Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo akifungua mkutano huo wa siku tatu wa maafisa Mipango na wachumi kutoka Serikalini unaoendelea mjini Morogoro.
sehemu ya washiriki wa mkutano huo
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango akitoa ufafanuzi kwa wachumi leo mjini Morogoro juu ya muundo wa Tume hiyo na changamoto zinawakabili katika kuhakikisha kunakuwepo maendeleo endelevu hapa nchini. Katibu Mtendaji huyo alikuwa akihudhuria mkutano wa siku tatu wa wachumi ulioandaliwa na Wizara ya Fedha na Uchumi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi Laston Msongole akichangia mada leo mjini Morogoro kwenye mkutano wa siku tatu wa Maafisa Mipango na wachumi inayokuwa inasema kuwa jukumu la maafisa mipango katika maendeleo ya uchumi. Mkutano huo wa siku tatu unafadhiliwa na Wizara hiyo

Picha na Habari na Tiganya
Vincent-MAELEZO-Morogoro

Akifungua mkutano huo juzi, Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo alitoa wito kwa wachumi na maafisa mipango kuandaa sera zitakazosaidia kuondoa matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi wa Tanzania katika kujiletea maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa ni wajibu watendaji hao kuandaa sera nzuri zitakazoweza kutoa majibu juu ya matatizo mbalimbali yaliyopo katika jamii ya Tanzania.

Luhanjo alisema hayo jana mjini Morogoro wakati anafungua mkutano wa siku tatu wa Maafisa Mipango na wachumi.

Alisema kuwa mipango mizuri ni ile inayojaribu kuondoa changamoto zinazokabili jamii kama vile miundo mbinu mibovu, msongamano wa magari mijini, ongezeko la idadi ya watu lisilolingana na rasilimali zilizopo , magonjwa kama vile malaria, UKIMWI na utegemezi wa bajeti kutoka kwa wafadhili.

Luhanjo aliongeza ni vema watendaji wakaanda mipango inayotekeleza kwa kuchagua michache ya kipaumbele kulingana na rasilimali zilizopo ili kufanya mipango hiyo kuwa halisi na inayoleta maenendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Pamoja na kutoa vipaumbele katika mambo machache , Katibu Mkuu Kiongozi pia aliwaagiza Maafisa hao kuzingatia maelekezo yaliyomo katika Dira ya Taifa 2025 na MKUKUTA ili kuwa na mipango mizuri na michache inayotekelezeka.

Alisema wakati umefika kwa Maafisa mipango kuandaa mipango mizuri itakayokuwa ukumbusho wa kazi zao na mchango wao kwa Taifa na raia wake.

Mkutano huo ni wa nne kufanyika ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu yake ni jukumu la Maafisa Mipango na maendeleo ya uchumi.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi,.
    This is good!
    Kwa mara ya kwanza naona Ofisi ya Rais inawaleta wachumi katika kujadili ishu muhimu. This is good na hawa jamaa "wachumi" ndo wanatyakiwa waipe nchi mwelekeo.Hakna nchi hata mojka iliyoendelea bila kuwapa hawa jamaa "wachumi" nafasi ya kuongoza sera na mipango. hata kuho marekani, Singapore, chiona, ulaya na kwingineko kila siku viongozi wa nchi hizo hujadili ishu maalim na wataalamu hawa kila siku. Naamini kabisa kuwa tuna idadi ya wachumi waliobobea katika fani zao na wanaoweza ishauri serikali na nchi vizuri tuu....tatizo ni moja ambalo naliona hapa.....ushauri wa wataalamu hawa ikiwa ni pamoja na sera nzuri zinapogeuzwa kuwa siasa..huwezi pata matokeo yanayokusudiwa...kuna mipango mingi mizuri na ushauri mzuri ambao hawa Wachumi wetu wanautoa kwa serikali na jamii...na aidha hupuuzwa au hutupiliwa mbali kwa sababu mbali mbali hasa "maslahi ya mkisiasa"
    Ni matumaini yetu kuwa Bw. Luhanjo atasimamia mabadiliko katika eneo hili na tuna imani kubwa sana na yeye katika kutatua matatizo ya jamii yetu,...
    Nawatakia mkutano mwema wenye manufaa

    ReplyDelete
  2. Mara kadhaa nimekuwa nikijiuliza hivi Tanzania ina Maafisa Mipango???!! Nawao wanapokea mishahara?? Kwa kazi ipi wanayofanya? Yaani naona hapo wamekaa mkao wa posho tu kisha warudi makazini kwao kusoma magazeti. Mipango gani wakati barabara zinabomoka kamvua hata kadogo kakinyesha, zahanati hazina dawa, foleni Dar za ajabu utadhani nchi haina mwenyewe, maji tabu, umeme kama disco light, Wizii Mtupu!!!

    ReplyDelete
  3. Kama kwako mdau hapo juu. Mimi siku hizi nikiona picha kama hizi presha inapanda na roho inaniuma kabisa kwa kweli. Napata shida kwani sioni output na impact ya vikao kama hivi. Nawaombeni msaada huenda ninashida ya macho. Michuzi kabla ya kuzipiga chini comments uwe unazisoma mara mbili. Sisi wote ni watanzania kwanza na tunaucngungu na nchi yetu haya mambo mengine ni baadaye kwani yameanza juzi tu hapa nadhani ni 1992

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...