Baadhi ya mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwa katika semina yao katika Hoteli ya Giraffe, Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Jackson Kalikumtima wakala wa Miss Ilala, Ben Kisaka wakala wa Miss Temeke na Asmah Makau mwandaaji wa Miss Tanga Baadhi ya mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwa katika semina yao katika Hoteli ya Giraffe jijini Dar leo. Kutoka kushoto ni Awetu Salim, wakala wa Wilaya ya Bagamoyo, Nasib Mahinya wakala Mkoa wa Pwani na Sylivia Mwakilufi wa Miss Njombe. Meneja Huduma na Bidhaa wa Vodacom, Elihuruma Ngowi (kushoto) akishikana mikono na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari na Utamaduni, Herman Mwansoko katika hafla ya uzinduzi wa semina ya mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali nchini katika Hoteli ya Giraffe jijini Dar leo. Wengine kutoka kushoto ni Mshauri wa Miss Tanzania Dk Ramesh Shah na Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa semina ya mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali nchini katika Hoteli ya Giraffe jijini Dar leo. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Huduma na Bidhaa wa Vodacom, Elihuruma Ngowi na Mshauri wa Miss Tanzania Dk Ramesh Shah.
Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari na Utamaduni, Herman Mwansoko (kulia kwake) katika picha ya pamoja na mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali nchini mara baada ya hafla ya ufunguzi wa semina ya mawakala hao katika Hoteli ya Giraffe, Dar.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. kaka michuzi mimi kwa kweli nayachukia sana haya makampuni ya kibiashara. yani matatizo yote yaliyopo hapa nchini kipaumbele cha makampuni haya ni kwenye mambo ya starehe na urembo!! utasikia kampuni linafadhili uzinduzi wa albamu ya muziki na kutoa mamilioni kufadhili urembo!!! haya sasa hapa tunaona kila wilaya tanzania ina wakala wa vodacom miss tanzania!! kwanini wasianzishe mawakala wa vodacom wa mambo ya watoto yatima kila wilaya?? kwanini wasiweke mawakala wa vodacom wa kushughulikia tatizo la kinamama kupeteza maisha wakati wa kujifungua kila wilaya, kwanini wasiweke mawakala wa vodacom malaria na hiv fight kila wilaya?? kwanini wasijikite zaidi katika corprate social responsibilities zaidi. ningekuwa rais wa nchi ningepiga marufuku takataka zote hizo na kampuni ambalo halitaki funga biashara anza kwenu

    ReplyDelete
  2. Haya ndugu yangu Mahinya mwili unaanza kukutangulia huo. Basketball imeshindikana nini, au yale yalikuwa na Zimanimoto tu.

    ReplyDelete
  3. yaani hawa watu michuzi sura zao zinawasuta..kama huyo mwakilishi wa bagamoyo...anawaza fweza tu huyo,na namna gani ataweza kuwaducha! vyamtindo dhaifu..haya mashindano yamekosa maana kwa sasa!
    MZAZI

    ReplyDelete
  4. kalikumtima aliacha kujishulisha na Basketball akaenda kwa warembo, alikuwa mtu committed na serious sana katika maendeleo ya basketball. Wish he could come back akaachana na warembo. we need strong and serious personality in basketball like this guy.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...