bango linaloelezea mradi wa Daraja la Umoja
mwanzo wa daraja upande wa Tanzania
Daraja linavyoonekana kwa karibu
Sehemu ya chini ya daraja inavyoonekana
Daraja linavyoonekana kwa mbali
Daraja linavyoonekana kutokea upande wa Msumbiji

Hellow Kaka Michuzi!
Kwanza nikupe pole kwa kazi ngumu ya kutupatia habari za uhakika kupitia globu yetu hii ya jamii,pia nikupongeze kwa kazi nzuri inayokubalika na jamii yote ya Watanzania.


Kaka Michuzi mimi ni mdau wa globu ya jamii nafanya kazi huku Masasi -Mtwara,na wiki endi iliyopita nilipata bahati ya kutembelea Daraja la Umoja "Unity Bridge".


Kwa kifupi tu kaka ni kuwa daraja hili linavuka mto Ruvuma na lipo eneo linaloitwa Mtambaswala (Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania) .Daraja hili ndo linaunganisha nchi yetu ya Tanzania na majirani zetu Msumbiji,na limejengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Msumbiji.Kaka Michuzi daraja hili limeshakamilika tunasubiri tu sherehe za ufunguzi.

Kaka Michuzi daraja hili ni muhimu sana kwa sababu sasa linatuunganisha wananchi wa nchi mbili hizi,matokeo yake ni kuwa tunategemea mabadiliko makubwa kiuchumi,kibiashara na kwenye nyanja nyinginezo kama michezo.
kaka Michuzi sasa safari yetu ya kwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia mwezi Juni hapo Afrika Kusini imerahisishwa kupitia daraja hili la Umoja.

Mwisho kaka Michuzi kwa niaba ya wadau wote wa Ukanda huu wa Kusini mwa Tanzania nifikishe shukrani za dhati kwa viongozi shupavu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Msumbiji.

Ahsante
Mdau
Eng.Jimmy Wilbard-
Ingerosec Corporation
The Project for Improvement
of Masasi -Mangaka Road






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. kweli uchaguzi unakuja du ni kiboko ndugu zangu

    ReplyDelete
  2. Hu ni uchaguzi tu akuna jingine mkuu wetu michuzi vipi kure kusini sio nyumbani kweli ?

    ReplyDelete
  3. Uchaguzi uchaguzi uchaguzi............ tu apa akuna jipya

    ReplyDelete
  4. ANSANTE MHESH. RAIS MSTAAFU BENJAMINI MKAPA: BADO MBEGU ULIZOPANDA WAKATI WAKIPINDI CHAKO SASA ZINZIDI KUTOA MATUNDA; DARAJA SAFI: BARABARA KUU DODOMA TO MWANZA; MTUKULA KAGERA TO BURUDI KUPITIA BUKOBA: BAHATI MBAYA KAZI ULIYOWAACHIA BARABARA MBAGARA WAMESHIDWA KUMALIZA; WEWE ULIKUWA MTU WA VITENDO NA SI MPIGA MDOMO! UBARIKIWE SANA.

    ReplyDelete
  5. Tuombe Mungu hili daraja lisiwe sehemu nyingine ya kupotezea maisha ya wananchi wa pande zote mbili. Maana kila siku twasikia ajali ajali ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva.

    ReplyDelete
  6. Ankali Asante kwa kutuhabarisha, madau asante kwa kutuma picha kwani hata siku nyingine nikiona picha kama hizi nitakumbuka hili ni daraja letu la Muungano na wala sio lango la kuingilia jiji la Mombasa. na wao wana pembe kama daraja letu sema za kwao zimeunganika. shukran Mdau ugaibuni

    ReplyDelete
  7. Sioni ofisi za uhamiaji jirani. Kumbe kwenda Msumbiji huitaji kuwa na passport? inapendeza sana.

    ReplyDelete
  8. Eng.Jimmy Wilbard,hakuna kunywa bia wala kuhama mpaka mkamilishe Tunduru-Masasi na Songea-Tunduru Road,Mdau wa south.

    ReplyDelete
  9. hili ndio daraja alojenga mkapa,lile la mwanzo likaitwa mkapa brige ni la mzee ruksa ndo alojenga,kila kiongozi wa tz atakumbukwa kwa kazi zake.

    ReplyDelete
  10. ASANTE SANA ANKAL KWA TASWIRA NZURI.HAPA HAKUNA SUALA LA UCHAGUZI BALI NI MRADI UMEKAMILIKA KWA KALENDA YAKE.SASA NAOMBA WADAU MNIJULISHE KUPITIA DARAJA HILI SAFARI ZA MABASI NA MALORI YA MIZIGO KATI YA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI ZITAKUWA ZIMERAHIRISISHWA KADRI GANI?

    ReplyDelete
  11. SAFI SANA MH. MTUFUFU RAISI KIKWETE KWA KAZI YAKO NZURI YA KUSIMAMIA WATENDAJI WAKO MPAKA KITU KEELEWEKE.

    HAYA NDIO MAENDELEO KWANI DARAJA HILI LITAFUMUA MLIPUKO WA SHUGHULI ZA KIUCHUMI NA BIASHARA.

    ASANTENI MAIINGINIA VILEVILE.

    KIKWETE UNA KULA YANGU BILA YA WASIWASI WOWOTE.

    M/MUNGU AKULINDE NA UENDELEE KULITUMIKIA TAIFA LETU.

    ReplyDelete
  12. nawapenda hawa jirani zetu wapole, sijasikia vurugu nao, great neighbors, hapo pia dili ya magari inakua poa, badala ya kupitishia bandari ya dar, i might try msumbiji then drive hapo darajani, poa sana.

    ReplyDelete
  13. ooh Mkapa hakufanya kazi....vitu alivyofanya vinaonekana. Vingine vimemalizikia tu awamu hii. Angeendelea kubaki madarakani tungekuwa mbali zaidi kuliko ilivyo sasa....Maoni yangu tu!... Michuzi usibanie hii

    ReplyDelete
  14. Wajumbe ukiwa na gari bishi unaweza kwenda kucheck world cup SA kutokea TZ kiulaini. Dar Masasi km 596, Masasi-Maputo haizidi na haipungui 2300km, Maputo J'burg 605km. Kwa km hizi world cup haujaliona bado?

    ReplyDelete
  15. Mdau wa Sat Mar 13, 03:13:00 AM,
    Ku-plan, Consultancy Services za Ku-design, mpaka construction ni miaka! Kujenga 720m Concrete Bridge kwa Uchumi wa Tz sio fast kama unavyofikiri ni uchaguzi! Fikiria zaidi kila wakati!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...