Pole na majukumu ya kila siku ya kuuhabarisha umma wa watanzania.
Mimi naishi Sinza Mori. Leo asubuhi nimepotelewa na Mbwa wangu aitwaye TIGER (Pichani). Inaaminaka kuwa ameibwa kwani alionekana akiwa ameambatana na kijana asiyefahamika.

Kwa yeyote atakayemuona naomba awasiliane nami kwa namba
0652877595 au 0655680037
au njoo SHIENI BAR na uliza KITEGO utanipata.
Zawadi nono itatolewa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Swali,
    huyo mbwa ni wa ulizni au ni wa urembo "pet".

    ReplyDelete
  2. SHILLINGI ngapi?

    ReplyDelete
  3. Pole sana ndugu. Jaribu kucheki vichwa vya mbwa waliochinjwa leo kwenye hoteli za wachina. Mbwa siku hizi dili.

    ReplyDelete
  4. kapotea mbwa ulikuwa wapi? manake kama tu ulimwacha humpi chakula siajabu kapata mtu atakaemlea vizuri.

    ReplyDelete
  5. wabongo na mbwa kama "PET" toka lini? siajabu jamaa ni mhehe huyu anataka kwenda kufanya mambo yake.

    ReplyDelete
  6. NdumbaNangaeKamosingaMarch 25, 2010

    Huyo alishafanywa ndafu Iringa, ni vyema tu ukafanya misa ya kushukuru.

    ReplyDelete
  7. ha ha ha hawezi kuwa mbwa labda mdoli

    ReplyDelete
  8. DUH UZUNGU SASA UNAINGIA BONGO TIGER AME CHEAT. HAHAAHA TUTAANZAK UONA MATANGAZO YA PAKA NA PANYA PIA SOON.

    ReplyDelete
  9. HUYO UKIMTAKA NENDA BEACH TUU. WATOTO WAKIWA NA MBWA LAZIMA WATAENDA NAYE BEACH WEEKEND..

    ReplyDelete
  10. Pole sana. Ni wazi kwamba huyo si mbwa wa ulinzi mdau wa kwanza.

    ReplyDelete
  11. Ndo maana amepotea...utamwitaje Tiger? Tiger hawakai nyumbani wanakaa porini..tena India ndo wako wengi...usikute ameenda India...!!Mdau-NYC, USA

    ReplyDelete
  12. Kumbe mbwa mlinzi naye anaweza kuibiwa!!.

    Pole kwa kupotelewa mbwa, nakuombea apatikane.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  13. Huyo boby mpaka amefikia kupotea ama kuibwa - ameshakuwa ukoko na kama tena umekuwa ukimpa mananasi na matikiti maji basi huyo kehskuwa wa wote...afterall ni wa kike..... Nakushauri umsahau...

    ReplyDelete
  14. Male or female!!yaani jinzia yake ni ya kiumeni au kikeni - toa picha ya pande ingine pls

    ReplyDelete
  15. Hatutaki zawadi zaidi ya kitoea kinono kama hiki bei poa sana IRINGA

    ReplyDelete
  16. TK ha haha ah aa.....uzungunaisheni

    ReplyDelete
  17. Tumieni lugha zinazoeleweka kuandika humu maanake tunatumia nguvu nyingi kuelewa! Mara 'ahamue' 'anahamua' mwisho na ninyi 'mtahamua' hovyo hovyo. Mnafikiri Kanyigo hapa.

    ReplyDelete
  18. Waliotoa maoni ya hovyo hovyo hawajui mbwa ni nini na thamani yake. Kwataarifa, hawa wezi wa mbwa ni professional,wanapoamua kumuiba mbwa hata awe mkali namna gani watamuiba tuu. Na haya matukio ni mengi ya kuibiwa mbwa. Ok it depends umekulia wapi na unatokea mazingira gani, nyie ndo wale mkiona mbwa mnapiga kwa mawe hadi anakufa.
    Kaka pole Mungu atakusaidia utampata tuu, Tuko pamoja.

    ReplyDelete
  19. Dah Pole Mzee.. ungekua Abidjan, Paka na na Mbwa wanaliwa! Afadhali kapotelea Bongo.. kama mdau wa juu kasema, ni kutazama kwa wachina na ndugu zetu wa asili ya kusini!!

    ReplyDelete
  20. Mama yangu, WACHINA wameshakula huyo. Mimi jirani zangu wachina wamekula wangu wawili. mpaka nilivyowabana na kutaka kuwapeleka polisi ndio walikubali...

    ReplyDelete
  21. AISEE NDIO NIMEIONA POST YAKO SASA HIVI KWA KWELI NAKUMBUKA JANA NIKIWA KWENYE FOLENI JANGWANI NILIMWONA KIJANA MMOJA AKIWA MAENEO YA JANGWANI ANAELEKEA K/KOO NA HUYU MBWA ILIKUWA KWENYE MCHANA HIVI YAPATA SAA NANE KITU KILICHONIFANYA NIMWANGALIE HUYU MBWA NI KUWA ALIKUWA AMECHOKA AMEKAA CHINI SASA JAMAA AKAWA ANAJARIBU KAMA KUMPUSH LAKINI IKASHINDIKANA IKABIDI ASUBIRI NAE PALE HUKU ANAJARIBU KUMVUTAVUTA KIAINA NA NAKUMBUKA JAMAA HUYO ALIKUA NI KIJANA AMEVAA SHATI KAMA JEUPEJEUPE HIVI NA ALIKUWA AMEMSHIKA NAKUMBUKA KAMA HUO MNYORORO HIVI SHINGONI,POLE SANA KAMA NINGEKUA NIMEIONA HII TAARIFA YAKO MAPEMA NINGEMSHTUKIA.

    ReplyDelete
  22. pole mdau.. huyo kwishne ameshageuzwa kitoeo.. nenda pande za Mwalimu Nyerere pale kuna apartment imejaa wachina nakuhakikishia utampata.. ila condition moja unda urafiki na afisa uhamiaji ndio umshawishi muende wote... mimi nililipwa keshi baada ya kugundulika kuwa walishamfanya kitoweo...

    ReplyDelete
  23. HUYU MBWA NA PASSPORT NAMBA AU???

    LABDA NAWEZA KUMTRACK.????

    ReplyDelete
  24. DUH KAMA KAELEKEA IRINGA UJUE KAUMIA WAHEHE HAWAMUACHI NDIO WAHEHE. KIMARO.

    ReplyDelete
  25. Pole sana. Na wazazi wangu wameibiwa Mbwa pale Tangi Bovu majuzi. Tulikuwa tunamwita 'Baby'. Rangi yake ni Brown, dume, mkubwa kiasi. Baby ana miaka minne.

    Tuache utani pembeni, miaka ya 90, ilibidi watu wafiche mbwa wao Dar, kwani ni kweli watu walikuwa wanawaiba na kuwuuzia waChina/Japani. Eti walikuwa wanakula nyeti zao!

    ReplyDelete
  26. AISEE HUYO KIJANA LAZIMA ALIKUWA NA ODA YA WACHINA. NDIO IMETOKA HIYO, SAA HIZI UTAAMBULIA NGOZI TUU KAMA UTABAHATIKA KUIONA... HAWA WACHINA WAKIMALIZA MIAKA ISHIRINI HAPA MBWA WATAKUWA WAMEISHA KABISA..


    Mzozaji

    ReplyDelete
  27. sasa kaka wewe umepotelewa na mbwa au chui???

    ReplyDelete
  28. watanzania bwana sasa nyingine natamani nihave hii inchi, watu wengi emeandika comments zao kuhusu mbwa kama vile jambo kubwa sana mbona hamuongelei ile ajali ya kule sijui kibaha, na hiyo yote ni kwa ajili watanzania hawapendi wanyama ambao watu wanasafiri miles and miles to come and see animals.. Dogs are very good animals i have 5 and they are part of our family. mbwa kuibiwa jambo la kawaida sasa badala ya kumsaidia mwezetu kupata mbwa wake watu wanapoteza mda kuandika upuuzi. badilikeni, i wish i could help you to get that dog

    ReplyDelete
  29. Mbwa ameibwa?

    ReplyDelete
  30. Nashukuru kwa wale watu waliozaliwa na busara kwa maoni yao ya faraja na ya kusaidia. Nimeanza kupata tetesi wapi mbwa aliko na nimepigiwa simu nyingi ambazo zimekuwa msaada mkubwa sana kwangu. tutumie technology hii vizuri-AKSANTENI!

    ReplyDelete
  31. kama kweli huyo jamaa aliyekuwa kwenye foleni maeneo ya jangwani alimuona huyo mwizi wa mbwa akielekea kariakoo baasi atakuwa ameenda kuwauzia wachina tu! manake kuna wachina wengi sana kariakoo na soon itageuka china town!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...