waliokaa ni majaji na nyuma yao ni ma-MC wa kipindi kipya cha "SELEBUKA' kinachotarajiwa kuanza kuruka Jumapili hii kuanzia saa 3unusu usiku kupitia TBC-1 ambapo nyota wa fani mbalimbali kama vile filamu, muziki, mpira wa kikapu na kadhalika, wakiwa na waalimu wao wa dansa watashindana kwa muda wa wiki 13 ambapo kila wiki nyota mmoja atatolewa na atakayebaki hadi mwisho anatarajiwa kulamba zawadi ya shilingi milioni 15. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni ya PowerHouse Productions, Mama Anne Iddrissu, washindani wataanza kuchujwa kwa kura za watazamaji baada ya maonesho mawili. Shughuli hii imeanza kufanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Club Billicanas jijini Dar.
majaji Masoud Masoud a.k.a DJ Neagre J, Monica na Zahir Ally Zorro wakiwa kazini

MC Adam Mchomvu na MC Tayana
Ankal Anwar (kati) na wataalamu wenzie wa 2Eyez Production wakijiandaa
Kikosi kizima cha 2Eyez Productions kikiwa tayari
kuanza kazi ya kurekodi shindano hilo la aina yake
MC Adam Mchomvu akipigwa sopsopu
Muongozaji mkuu Bw. Chuzi (kati) katika maandalizi
Muongozaji mkuu Bw. Chuzi akitoa maelekezo
Nyota na waalimu wao wa dansa wakipata maelekezo
Nyota wa bongo fleva toka kundi la Wanaume TMK,
Chege (shoto) akiwa na nyota wa basketball Kissoky, ambao pia wanashiriki










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. idea ni nzuri lakini naona kama vile hakuna tofauti kati yenu na bongo star search hebu tujaribu kuwa serious kwenye kubuni vitu,nawatakia mafanikio mema next time tuwe more creative there so many things to introduce just sit,learn from various source then we can come up with great uvumbuzi!!!!!!!!!!!!!!ahsante,wakucox(traveller chris)

    ReplyDelete
  2. what is this?i dont get it
    jinsi ya kumaliza pesa za EPA eeh?

    ReplyDelete
  3. THIS IS TYPICALLY DANCING WITH THE STARS VERSION OF BONGO.........ONLY THAT STARS DANCE ALONE THATS WHAT I HAVE UNDERSTOOD......I THINK IT WILL BE A GOOD SHOW TO WATCH.........

    ReplyDelete
  4. Kwa hiyo BBC STRICTLY COME DANCING inakuja bongo! sio mbaya ni idea nzuri.

    ReplyDelete
  5. Dancing with the stars ya Bongo....

    ReplyDelete
  6. Huyo jaji mwenye rasta ni MONICA ama JOAN?

    ReplyDelete
  7. Ni mawazo mazuri kutoka kwa wanazuoni wa dansi lakini je ni nini hitimisho dahahiri kwa utamaduni wa mtanzania ndani ya anga la kimataifa.Stesheni ya taifa imenufaika kimapato na mshindi anaondoka na kitoweo chake lakini taifa linaondoka na nini?Mimi ni mdau wa lugha ya kiswahili na utamaduni wa mtanzania kwa ujumla lakini nilichogundua ni jinsi watanzania wasivyokuwa tayari kuwekeza katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili na utamaduni wa mtanzania kwa ujumla.Lakini wanashau kuwa:-"JASIRI HAACHI ASILI NA MUACHA ASILI NI HASIDI".

    ReplyDelete
  8. Wabongo bwana! Yaani hatunaga ubunifu wa kwetu wenyewe kabisa. Yaani kuigana tu.

    Unakumbuka alianzaga mtu mmoja biashara ya Grosare, basi ikawa mtaa mzima grosare, akaja mtu wa Saluni za kiked, basi ikawa mtaa mzima saluni za kike, akaja mtu wa saluni za kiume za kuoshwa na wanawake, basi imekuwa mtaa mzima saluni hizo, Mweeh!

    Jamani tuwe wabunifu wa vitu vipya. Khaa!

    ReplyDelete
  9. mh kokoliko kacheza wee hakupata mapromota wa kukopi,taratibu kuna vipindi vingine msiige haviendani na maadili yetu.jaribuni kumiza vichwa mbuni vitu vyetu wenyewe jamani.

    ReplyDelete
  10. DANCING WITH THE STAR NDANI YA BONGO.

    ReplyDelete
  11. mdau nauliza lini tutaona television za bongo online hata kama kulipia tutalipia wadau wa huku nje tunamiss mengi..ankal tusaidie kuuliza

    ReplyDelete
  12. Nakubaliana 100% na Bw. Mlevi. Wale ndugu zetu wenye mtaji wa kuanzisha biashara kuweni wabunifu. Kwa hilo tu tuwaige Wakenya. Ukiwa na mipango mizuri utafanikiwa tz kwa sababu soko letu ni kubwa mno. Sio lazima wote tuwe na magrosari, masaluni, teksi, kuku na maduka ya spea feki ya magari. Ngowi.

    ReplyDelete
  13. hao judges wana experience yoyote ya dancing??au ndo yale yale ya kujuana? maana kama mnaamua kuiga Dancing with the stars ama strictly come dancing basi muige na jinsi ya kuweka judging panel.hao majaji watajaji vipi kama wenyewe hawajui jinsi steps za different dances zinavyotakiwa kuchezwa???? ankal tutafutie jibu tafadhali..

    ReplyDelete
  14. Kila la kheri Tuesday Kiangala, nakumbuka ulitufanza wakati tupo Kaole Sanaa Group kule Morogoro, sijafanya kazi na wewe muda mrefu sana so I hope is going to be a good project, na hatutegemei skendo, mara hujawalipa Majaji, Ma-Mc au Production crew maana naona unawatu wazuri tu ambao hata mimi nimewahi kufanya nao kazi, namuona Anwar mpiga picha mzuri saaana Bongo,Nuri na Dame, Mzee wangu Zahir Ally, Brother Masoud na Binti Matovolwa. But kikubwa ninacho kiona si mbaya ni katika kujitafutia fedha maana hali ya nchi ilipo sasa, siwezi kumlaumu mtu asifikirie tumbo lake kabla ya ki kitu kingine chochote, hasa mustakabali wa Taifa na watu wake. Mimi nikionacho sioni kama mliopo katika nafasi mnabuni mambo yatakayo wafanya vijana wawe motivated katika mambo ya maana. Maana ukiangalia mashindano mengi hayatoi nafasi kwa vijana kuona mambo yale ya maana na ya msingi kwa wao kama viongozi wa leo ama wa kesho kuwa ni ya kuyafanya, mfano vijana wengi unaona wanataka wawe Wanamuziki wa Bongo fleva, Waigizaji filamu, Ma-miss, Ma-Modo, Madansa na waonekane kama Rihanna ama JZ n.k. Mashindano mengi yanayotoa zawadi kubwa kama milioni 15, 20, Magari, Nyumba n.k utakuta ni ya kuimba,urembo,kucheza (Dance) na sasa hilo hapo but hukuti mashindano yanayo shirikisha vijana katika taaluma ama kuwajengea uwezo wa kufikiri, ubunifu katika Teknologia n.k matokeo yake vijana wengi sasa wanaona ni dili kuwa katika mambo fulani na si fulani thats why leo hii Tanzania hata tukiambiwa mgao wa umeme no body reacts! Nakupa mfano na wewe mwenzangu unayesoma maoni yangu na yeyote atakaye taka kubisha nikisemacho jiulize Unamfahamu Mwanafunzi bora wa kidato cha Nne kwa mwaka huu? then jiulize tena unamfahamu mshindi wa Bongo Star Search wa Mwaka jana ama Miss Tanzania? utakapo pata jibu najua unanielewa nasema nini! inasikitisha kuingalia Tanzania yetu! Kila lakheri!

    ReplyDelete
  15. Mdau hapo juu kanena vema.Kwa kweli tubuni kitu cha kuiendeleza jamii yetu katika kukuza taaluma na ubunifu kuliko haya mambo ya anasa kila siku.Kila siku watu wanamaliza vyuo vikuu na tafiti kibao zisizo na tija kwa jamii.Poleeee Tanzania;Poleeeni watanzania.

    ReplyDelete
  16. Mr. Michuzi,
    Sikujua kwamba kuna baadhi ya comments hu-publish. Anyway, I wanted to register my disagrement kwa TVT kukumbwa na ugonjwa wa biashara na Dili. Hizi biashara zinawafaidisha wachache, lakini mamilioni ya watanzania wanaachwa na impression isiyo sahihi.
    TVT iachwe kuelimisha watanzania na siyo kuwalisha kasumba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...