hapa ni mtaa wa 3 Stratford Place W1C 1AS, London,
ambapo ndipo ulipo ubalozi wetu ukerewe ambapo shamra shamra za maandalizi ya Diaspora 2 yamepamba moto na wadau kibao wamejiandkisha kuhudhuria mkutano huu muhimu.
MEMBE KUFUNGUA MKUTANO WA DIASPORA 2 LONDON ASUBUHI HII
Na Ripota wetu, London
Maandalizi yameshakamilika kwa ajili ya mkutano wa Watanzania waishio Ughaibuni maarufu kama DIASPORA 2 Conference unaofanyika asubuhi hii katika ukumbi wa The Sattavis Patidar Centre, Wembley Park, London. HA9 (PE UK.
Washiriki takriban 400 kutoka sehemu mbalimbali ughaibuni wanatarajiwa kuwepo kwenye mkutano huu ambao ni wa pili kufanyika, kufuatia ule wa mwaka 2008. Mgeni rasmi kwenye mkutano huu ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernad Membe, ambaye tayari ameshawasili London.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ubalozi wetu hapa London, Shughuli itaanza saa tatu unusu asubuhi kwa wimbo wa Taifa kuimbwa na washiriki wote wakiongozwa na kundi la Glorious Group.
Kitachofuatia ni Mwenyekiti wa Tanzania Association in UK, Bw. Abubakar Faraji kutoa risala ya utambulisho na baadaye wimbo maalumu wa Diaspora utaimbwa ukiongozwa na msanii Fransia Chengula. Mwenyekiti wa shughuli za ufunguzi atakuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha University of Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandala.
Salamu za ukaribisho zitazotolewa na Mh. Balozi Mwanaidi Maajar zitafuatia,naye atamkaribisha mgeni rasmi Mh. Membe kusoma hotuba yake ya ugunguzi. Kura ya shukrani itafuatia baada ya hotuba hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wadau wengi hapa. Mapumziko mafupi ya chai na picha za ukumbusho yatamalizia shughuli za ufunguzi rasmi wa mkutano.
Kesho Jumamosi kutakuwa na shughuli za uchaguzi mkuu wa uongozi wa wanajumuiya ya Watanzania waishi UK. Jioni yake kutakuwa na mnuso wa Libeneke Dinner & Dance Bash litaloandaliwa na New Deal Africa
Kupata ratiba kamili ya yote hayo na mengine
Ama nenda kwenye tovuti ya Ubalozi wetu UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ankal, 3 stratford place ni adress ya ubalozi wa TZ ya zamani, pic. ya juu ni ubalozi mpya>>>>make correction...see you tmr kwenye diaspora.

    ReplyDelete
  2. JAMANI MBONA HATUJAMUONA DIASPORA ORIGINALI NABII MTAKAFIFU YOIHANNA JOHN MASHAKA AMABYE NIDIYE MPIGA DEBE MKUU WA DIASPORA WA RONDONI HATA PICHA YAKE WAKISALIMIANA NA MAAJORI MKUU WA UBAROZI WA TANZANIA UK. MICHU HEBU PIGA PICHA YA NABII NA BAROZI MAAJORI ILI WADAU WAONE HAO MAGWIJI WAKIWA KATIKA JUKWAA MOJA AISEE. HII ITANOGA SANA KWENYE GROBU YA JAMII TUKUFU

    ReplyDelete
  3. Haya, Michuzi, vuka barabara hapo uingie Oxford street uende Primark ukanunue shati, sawa?

    Hako ka fulanaz sasa basi jamani. Shemeji from across the border hakuambii?

    Halafu this time usiingie Ann Summers wala Harmony tafadhali, hizo fedha tumia kwenye kununua mashati, ok?

    Usibanie.

    Mdau, Bloomsbury,UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...