ANKAL:- Mdau wa Libeneke,
Mkuu nime attach picture hiyo iweke hapo wadau wa weze kuona jinsi mansipaa ya mji wa Al-Khobar na selikali kwa ujumla nchini Saudi wanavyoboresha sehemu za kupumuzikia raia wake na wengine wote. picture hiyo uki angalia vizuri ina parking kubwa tu ya kutosha gari mia mbili, kule pembezoni hiko nyengine parking zote hizo ni free no CHARGES.
Mkuu nime attach picture hiyo iweke hapo wadau wa weze kuona jinsi mansipaa ya mji wa Al-Khobar na selikali kwa ujumla nchini Saudi wanavyoboresha sehemu za kupumuzikia raia wake na wengine wote. picture hiyo uki angalia vizuri ina parking kubwa tu ya kutosha gari mia mbili, kule pembezoni hiko nyengine parking zote hizo ni free no CHARGES.
Kuna kijumba cha rangi ya blue kwa chini hivi ni beach PUBLIC TOILET for ladies n gents pia no charges ever clean kuanzia asubui mpaka jioni na wafanyakazi ni wa dosi kwakweli wanafanyakazi asubui hadi jioni,sehemu za beach huku ni safi na ninyingi sio sehemu moja tu kama ilivyo coco beach, fukwe zote za beach huku ni manispaa ndio muhusika mkuu, play grounds za watoto za ku mwaga fast foods rest'ts zimejaa beach kwa ajiri ya wanao kula raha zao beach.
Ukiaangalia Saudi sehemu kubwa ni jangwa lakini angalia miti hiyo beach na majani, je beach kinashindikana nini kua kama hivyo, hiyo risiti ya parking ya Mdau wa Oysterbay ni wizi tu ya hao mafisadi hawajatosheka haina hata nembo ya selikali za mitaa au manispaa, sasa huo si wizi tu wa wazi kabisa.
Mdau wa- Al-Khobar,
Chief Edochi.
Mdau wa- Al-Khobar,
Chief Edochi.
ha ha ha ha ha ha!!!!
ReplyDeletehata ulete picha za arabuni wewe unavunga!!!
ha ha ha ha ha ha!!!!
CHELSEA wamefulia ha ha ha ha ha ha!!!! Misupu umefuliaaa
ha ha ha ha ha ha!!!!
Asante sana mdau kwa kutuletea taswira hii.Bila kutafuna maneno mamlaka za miji yetu hapa bongo zimeshindwa kutambua wajibu wake kwa jamii husika.Wanapita tena na vipaza sauti wakidai wafanyabiashara wakalipie huduma za Jiji lakini huduma hizo kuanzia vyoo vya umma,parking na nyingine zote zinalipiwa tena kwa bakora.
ReplyDeleteMiji yetu imetawaliwa na uchafuzi wa mazingira na askari wa jijini wanavizia wachinga na mama lishe ili mwisho wa siku mfuko yao ijazwe matembele.Hakuna anayejali huduma bora kwa wananchi wavuja jasho lakini kwa wenzetu kodi za wananchi zinawarudia wenyewe kwa raha zao.Hongera Saudia!!!!!!!!!!!
Safi sana na inapendeza kupita kiasi. Mungu awazidishie neema
ReplyDeleteLakini kumbuka kuwa kila mtu na nafasi yake.Aliyewapa ndiye aliyetupa, wengine awapa makengeza,wengine chongo na wengine upofu, ukitaka kuuliza WHY utakufuru.
Tupo nyuma sana lakini inshallah tutafika tu siku moja.
I am not sermonising anyone, but I am just thinking "loudly" it helps me to keep my faith and remain sane
Mungu ibariki Tanzania
Tatizo ni risiti? Subirini sasa tuzihalalishe! Halafu zaidi ya parking tutaleta na kiingilio cha beach kwa kichwa, si mnajifanya mabwege? Watu mnakamuliwaaaa kimya! Toka lini mlipakodi (PAYE, Biashara, VAT, Baiskeli etc) bado manalipishwa kiingilio cha kumpokea mgeni stendi?
ReplyDeleteMwanzoni umeandika vizuri ulipokuja kuchefua hali ya hewa hapo ulipoikandia bongo hali unaijua wahusika wameziba masikio japo wengi wao wanasoma hiii Blog hawana mpango na walipa kodi wao wala nini,cha kufanya tukae chini tujiulize nini tufanye tusiwe wanafiki,Leo Ndio,kesho Hapana,MSISAHAU MBUYU HAISHINDANI NA MGOMBA,,UKIMUIGA TEMBO KUNY..MAV MAKUBWA UTAPASUKA NANI HII
ReplyDeleteWAKATABAHU
NAGAL WASHNGTON
PAMOJA NA ULIYOYASEMA NI SAHIHI NA TANZANIA TUNATATIZO LA VIONGOZI AMBAO BADO WANAFIKIRI NDANI YA BOX TU, WENYE NGUVU ZA SODA UNAPOIFUNGUWA NDO INAFOKA IKIPIDA SEKUNDE TU NGUV IMEISHA, NI KWELI TUNATAKIWA KUIGA WENZETU BEACH ZOTE TOKA TANGA HADI MTWARA NI BISHARA NZURI TU KWA WATALII. LAKINI MWISHO KABISA HATUWEZI KUJILINGANISHA NA SAUDI ARABIA, NI WATU MATAJIRI, WANA PETROL DOLLAR, PESA NI ZA KUMWAGA WANAWEZA KUFANYA KILA KITU BURE KWA WANANCHI WAO, SERIKALI HUWA INAGAWA HADI CHAKULA KWA WAZAWA WAO KILA MWEZI NA POSHO NYINGINE KIBAO TU, PETROL DOLLAR INAFANYA KAZI, PAMOJA NA YOTE HAYO NI UONGOZI MZURI KIDIGO NA KUWA NA JAPO ROBO HURUMA KWA WANANCHI, PAMOJA SI WAZURI SANA KWA HAKI ZA BINADAMU NA WAO PIA, WAMEBADILIKA SIKU HIZI ZA KARIBUNI TU BAADA YA MAKUNDI YA WAZAWA KUWAAMUSHA WENZAO NA KUANZA KUOPIGANIA HAKI ZAO. NDO WANAJARIBU KUWAPIGA CHANGA LA MACHO ILI WATULIE WASIJIUNGE NA MAKUNDI YANAYOWEZA KUWADHURU, LAKINI MABADILIKO HAYO YOTE YAMEKUJA BAADA YA JUMUIYA ZA KIJAMII KUANZA MFURUKUTO WA KUDAI HAKI ZAO, KWANI WALISEMA HAYO MAFUTA SI MTU MMOJA YAKO ARDHINI NA NI ARDHI TULIYOZALIWA WOTE KWA NINI TUSIZITUMIE HIZO DOLLAR WOTE? PALE UKOO WA KIFALME ULIPOKUWA KIZIWI MATOKEO YAKE WALIZALIWA HAWA WA SIASA KALI, NDO KUONA HIVYO UKOO WA KIFLME UKABADILI MSIMAMO WAKE NDO ANGALU NA JAMII YA KAJAMBA NANI WAMEANZA KUFAIDI. MAENDELEO HAYAJI BILA MSUGUANO.
ReplyDeleteHiyo ni petro-dollar huwezi kufananisha na Tanzania.Mimi niliishi huo mji 1980-1986 kweli wamefika mbali ukilinganisha enzi niliyokuwa naishi huko.Tatizo la Tz watu wanaibia sana nchi ukiwa madarakani iba haraka haraka kiasi muda wako haujaisha ama kufukuzwa kazi kweli kuna maendeleo hapo.
ReplyDeleteMdau wa Uswidi
Kwa wenzetu kusafi kichizi, picha kama hii ingekuwa Dar ungeona hata mavi kibao kando kando ya hizo taa! Watanzania sijuwi ni watu wa namna gani.
ReplyDeleteWanaosema tusilinganishe na Saudia kwani wao wana Petro dollari ni kweli na sikweli pia. Si kweli kwa maana ya hivi, manispaa na ianzishe huduma hizo tokana na kodi wanazokusanya toka makampuni na wafanyakazi na wafanyabiashara wakishaweka huduma hizo hapo ndio waanze kuzitoza kiingilio. Kwa idadi ya watu wanaoingia sehemu kama hizi ukitoza choo sh 100 au 200 at the end of the day umekusanya ya kutosha kuhudumia usafi wa eneo. Mimi naamini watanzania tukishaekewa mazingira ya kuridhisha na kutufurahisha katika sehemu hizi tutakuwa radhi kulipia huduma hizi. Nakubali asilimia 100 kuwa hatujafikia hatua ya kupata hizi anasa bure,lakini tukiwekewa huduma bora na kutozwa kihalali mind you kihalali na si kutaka kurudisha mtaji in a month kwa kutoza pesa nyingi basi tutajitutumuwa.
ReplyDeleteUkianza kuleta vitu kama hivyo hapa utapelekwa Bungeni umefuja pesa za umma nawapambe kibao wataponda saaaaana tu
ReplyDeleteSema mzee wa box, wewe hawakunyanyapai huko kwa kina Osama...
ReplyDeleteMdau upo Khobar tuwasiliane kwa number hii 0557839486
ReplyDeleteSwali la kizushi, watu wanaogelea vipi Saudi Arabia?
ReplyDelete