Ankali Michuzi
Ona hapo mambo ya Technohama sasa Dr Manyuki
anapatikana kwenye tovuti kwa wanaohitaji huduma zake
Hili bango nimeliona pale morocco this afternoon.

Naomba kuwakilisha mkuu.
Mdau Mac Temba Jr
Sent from my BlackBerry®
smartphone from Vodacom

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. safi sana manyuki,unakwenda na wakati

    ReplyDelete
  2. Dr. NatureMarch 24, 2010

    matatizo ya nguvu za kiume Afrika yalikuwa matatizo kwa watu wachache sana ingawa siku hizi yanakuwa matatizo ya kawaida tena yanawaathiri mpaka vijana. Dawa ni kula chakula kizuri na kuacha kunywa pombe kibwegebwege. Uzuri wa Afrika ni kwamba, chakula kizuri kina bei rahisi kuliko chakula kibovu.

    Chakula kizuri...(kisamvu, bamia, mchicha, fenesi, dagaa, wali wa maji, ugali,....na kuendelea)

    Chakula kibovu...(Lager, chips, kuku wa kizungu, pilau, biryani,fanta,...na kuendelea)

    ReplyDelete
  3. yaliyomo yamoMarch 24, 2010

    dr manyuki ana mtandao ilhali wizara na idara za serikali hazina? duh!
    nadhani hata mwanyanyamala hospital haina mtandao - hata ka-blogu.

    ReplyDelete
  4. Ni vizuri kuwa na web site ila: Tuache kujiita maDoctor na ma Profesa bila kupita shule. Kama unabisha: Mtafute mtu aliyeondoka na grade 1 A level, akasota 5 (FIVE!) years pale muhimbili na kula sana cadaver (if you dont know how, feel free to ask)ili aitwe doctor akueleze.
    Otherwise mie naona hii ni kanyaboya, watu wamekaa mwendo wa kula tu. Kwani sio wakati wote size matters!!!
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  5. ebwana hii nimeikubari sana maana sasa ifike wakati watu wafanye vitu vyao international maana watanzania tuko nyuma sana kwa haka katechnologia labda na wengine watamwiga dr. kwa kuwaonyesha njia nikimaanisha tekinolojia ya habari ndio njia rahisi ya mawasiliano kwakweli

    ReplyDelete
  6. 1)Anauwezo wa kukuondolea nuksi na mikosi mbalimbali
    2)Anasaidia kurudisha mahusiano yaliyovunjika.
    3)Anatibu matatizo ya mimba
    4)Anakomesha uchawi wote, mizimu, nuksi, balaa, na mikosi.
    5)Anarudisha mpenzi uliyepoteza naye kwa muda mrefu.
    6)Anasaidia kufuta kesi, talaka, na madeni sugu.
    7)Anavidonge vya kupunguza uzito.
    8)Anasuluhisha matatizo ya kifedha nay a kifamilia.
    9)Anauwezo wa kuridisha mali iliyopotea
    10)Anaweza kukupa dawa ya mvuto kwenye biashara yako.
    11)Anaweza kukusaidia kupandishwa cheo.
    12)Ana mchanganyiko wa wa dawa za kuinua hamu ya kufanya mapenzi.
    13)Ana dawa ya kunenepesha uume hivyo kuweza kumridhisha mwenzi wako.
    14)Anaponya uchizi, msongo wa mawazo, utegemezi (addiction), kuugua kwa muda mrefu.
    15)Anatibu magonjwa ya zinaa kwa muda mfupi.
    16)Anatibu matatizo ya kufika kileleni kwa haraka.
    17)Ana dawa maalum ya kukukinga na wezi wa gari lako, watekaji, wizi wa mali


    Duh! wote chezea dr. manyuki kiboko chao... mimi nimeipenda hii ya kufuta kesi na madeni sugu; na ile ya kukuwezesha kupandishwa cheo. tehe tehehe

    ReplyDelete
  7. Hongera kwa hatua nzuri ya kimaendeleo uliyoichukua.

    Hata hivyo, lugha ya kiingereza iliyoandikwa inaweza kua tabu kueleweka hasa kwa mtu asiyejua kiswahili (ni kiswahili kilichowekwa katika maneno ya kiingereza au kwa maana nyingine alieandika alikua anafikiri kwa kiswahili huku akiandika kiingereza).

    Tafuta mtaalamu wa lugha tena ya kibiashara ili akuwekee sentensi fupi zenye mvuto na kuleta maana kirahisi.

    mdau
    Easy K

    ReplyDelete
  8. manyuki kiboko ana uwezo wa kujenga flyover!!!

    ReplyDelete
  9. Wajinga ndio waliwao.
    Hii ni biashara, na kimsingi anatafuta njia ya kudanganya watu ili ajipatie fedha za kimaisha.
    Waganga wote wizi mtupu

    ReplyDelete
  10. Mr. Mpingo Mweusi, I think you were "disco-d" from Muhimbili that is why you dont call yourself Doctor. But this is life, aliewahi amewahi and late commers wll die. Let Dr. make his life on foolish people, who believe on super powers. Mdau Ex Paramedical

    ReplyDelete
  11. Kwa nini nguvu za kiume kila siku, za kike je?

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  12. Rafik ReakaMarch 25, 2010

    Kwani huyu na sheikh Yahya tumshangae nani zaidi na ni nani mwenye mchango hasi zaidi kwa Afya na hata mahusianio katika jamii?

    Kwa taarifa tu ubashiri una uongo mwingi na unaleta hofu na au matumaini yasiyo kweli kuliko tiba za baadhi ya waganga wa jadi wanaotumia dawa asilia ambazo baadhi yake kweli zimegundulika kisayansi kuwa na chemical components!

    Tuache uvivu! tembeleeni tu hata hapa Muhimbili Chuo Kikuu cha Tiba Asilia msomeshwekinachoendelea!


    Hata nchi zilizoendelea Alternative Medicine zipo na zina nafasi yake.

    Cha msingi ni kuwapiga marufuku wale waongo na matapeli wanaojisingizia kuponya wasichoweza kama vile ambavyo pia kuna madaktari wetu na Wauguzi ambao wanajifanya kuweza kila ugonjwa na wengine wana mistreat wagonjwa na hao pia wanatakiwa kunyangánywa hizo registration cert zao.

    Ni vyema tuwe na mtizamo wa kuhimiza tafiti na kuendeleza tiba zetu asilia ili ziwe zenye ufanisi kama wengine walivyofanya mfano China, Japan, USA, n.k kuliko kubeza tu kila kitu.

    Mwisho wa yote;

    "Tiba ya Kisasa imetokana na Tiba asilia, jadili!"

    ReplyDelete
  13. Ndumbanangai! Hiyo statement inatumika zaidi kuashiria waganga wa kichawi (witch doctors). Sijui Manyuki yupo upande gani, but I'm a proponent for natural medicine...sio tunguli.

    Ingawa siamini baadhi ya tiba anazodai kufanya bwana Manyuki, nafikiri waganga wa miti shambe wako under-appreciated.This is a noble profession...in the same category with MDs, Health Therapists of all kinds. They are HEALERS.

    Wengine wamejifunza miaka na miaka kazi hiyo, wamejifnza mizizi mamia kwa mamia, na combinations kadhaa kutengeneza dawa. Wapo walioponya thousands of people that MDs could not.

    Wewe unayesema waganga wote wizi mtupu....negro please!. Majani na mizizi hiyo hiyo ukipewa na mganga kutoka kijijini Mpapore utasema ni tapeli, lakini ikiwekwa katika pills ama kichupa charangirangi na kupewa jina la kizungu...utatumia...tena hata kikiuzwa $30. What's the difference? Mganga wa kijiji cha Mpapore ametumia ingredients in their purest forms while the dude from GNC or any "Health food, suppliment store" anatumia ingredients zilizoharibika baada ya kupitia process kibao.

    Who are you to suggest that he can't be called Doctor?. Waganga wengine wamejifunza kazi hiyo miaka zaidi ya kumi kutoka kwa wataalam. You're talking about 5 years!. Would it be ok to use that designation if he had a PHd of Natural Medicine?

    Tuache kudharau wataalam wetu. Wapo matapeli na wengine ni legit. Wapo wanaofata maadili na wengine wasiojali. Dr Conrad (Dokta wa marehem Michael Jackson) was "a good doctor" right? reputable and all that stuff.

    But look at what he did to the man. Miaka yote ya shule aliyosoma haina thamani kama amejali zaidi fedha kuliko usalama wa mgonjwa wake. That's worse than that guy selling harmless herbs under the tree shade at Magomeni Mapipa bus station.

    Dawa nyingine huenda hazina athari ya kutibu lakini watu kadhaa hupona thru the power of their own minds or placebo effect. If it's harmless...let the man do his thing to earn a living. Some people may benefit.

    Zipo dawa kibao tunapewa hospitali wala hazihusiani na magonjwa tunayoumwa lakini tunapona by placebo.

    By the way....have you all heard about NEEM products? what about Aloe Vera?

    Kikopo kidogo cha pills za NEEM ni $14 in the US (It is FDA approved). Aloe Vera is pretty popular, but NEEM? thats Mwarobanini....inaaminika tuwa na health benefits nyingi sana...huweza kufika 40!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...