Kampuni ya African Barrick Gold, (ABG), leo imetangaza kuanza tena shughuli za uchimbaji katika mgodi wake wa Bulyanhulu baada ya kutokea kwa ajali ya kuanguka kwa mwamba Machi 16 na kuua wafanyakazi watatu.
Eneo ambako mwamba ulianguka litaendelea kufungwa kufuatia uchunguzi kutambua chanzo cha ajali hiyo.
Timu ya wachunguzi waandamizi kutoka Barrick Gold Corporation (Barrick) wamewasili mgodini kufanya uchunguzi kamili na wa kina wa ajali. Kampuni ya ABG imedhamiria katika kuhakikisha usalama wa kila mfanyakazi wake na itaendelea kutoa kipaumbele cha juu katika masuala ya usalama katika migodi yake.
Barrick nchini Tanzania haijapata ajali yoyote ya kusababisha kifo tangu mwaka 2006 na mgodi wa Bulyanhulu ulitunukiwa Tuzo ya Kitaifa ya ubora katika Mfumo wa Usalama na Afya iliyotolewa na Mamlaka ya Usalama na Afya Kazini, Tanzania, (OSHA), mnamo mwaka 2009.
Wafanyakazi wa mgodi walitoa heshima zao za mwisho kwa wafanyakazi wenzao mgodini hapo kabla ya miili ya marehemu haijasafirishwa kwenda makwao kwa ajili ya mazishi. Shughuli za uchimbaji na uchenjuaji dhahabu zilisimamishwa Machi 18 ili kuomboleza msiba wa wafanyakazi.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Teweli K. Teweli

PR & Communications Manager
African Barrick Gold
+255 (22) 216 4229
+255 (22) 216 4229
+255 767 308 600
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...