Mwaliko huo ambao umetoka kwa Spika wa Bunge la Uturuki Mhe. Mehmet Ali Sahim amemwomba Mhe. Spika kutembelea Uturuki pamoja na Bunge lao ili kujionea shughuli mbalimbali za Bunge, Maendeleo na kiuchumi ikiwa ni jitihada za kukuza mahusiano kwa nchi hizi mbili pamoja na kuwahamasisha waturuki kuja kuwekeza chini katika sekta mbalimbali.
Mhe. Balozi amesema hivi sasa Waturuki wengi wanataka kuwekeza katika nchi za kiafrika hususani katika sekta za viwanda vya Nguo na Utalii. Hivyo itakuwa fursa ya kipekee kwa viongozi wa kitanzania kutembelea nchi hiyo ili kujionea mambo mbalimbali kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuweka hamasa ya kukuza ushirikiano wetu kati ya Uturuki na Tanzania.
Akiwa nchini Uturuki, Mhe. Spika ameombwa kukutana na Rais wa Nchi hiyo, Vioongozi mbalimbali wa Bunge pamoja na waturuki wanaofanya biashara na Tanzania. Aidha Balozi Qubuz ameomba katika msafara wa Mhe. Spika, aweze kuambatana na wabunge wachache wa chama cha uhusiano wa Tanzania na Uturuki kinachoundwa na Wabunge wa Tanzania.
Amesema, ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kikwete aliyoifanya hivi karibuni nchini uturuki imefungua mlango mkubwa kwa nchi hizi mbili kuweza kufanya biashara kwa ukaribu zaidi hali ilnayofanya uturuki kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja toka Dar es salaam hadi Istanbul kuanzia juni 10 2010.
Anasema baada ya ziara ya Mhe. Rais hivi sasa zaidi ya maombi 25 ya visa huwasilishwa kila siku katika ubalozi wa uturuki kwa watanzania wanaofanya biashatra na wenzao wa uturuki ikiwa ni matunda ya ziara hiyo.
Mwaliko huu wa ziara ya Mhe. Spika nchini uturuki utakuwa ni wapili kufanywa na viongozi wa Tanzania katika nchi hiyo na amesema awamu nyingine wangependa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa nae aweze kutembelea nchi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...