Ndugu yangu, nakupongeza kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya. Huwa napata picha za matukio mbalimbali. Nimeona ni vema niwe nakurushia ili wadau wa blog ya jamii waweze kufaidika nazo. Kwa kuanzia, nakupa hii picha ambayo nimeipiga wikiendi hii katika Hifadhi ya Loliondo mkoani Arusha. Watu wanadhani ngumi ziko mkoani Mara tu, na kusahau kwamba hata hawa ng'ombe wa Loliondo nao wana "Tarime" yao.
Na mdau Manyerere Jackton
Na mdau Manyerere Jackton
mbona hujatoa sababu ya hao ng'ombe kupigana.
ReplyDeleteChanzo cha ugomvi ni huyo jamaa wa kulia alimwambia jamaa wa kushoto mwenye baka jeupe kuwa ana mbalanga
ReplyDeleteWakatabahu
Nyote mmekosea hawa walikua wanagombea kadem kapya ka mtaa wa pili
ReplyDeleteAnko naomba umuulize kaka Manyerere, Loliondo imekuwa lini hifadhi? LoL
ReplyDeleteLoliondo ni hifadhi sababu wanaishi wamasai, na wamasai kwa kibongo bongo wanatambuliwa kama kivutio cha watalii, yaani hawana tofauti na wanyama wa porini, ndo maana unaona kwenye matangazo ya utalii wanatumia picha za wanyama pamoja na wamasai! na ndio maana ni wamasai pekee wanaruhusiwa kuishi ndani ya hifadhi ya taifa kama ngorongoro au serengeti.
ReplyDelete