TPN (shoto) akipeana mikono na naibu katibu Mkuu wa Red Cross Bw. Peter Mlebusi

mara baada ya kukabidhiwa Misaada hiyo.
TPN Yakabidhi Misaada Ya Wahanga Wa Mafuriko Kwa Chama Cha Msalaba Mwekundu
Katibu Mkuu wa TPN Mzalendo Method Bakuza, alikabidhi misaada ambayo
imekusanywa na TPN na Wadau wake (Jamiiforums.com na issamichuzi.blogspot.com) kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Peter Mlebusi.
Misaada iliyotolewa ni pamoja na: Ndoo 40, Magodoro 40, Sabuni Cartoon 5,
Vyandarua 40, Mablanketi 200 vyote vikiwa na thamani ya TZS 1,619,000 Pia
kulikuwa na misaada ya vitu mbalimbali kama nguo nyingi sana, viatu, vyombo vya nyumbani vyote vikiwa mizigo kama 10 vikiwa na thamani ya TZS 4,600,000 ambavyo vilichangiwa na wadau mbalimbali.
Katika Misaada hiyo SimbaNET Limited ilichangia kiasi cha TZS 1,500,000
ambazo zilitumika kununua misaada hiyo. Misaada hiyo kwa upande wa SimbaNET ilikabidhiwa na Sanctus Mtsimbe, Meneja Mauzo na Masoko wa SimbaNET. Kampuni ya simu za Mkononi ya Tigo ilichangia kiasi cha mablanketi 200 yenye thamani ya TZS 1,600,000.

Kampeni ya Kuhamasisha uchangiaji imeshamalizika huku TPN na Wadau wake wakiwa wamechangia misaada yenye thamani ya karibia TZS 20 Million. Jumla ya watu 2000 Walichangia kwa SMS na kiasi cha Shilingi TZS 2,037,332
zimekusanywa.
Misaada yote ambayo imekabidhiwa ni kwa ajili ya wahanga wa mafuriko katika maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua kubwa.
TPN inazindua Mfuko wake wa Uwezeshaji katika Mkutano Mkuu wa Mwaka
utakaofanyika siku ya Jumapili Tarehe 14-03-2010 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel Ubungo Plaza.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...