Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo akimkabidhi jana jijini Dar es salaam tuzo ya Shirika la Fedha Duniani(IMF) mfanyakazi wa Shirika hilo tawi la Tanzania Mita Samat kwa kufanya kazi kwa bidii hatimaye kufanikisha mkutano wa IMF ulifanyika hapa nchini mwaka jana.Mtanzania huyo ni mtu wa kwanza kupata tuzo ya shirika hilo.
Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo (kulia) akifafanua jambo jana jijini Dar es salaam kwa waandishi wa habari juu makubaliano waliyofikia kati ya Tanzania na uongozi wa Shirika la Fedha Duniani (IMF). Kushoto ni Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa IMF David Robinson .Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO


Mawaziri kama hawa angalau mtu unaweza kuwafagilia, yaani ni mfano kidogo tu, au kiduchu tu,
ReplyDeleteLakini kama huyu wa Nishati ni bora ajiuzuru maana hii miumeme inayokatika kila mda ni kero sana ukichukulia tumeshailipia na bado wanaleta dharau, mi naona tuungane ili tupate umeme mbadala kama wa Solar na aina nyingine ya nishati mbadala baadala ya maji, na wizara ifutwe na Tanesco ifutwe maana ni kero hawajui wanacho kifanya zaidi ya kusubiri mwisho wa mwezi