Ndugu yangu, nakupongeza kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya. Huwa napata picha za matukio mbalimbali. Nimeona ni vema niwe nakurushia ili wadau wa blog ya jamii waweze kufaidika nazo. Kwa kuanzia, nakupa hii picha ambayo nimeipiga wikiendi hii katika Hifadhi ya Loliondo mkoani Arusha. Watu wanadhani ngumi ziko mkoani Mara tu, na kusahau kwamba hata hawa ng'ombe wa Loliondo nao wana "Tarime" yao.
Na mdau Manyerere Jackton

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. mbona hujatoa sababu ya hao ng'ombe kupigana.

    ReplyDelete
  2. Chanzo cha ugomvi ni huyo jamaa wa kulia alimwambia jamaa wa kushoto mwenye baka jeupe kuwa ana mbalanga
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  3. Nyote mmekosea hawa walikua wanagombea kadem kapya ka mtaa wa pili

    ReplyDelete
  4. Anko naomba umuulize kaka Manyerere, Loliondo imekuwa lini hifadhi? LoL

    ReplyDelete
  5. Loliondo ni hifadhi sababu wanaishi wamasai, na wamasai kwa kibongo bongo wanatambuliwa kama kivutio cha watalii, yaani hawana tofauti na wanyama wa porini, ndo maana unaona kwenye matangazo ya utalii wanatumia picha za wanyama pamoja na wamasai! na ndio maana ni wamasai pekee wanaruhusiwa kuishi ndani ya hifadhi ya taifa kama ngorongoro au serengeti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...