe kule maji nadra hivyo tulikuja kuoga mara baada ya kufika gesti pale rufiji na hatukuoga dawa. Tuachane na mila za kijinga ama imani potufu jamani. Ila ninachoweza kusema ni kwamba kumwinda pofu kuna kazi kidogo kwani ni mnyama anayependa kujificha ndani ya msitu mnene, si rahisi kumuona tu hivi hivi. Kumwinda kwake ni asubuhi sana ama jioni wakati jua linazama, jua likijitokeza tu anaingia msituni.
ReplyDeleteJAMANI SIJUI SISI WATANZANIA TUTAELIMIKA LINI!!ETI POFU ANA MASHETANI!!MIE NIMEKAA SELOUS GAME RESEWRVE NA POFU ALIKUWA ANAWINDWA KAMA WANYAMA WENGINE,NA POFU NI MRAHISI SANA KUMUWINDA USIKU UKIMWASHIA MWANGA WA GARI AU TOCHI KALI MACHONI....HUWA WANASHINDWA KUKUMBIA...KWAHIYO SIO RAHISI KUMUWINDA POFU MCHANA.....SIO KWAMBA ANA MASHETANI...SAWA BWANA
ReplyDeleteYaani, wewe unaeona mila za watu ni za kijinga wewe ndiye MJINGA namba moja.
ReplyDelete1.Hujui unachokitaka, kitu ulichouliza, na baadae msururu wa pumba ulizoandika ku justify swali lako havina uhusiano, na huu ni ujinga.
2.Si kila mila ya hao wazungu ni nzuri saana kiasi kukufanya usahau na kudharau za kwenu Mtwara.Na huu pia ni ujinga mwingine!
3.Tumia vema hayo makamasi ndani ya kichwa chako unayoyaita AKILI.Kushindwa kufanya hivyo ni ujinga mwingine.
Kama huna vya kuandika , Please USIANDIKE!!
hao wanaosema oga dawa sijui pofu ana mashetwan yaelekea kwao wachawi tuu hakuna kitu kama hicho! hata hivyo nyama ya oofu si tamu full mawter water nyama ya swala bwana kula dikdik na kile kiti moto pori a.k.a ngiri ile ndo nyama tamu kuliko nyama zooooote huko porini na buchani dunia nzima nyama ya ngiri ni tamu nyama ya ngiri ni tammmmmmm
ReplyDeletekamanda tosi kamata mara moja hili jangili likawindwe lenyewe ukonga.
ReplyDeleteUNATAKA KUWINDA POFU?
ReplyDeletekAMATA PEMBE ZAKE ATALAINIKA
AU MSHIKE MKIA ATAKUAMKIA SHIKAMOO!!!!!!!
KUWINDA POFU NI RAHISI SANA, KWA KUWA ANA MAFUTA MENGI NI MWOGA UKIMSHTUA ANAKIMBAI KUPITA KIASI NA HAFIKI KILOMETA MOJA ANAANGUKA MWENYEWE! ANAWAFAA WAISLAMU KWANI NI RAHISI KUWAHI KUMCHINJA!
ReplyDeleteAnon wa Sat Mar 20, 05:36:00 PM
ReplyDeletePofu ni aiana ya swala nafikiri ni largest kwa kiingereza anaitwa Eland.
Unaweza kujifunza pia aina za wanyama kwa kutembelea http://www.victoriatz.com/animals.htm#Kudu
Michuzi najua matangazo ya biashara hapo juu yanakutoa, lakini jaribu yawe saizi ndogo kidogo. Kwa sasa ni makubwa sana, wengine tunasoma blogu yako kwenye simu!
ReplyDeleteHuyo jamaa aliyeweza kuua chui halafu anauliza namna ya kuua pofu either mwongo au mjinga au vyote