Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akipata maelezo ya mfumo mpya wa utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za wateja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutoka kwa Afisa Nyaraka wa mfuko huo Bw.Erastus Msigwa jijini Dar.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akizindua ramani inayoonyesha mtandao wa vituo vya matibabu vya ngazi mbalimbali na sehemu vilipo hapa nchini mara baada ya kutembelea Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya leo jijini Dar es salaam.Kulia ni Mganga Mkuu wa serikali Dkt Deo Mtasiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Emanuel Humba (aliyesimama nyuma ya waziri)
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Emanuel Humba(katikati) akimwonyesha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa maeneo mbalimbali na namna Mfuko huo unavyoendelea kuboresha miundombinu na kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi ili kuinua utoaji wa huduma kwa wateja.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akipata maelezo ya namna mtambo mkuu wa kuhifadhi kumbukumbu (main server)unavyofanya kazi ndani ya ofisi za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
Meneja Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Ellentrude Mbogoro akitoa ufafanuzi juu ya mfumo mpya wa uhifadhi wa Nyaraka na kumbukumbu za wateja kwa kutumia teknolojia ya kompyuta kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa (aliyekaa katikati) akifuatiwa na Mganga mkuu wa Serikali Deo Mtasiwa (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Emanuel Humba (wa kwanza kushoto.
Picha zote na Aaron Msigwa - MAELEZO.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mimi sio mnyakyusa lkani wanyakyusa wakiwekwa sehemu hufanya kazi sawa sawa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...