Ankal kwanza nakupongeza kwa kutukutanisha wabongo kutuhabarisha.
Mungu awe mbele yako siku zote ili libeneke liendelee. Mkubwa nina
tatizo kidogo naomba uniwekee kwenye blog yetu ili wadau waweze
kunisaidia. Nina gari aina ya Toyota Landcruiser GX automatic model U-HZ J77HV-PEU nyingine IHZ ya mwaka 1992. Tatizo lake ni kwamba huwa inapoteza nguvu inapokuwa kwenye miinuko mikubwa. Haishindwi kabisa kupanda ila huwa inapanda kwa kujirusha rusha. Nimejaribu kuwaona mafundi kama wawili hivi wakaniambia tatizo ni
pump. Pump roter inatakiwa kubadilishwa pamoja na parts nyingine ndogo
ndogo ndani ya pump. Fundi wa kwanza alibadilisha pump roter lakini
tatizo halikuweza kuisha. Baada ya kubadilisha pump roter gari ikawa
inatoa moshi mwingi na nguvu yake kwenye miinuko haikuweza kurudi.
Nikapeleka gari kwa fundi wa pili, yeye aliweza kukata kabisa moshi
lakini tatizo la kupoteza nguvu kwenye miinuko mikubwa liko pale pale.
Wadau, inawezekana miongoni mwetu akawepo mtu ambaye amewahi kupata
tatizo kama langu. Naomba mnisaidie kujua tatizo hapa ni nini hasa na
wapi hapa mjini naweza kupata fundi/mafundi wazuri ambao wanaweza
kumaliza hili suala?

Mdau Kaburu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Nenda kwa dealers, sio mafundi wa chini ya mti.Unaweza kumiliki gari kama hilo, kulitengeneza huwezi?

    ReplyDelete
  2. kwa mimi naona transmission yako inaanza kufa maana nilikuwa na tatizo kama hilo aina ya gari Acura ilikuwa inakufa nguvu nikipunguza mwendo na kwenye vimwinuko kidogowakafanyia computer diagnosis ikaonyesha transmission inashida kwa hiyo waambie waangalie hiyo

    Miss GA-USA

    ReplyDelete
  3. KWANZA KABISA MTAFUTE FUNDI MMOJA ANAITWA HASSAN YUPO HAPO NJIA PANDA YA MAKONDE NJIA INAYOELEKEA MAGOROFA YA PPF UPANDE WA KUELEKA BAHARI, HUYU NI KIBOKO HASHINDWI KITU, KAMA HAPATIKANI HAPO KWA VILE KULIKUWA NA TETESI ZA KUFUKUZWA HAPO NENDA HAPO KITUO CHA MAFUTA JIRANI ENGINE MUULIZIE WATAJUWA HABARI ZAKE. NA KUISHA KWA NGUVU YA GARI ZIKI SABABU NYINGI TU.

    MOJA INAWEZA KUWA CLUTCH PLATE IMEISHA.

    MBILI CUMBELT IMEISHA, GARI ZINGINE HUWA NAYO YA MPIRA ZINGINE ZA CHAIN.

    TATU RING ZA PISTON KWENYE ENGINE ZINAWEZA KUWA ZIMEISHA.

    NNE INJECTOR PUMP KAMA NI DIZEL IMEISHA

    NA ZIPO NYINGINE MUONE HASSAN ATAKUMALIZIA TATIZO LAKO. NI KIJANI WA MAKAMO NA ANAJICHO CHONGO UPANDE MMOJA. KILA LA KHERI MZEE

    ReplyDelete
  4. NJIA PANDA YA MAKONDE NI MBEZI BEACH BARABARANI KUELEKEA TEGETA KABLA NA KARIBU NA INTERCHICK NILISAHAU KUKUELEZA NJIA PANDA YA MAKONDE IPO WAPI, SAMAHANI KWA HILO

    ReplyDelete
  5. pole sana nduguyangu kwanza hiyo gari
    ni enjaction ukae ukijua lazima
    upate fundi wagari hizo sio wale
    wa kujaribu.kuna chombo kama sikosei
    kipo chini ya drow ya gari ndani
    cheusi kibox. ndani kipo kama utumbo wa radio.basi ukibadilisha hicho
    ninaimani litakwisha tatizo lako.

    ahsante

    ReplyDelete
  6. NautiakasiMarch 13, 2010

    Mdau umeongea kwa parables (mafumbo) au ulikuwa unamaanisha ulichoandika! Kama umeongea kwa parables hilo tatizo la gari yako, la kushindwa kupanda "miinuko mikubwa" au kupanda kwa kujirusha rusha litakwishwa ukimuona Dr manyangunyangu kutoka ufipa! Anadawa mujarabu wa matatizo kama hayo, au hata kama "hipigi stata" basi hapo umefika. Lakini unaweza anza kwa kunywa supu ya pweza (watu wa pwani twaita mwengo) na na karanga mbichi usiku. Kwa mchana mihogo mi bichi, shushia na juice ya parachichi...Halfu hiyo gari yako isjali rasmi kwenye mbio za magari,Formula 1 2010... Nakuhakikishia utakuwa bora kuliko Schumacher.

    ReplyDelete
  7. Mdau nimekupata na tatizo lako naamini ni dogo sana ila mafundi unaowapata hawajui kitu wanajaribu kujifunza ufundi kupitia gari lako,sasa tatizo lako linaweza kutatuliwa pale mjini A-Town kwa fundi wa uhakika na anaeaminika East Africa nakupatia contacts zake ni 0754055168 na 0715175217 anaitwa Manyundo ukimpata mweleze tatizo la gari yako na atakupa ushauri nini cha kufanya,mwambie umepata contacts zake kutoka kwa Meneja Marekani,hope utafanikiwa.

    ReplyDelete
  8. Aisee... If the car has a manual transmission, probably the problem is with the clutch assembly. Slipping of the clutch is the probably cause. I'm not in Tz so I can't help you finding the best mechanic.

    ReplyDelete
  9. Transmission problem hiyo.

    ReplyDelete
  10. Mafundi wa kibongo, sorry to say, hawafai..especially kwenye magari haya ya 4x4. wengi wanabahatisha, kaka ningekushauri uende pale Mikocheni, kuna sehemu pamefunguliwa juzi panaitwa Tinys Garage, Old Bagamoyo Rd. Wanabango pale kwenye jengo. Nje nadhani kuna watu wanauza taa za nyumba, wako karibu na shule ya DIS-Dar es Salaam Independent School.

    ReplyDelete
  11. Kaka matatizo ya gari lako inaweza ikwa inatoka na moja kati ya mawili kwa jinsi nielewavyo mie. Moja na la bei ya nafuu ni hilo la pump na mafundi wengi wanapenda kukimbilia kubadili vitu fulani fulani ili wasimtie mteja wao gharama kubwa. Ikiwa ndio hizo rota nozzle na vinavyofanana na hivyo. Tatizo la pili ni kukosekana kwa mgandamizo wa kutocha katika silinda. hii inaweza ikawa inatokana na vitu kama valvu kutoziba vizuri, cilinda kupanuka piston ring kuchakaa na yanosababisha hilo. Ushauri wangu peleka hilo gari International Motors wao ndo wakala wa Toyota Tanzania.

    ReplyDelete
  12. Habaru za huko nyumbani mdau.Kama gari lako mailage yake imezidi 100,000 nakishuri utafute gari lingine maana hilo limechoka.kurudi nyuma katika mtelemko wakati liko kwenye "D" maana yake gari limezeeka.utabadilisha pum hadi gharama za matengenezo zifikie thamani ya gari lakini litaendelea kurudi nyuma.nenda shwroom kachukue kitu.

    ReplyDelete
  13. Bwana kaburu hapo watu wamekuchukulia tu hela wala pump haina ushirikiano na kupoteza nguvu kwa gari lako.Gari la automatic huwa inatakiwa kujibadilisha gears pale ikipungukiwa na nguvu kinajulikana kama (transmission control unit or TCU)na inawezekana kuna faults transmission solenoids zinazoleta shida kwenye gari lako.
    Kama unahitaji mtaalamu, piga simu namba +255754287069 muulizie fundi Kamala atakusaidia.
    Mdau Fau.

    ReplyDelete
  14. Braza,
    Hiyo maanake gari limechoka. Acha ubahili na tafuta gari nyingine. Watu kama nyie ndio mnachangia ku-pollute mazingira. Asante

    ReplyDelete
  15. wote wamesema sawa hila kwa ushauri wa kitaalamu nenda
    TOYOTA PALE PUGU ROAD KARIBU NA QUALITY GROUP AU MAARUFU BANDA LA NGOZI. kwa thamani ya gari yako inakubidi uende pale kwani wao wanawataalamu toka kampuni ya Toyota Japan usiende sijui kwa findi nani au nanai wote wanajaribu pale ndio haswa kazi yao.

    ReplyDelete
  16. Mdau Nautiakasi, Mar.13:03.00AM akili yako iko wapi? mbona ushauri wako na wawenzio uko tofauti sana.

    ReplyDelete
  17. Issue ndogo sana, weka vidonge 2 vya VIAGRA kwenye engine uone itakavyopanda hiyo milima. AS Well chukua tahadhari sehemu unapoipaki usiku maana unaweza kuamka asubuhi ukaikuta juu ya paa la nyumba!

    ReplyDelete
  18. Hao mafundi wanabahatisha...siku zote mafundi wa chini ya mwembe huwa ni makini kuliko magereji makubwa(siku hizi wamekuwa wezi sana)..mi nimeshatumia gari yangu mwaka wa sita sasa (mileage over 110,000km) lakinibado inadunda fresh..ila regular service with genuine parts ni lazima...siri kubwa ni mafundi wangu wa chini ya mwembe(kwa manyota)..kama vipi tuwasiliane

    Mazee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...