Kuna tukio nililiona MAISHANI:
Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woote;
IMAGINE:

ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau!!!

UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!

UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.

UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!

CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!

UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!

UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!

Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!

HIVI INGEKEWA WANAUME
TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?

Kwa leo acheni tu niwape
heshima zao wanawake wote:

I SALUTE AND LOVE THEM WOMEN!
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. we mdau uliyeandika haya una akili sana hv una phd au nimekupenda kweli umeshaoa?kama hujaoa niko ready hata leo uniweke japo kimada najua nitafurahi . nadhani unafaa kuwa mume wangu.nitakutafuta

    ReplyDelete
  2. Ndivyo unavomfanyia mke wako?

    ReplyDelete
  3. Mdau asante kwa kutambua hilo.

    Mwanamke asiye mvumilivu!

    ReplyDelete
  4. wee mdau hapo juu, Wed Mar 17, 09:41:00 AM huna akili mkichwa! Hujui hata kama aliyeandika ni mwanamke au mwanamume, licha ya kwamba kaoa. Huenda ni mtoto ambaye anayaona kila siku mama yake akitendewa.

    ReplyDelete
  5. HAKIKA WANAWAKE MNASTAHILI SHUKURANI NA PONGEZI. MDAU UMENENA SAWASAWA SANA. SIO WAKATI WOTE WANAUME HUWA TUNAKAA NA KUAFAKARI THAMANI NA UMUHIMU WA WAKE ZETU. UMENIPA CHANGAMOTO LEO HII YA KUFANYA KITU KWA AJILI YA KU-APPRECIATE WHO MY WIFE IS AND WHAT SHE DOES AND GOES THROUGH. INASIKITISHA TU KWAMBA LEO HII NDOA NYINGI ZA WADADA WASOMI, WENYE KAZI ZAO NA BIASHARA NA MAPESA KIBAO ZINAVUNJIKA KWA SABABU HAWAKO TAYARI 'KUVUMILIA NA KUSAMEHE' KAMA HUYU MWANAMKE ULIYEMZUNGUMZIA. MUNGU KAWAUMBA WANAWAKE NA MOYO HUO TOFAUTI NA WANAUME. THEY HAVE POWER AND COURAGE TO DO THAT. NAOMBA WAITUMIE FURSA HIYO WALIYONAYO ILI NDOA ZISIMAME. THE MORE THEY DO IT WITH LOVE, THE MORE MWANAUME ATA-REALIZE MAKOSA NA MAPUNGUFU YAKE NA KUBADIIKA. NASI WANAUME TUACHANE NA TABIA ZA ULEVI, UZINZI NA UKATILI KWA WAKE ZETU NA WANAWAKE KWA UJUMLA. A TRUE MAN IS A RESPONSIBLE MAN, SIO KUWA NA WANAWAKE WENGI NA KURUDI NYUMBANI USIKU NA UBABE NDO UNAKUFANYA UWE MWANAUME KWELI, TUBADILIKE!

    ReplyDelete
  6. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  7. Hapo kwenye "WALA HALALAMIKI" inaonyesha huyo Mwanamke ni Mpumbavu.

    ReplyDelete
  8. NIMEICHUKIA SANA HIYO MADA HAPO JUU. MIMI NI MWANAMKE LAKINI SIWEZI KUVUMILIA HUO UJINGA. KWA HAKIKA MWANAMKE ANAEISHI HAYO MAISHA NI MWANAMKE YULE TEGEMEZI, ASIE NA KIPATO CHOCHOTE. KILA WAKATI ANAOGOPA KWA SABABU ATAENDA WAPI? KWAO HUENDA NI MASKINI, KAZI YAKE NI YA KIPATO CHA CHINI. ANAOGOPA AKIONDOKA WATU WATAMSEMA NK. KWA KWELI NI UJINGA USIOKUBALIKA ETI MWANAUME ANAFANYA VITUKO VYOTE HALAFU MWANAMKE ANAKUWA KIPIMO CHA UPENDO KWA KUVUMILIA. NI UJINGA, UPUMBAVU NA MFUMO DUME USIO NA MAANA. KWA KIFUPI UMEPITWA NA WAKATI. NIKISOMA HAYA NINASHIKWA NA HASIRA SANA. WE LIVE ONCE AND WE DIE ONCE, KWA NINI KUMVUMILIA MAISHA MAGUMU HIVYO? IF IT WAS ME HUYO MWANAMKE, I JUST QUITE NA KUENDESHA MAISHA YANGU SEHEMU NYINGINE SIO KUVUMILIA. NI UJINGA SANA.

    ReplyDelete
  9. kwangu mimi naona hizo ni hadithi tu za kufikirika...jamani wanawake wetu wa siku hizi anaweza akavumilia yote hayo??du kama yupo mniambie..mi nimeoa almost 10yrs..nikirudi mtungi wa maana nakuta chakula cha hovyo au hakuna,kununiwa,asubuhi nguo natafuta mwenyewe na kupiga pasi mwenyewe...kununiwa au kugombezwa kutaendelea kwa siku mbili au tatu..then nitamchokoza na 'tutapeana' kwa siku tatu,siku inayofuata narudia mtungi wa maana..mzunguko unaanza upya ..then life goes on....
    Mdau Mbishi ;New-Ala

    ReplyDelete
  10. Huu UPUUZI wa kuvinyenyekea hivi vidume vya mbegu unaanzia kwenye the so called CHICKEN PARTIES.....Eti....mwanangu uwe na adabu mbele ya "baba"....akirudi kazini mtengee maji ya kuoga na uhakikishe apate chakula cha moto....eti...kama karudi late usimdodose sana...mwanangu ndoa ni uvumilivu....usipendelee kukaguakagua simu ya mumeo.....ETI NINI!?.....mtuonage hivihivi na nywele zetu za bandia tukiringa barabarani....WANAUME WENYEWE MKO WAPI?....kazi yenu ni kutuchuna tuu....tena siku hizi wala hamna aibu kwa hilo....JIREKEBISHENI

    ReplyDelete
  11. ni upuuzi mtupu.
    wewe uliyetoa hii mada hujui hila za wanawake.
    kama kuna mwanamke mwenye hizo sifa basi ujue ni mvivu, hana kazi na hataki kujishughulisha.
    ukumkuta mwanamke mwenye kazi au anayejua kujishughulisha na ana uhakika wa kuto kulala njaa utakoma. atakukalia kichwani.

    shauri yako.

    tembea uone, kua uyaone.

    ReplyDelete
  12. haha ahha.....daaahh kweli jamaa ni noumer

    ReplyDelete
  13. Wadau nadhani aliyeandika hayuko serious wala hajafanya utafiti... hawa wanawake wa "Bongo Flava".. hawako hivyo.. wao uvumilivu zero, ila hizo ulizotaja siyo sifa.. otherwise kama unachochea uonevu dhidi ya wanawake..

    Hebu tafuta movie inaitwa "A Diary of the Tired Black Man", ndiyo utajua wanawake wengine wakoje!

    ReplyDelete
  14. nyoo hata kama nikiwa mvivu or sina ajira utakoma na mie atii?? unijie uko njwii kila leo usiku wa manane mara una mademu he he heee utatambaa babaa na maji utayachota na kuyapeleka bafuni mwenyewee kimpango wako na kwangu mahot pot marufuku saa ya kula haupo ukirudi utaamua upashe chakula kwenye jiko la mchina au uwashe mkaa kama vipi tuachane fasta hata punda huwa wanabwaga manyanga haki sawaaaa hata kama mnaleta hela home hata sie tunaleta eboh!!

    ReplyDelete
  15. Mwanangu hayo unawazungumzia mademu wa bush saaaaaana, yaan hapa jijini Dar humpati hata kwa kutumia darubini. Na kama mkeo anakufanyia hivyo ujue tu anakupa timing au ni mbwisi saaana, na nina hakika haujaoa. We unadhani watu wangekuwa wanaruka ukuta kuingia majumbani mwao wanavyotoka kwenye mitungi usiku wa manane ?

    ReplyDelete
  16. LOH NI DHAMBI KUBWA KUMFANYIA MWANAMME HAYO BAADA YA MAUZAUZA YAKE HUKO NJE! YAANI WEWE MWANAMKE WA HIVYO HATA MUNGU ATAKUCHOMA MOTO.., MAANA HATAKI JITU BWEGE NAMNA HIYO.

    ReplyDelete
  17. wewe unaongelea wanawake wa wapi!!??!!Afrika,Asia,America au Europe???!!

    ReplyDelete
  18. Comment ni tamu kuliko hata maada yenyewe........

    ReplyDelete
  19. dunia ya leo mwanamke mjnga hivyo yupo?

    ReplyDelete
  20. mwanamke unaekubali kufanya hayo WEWE NI MPUMBAVU SANA na hustahili kuishi kabisa

    ReplyDelete
  21. wewe mwanamme acha kusifia upumbavu. eti ndoa, what ndoa? is there any ndoa there? yaani muache kuleta za kuleta. unarudi usiku umelewa kesho yake utakoma nakuambia hurudii tena na hakuna cha kuondoka, utaondoka ewe, shenzi kabisa.

    ReplyDelete
  22. maisha ni kuheshimiana sio eti kumnyenyekea mwanaume, hanyenyekewi mtu, kila mtu anahitaji heshima, wewe mwanamke TAFUTA PESA ACHANA NA KUTEGEMEA PESA ZA MUMEO NA KUISHIA KUFANYIWA USHENZI, UNYAMA WA KILA AINA HALAFU UNAISHIA ETI KUSIFIWA UJINGA TU, SIFA GANI HAPO? SUBIRI KIFO AU UKIMWI NDIO UJUE ULIKUWA MKE MWEMA. NO MORE SUCH LIFE. AKIRUDI USIKU FULL KUMBONDA HADI POMBE ZIISHE. HEBU JARIBU KWANGU UONE.

    ReplyDelete
  23. kweli kila mtu ana uhuru wa kuongea na kusema atakavyo ila tunatakiwa kukumbuka jambo moja kila mwanadamu ni mpekee so sijashangaa kuona wengime mnamsema huyo aliye toa mada.ukweli utabaki palepale kwamba jiwe haliwezi kushindana na nazi hata siku moja, mwanamke ni mtu muhimu na hakuna asiye tambua hilo bali mnajifariji tu na maneno yanu, mwanamke aliye kwenye ndoa anapaswa kuwa mtii,kusamehe na kumuonyesha mume wake upendo wa dhati. Mwanaume cku zote ataiga kutoka kwa mkewe mama akiwa kiburi baba atavumilia lakini ipi siku naye ataota mapembe, ila mama ukiwa mstarabu lazima tu baba ipo siku nae huruma itamwingia akuwa kama wewe, kamwe tusijidangamye kutaka kuwa sawa na wanaume cc ndio wajenzi wa familia,washauri na wamuhimu so tujitaidi kuwa bora ili ndoa zidumu.
    najua mpo mtakao nipinga kuonyesha umwamba wenu ila ukweli utabaki palepale,. MUNGU TUBARIKI WANAWEKE WOTE WA KITANZANIA TUWE NA HEKIMA, UTII NA UPENDO TUSIWE WASHINDANI WA MAMBO.

    ReplyDelete
  24. STRENGTH OF THE WOMAN-SHAGGY

    ReplyDelete
  25. SIKUBALI,.HATA KIDOGO NASEMA HIVIIII!!!!!!!!!!!!
    MIMI NI MWANAMKE NIMEKATAAA KATUKATU HUO USHENZI, ETI MTU AMESHINDIKANA NA FAMILIA YAKE AU KAZOEA KUONA WAZAZI WANAPIGANA NA HASWA MAMA ANAPIGWA KAMA KIBAKA ETI NI MAMA MWEMA ANAVUMILIA.

    KATUKATU NIMEKATAA ACHA JAMII ISEME ILA NAANGALI UHAI ALIONIPA MUNGU. HATA KWENYE BIBILIA KULIKUWA NA SINGEL PARENT AMBAO WATOTO WAO NI WATAKATIFU. NITATUNZA WATOTO KWA MAADHILI MEMA NA MUNGU ATAWAFANIKISHA.

    NAJUA MUME WANGU ATASOMA HUKU NAMPA MSG SIVUMILII KATU. NA WALA SIRUDI.

    SIVUMILIII

    ReplyDelete
  26. Upole siyo udhaifu,kwa hiyo wanaume tusiwaone wanawake kuwa ni viumbe visivyostahili heshima na staha kamili.Kuoa siyo dili bali dili ni kudumisha ndoa yako ikiwa imejaa raha na furaha.

    N=NYUMBANI
    D=DAIMA
    O=OMBENI
    A=AMANI

    ReplyDelete
  27. SOMA MITHALI (PROVERBS) 31 SURA YOTE UPATE MAELEKEZO YA MUNGU KWA MWANAUME (ACHA WANAWAKE,ULEVI, MPENDE MKEO) NA SIFA ZA MWANAMKE BORA KATIKA NDOA. KAZI, PESA, VYEO NA MIFUMO DUME ISITUDANGANYE, MWISHO WAKE HAPA DUNIANI.

    ReplyDelete
  28. INATISHA SANA KUONA JINSI MADA ILIVOBADILIKA GHAFLA NA HAO WANAOJIFANYA WANAWAKE WAKISASA WANAOTAKA USAWA.ALIEANDIKA ALIANDIKA KWA NIA NZURI TU KUONYESHA JINSI WANAWAKE WALIVO NA HURUMA KWAHIO NYIE MNAKATAA KWAMBA HAMNA UPENDO SIO.HALAFU TILL THE END OF MANKIND HAITAKUJA KUTOKEA HATA SIKU MOJA KWAMBA TUKAWA SAWA HATA SIKU MOJA YAKIHARIBIKA LEO HII WE MWANAMKE NA WATOTO WA TANO UKIACHWA KWENYE NDOA HATA KAMA UNA HELA KIASI GANI UTAISHI MAISHI YA AJABU TU NA KUWA SUGAMOMY WAKATI MWANAUME NDO KWANZA KIURAHISI ANAWEZA AKAOA TENA NA NDOA YA HESHIME TU.
    Badilikeni nyie wanawake wa kizazi kipya sio ujanja sa si kama tuna nyumba ndogo na nyie mnataka nyumba ndogo?????? mfano kama mwanaume saivi ametembea na wanawake watano halafu haogi si uchafu sasa fananisha na mwanamke alietoka kutembea na wanaume watano halafu akaacha nanihiiiii ndanii kinyaaaaaaaaaaaa mmmmmmm

    ReplyDelete
  29. Mdau Kimbuma Kingani, be blessed for your thoughtful comment. May God Bless You.

    ReplyDelete
  30. wewe mtoa maoni wa kwanza napenda kukujulisha kuwa nipo tayari kuwa na wewe. nitumie email yako pamoja na namba ya simu.

    nitakutunza sana tu. karibu

    ReplyDelete
  31. my people i love you, nawasalute madada na makaka wote wenye akili mliyemzodoa huyu mtoa mada, na pia nasema kama kuna mwanamme yeyote katika dunia hii ya sasa anampenda mwanamke mwenye sifa hizo za kijinga na za kimasikini basi huyo mwanamme atakuwa ana matatizo ya akili.

    ReplyDelete
  32. wallahi uwe mume uwe mke uwe mtoto uwe mkubwa ulosema yote yaukweli.wagenga walisema mvumilivu ula mbivu kwa wanawake hawa wenye shida kama hii inayo wakuba basi afaa apewe pongezi kubwa tena sana ukimpenda mumeo unastahamili lakini kama ningekuwa mie lolo zamani nishamtimuwa hanitesi mwana wamwenzie.mdau toronto

    ReplyDelete
  33. NYIE MADAU, IKO RAFIKI YAGU MOJA NAITWA SOMJI KUMAR, YEYE NAOA BHOKE NA KM SOMJI NARUDI JUMBANI LEWA SANA, NAACHIA NGAMA TANDANI ALAFU NAITA MKE YAKE BHOKE NAAMBIA: DARLING JOO NA POTI YA TOTO NA BABY-WIPE KUJA ZOA MIMI HAPA TANDANI MAANA MIMI KWISHAMALIZA PAKUA NGAMA, SASA NAJUWA MIMI HAWEZI SHUKA TANDANI KWENDA CHOO SABABU NACHOKA SANA MIMI, HAKUNA GUVU, SASA MIMI NANUNUA POTI MINGI SANA HAPA JUMBANI YETU YA TOTO YETU YOTE: KIMJI, NARENDRA, BHIMJI a.k.a MWITA, ANJARI a.k.a GHATI. DAD NA MOM YA BHOKE SIKU MOJA NAPATA HABARI TOKA JIRANI YA BHOKE KUSEMA KM BHOKE IKOTESEKA SANA NA SOMJI, PARENTS YA BHOKE ANA-ADVISE BHOKE TO SEEK DIVOCE LKN BHOKE YEYE NAKATAA NASEMA ATI NARIDHIKA NA YOTE KUMAR NATENDEA, ATI HIYO DIYO TRUE LOVE AND THAT DOES NOT CARE ABOUT ANYTHING WRONG, LOVE THAT TOLERATES BEYOND LIMIT/EXPECTATION. WAO NAISHI HUKO MWANZA MWAKA YA KUMI NA BILI SASA HAPANA TATIZO YOYOTE. NAJUA SOMJI YEYE HAPANA ONA SHIDA SABABU YEYE KULE INDIA NATOKA STATE MOJA ABAYO NAPATA INDEPENDENCE TOKA BRITISH AHEAD OF OTHER STATES YA INDIA.WAO NATUMIA BINU HII YA SOMJI YANI WAO ALITAPANYA NGAMA KWA STREETS YA COLONIAL MASTERS EVERY MORNING, COLONIALISTS NAZOA NGAMA KWA STREETS KILA SIKU PAKA NACHOKA,STREETS NANUKA SANA PAKA NAAMUA KUABIA QUEEN TO GRANT INDEPENDENCE TO THE FATEFUL STATE. SASA HAPANA SHAMBULIA SANA HIYO DAU NATOA MADA HAPO JUU MAANA NYIE HAWEZIJUWA WAO NAPATANA VIPI/NA-DEFINE VIPI DOA YAO? [HAWEZIJUWA NINI NAUNGURUMA KWA KIFUA YA PAKA]
    MIMI DAU YA MADRAS INDIA.

    ReplyDelete
  34. NYIE MADAU, IKO RAFIKI YAGU MOJA NAITWA SOMJI KUMAR, YEYE NAOA BHOKE NA KM SOMJI NARUDI JUMBANI LEWA SANA, NAACHIA NGAMA TANDANI ALAFU NAITA MKE YAKE BHOKE NAAMBIA: DARLING JOO NA POTI YA TOTO NA BABY-WIPE KUJA ZOA MIMI HAPA TANDANI MAANA MIMI KWISHAMALIZA PAKUA NGAMA, SASA NAJUWA MIMI HAWEZI SHUKA TANDANI KWENDA CHOO SABABU NACHOKA SANA MIMI, HAKUNA GUVU, SASA MIMI NANUNUA POTI MINGI SANA HAPA JUMBANI YETU YA TOTO YETU YOTE: KIMJI, NARENDRA, BHIMJI a.k.a MWITA, ANJARI a.k.a GHATI. DAD NA MOM YA BHOKE SIKU MOJA NAPATA HABARI TOKA JIRANI YA BHOKE KUSEMA KM BHOKE IKOTESEKA SANA NA SOMJI, PARENTS YA BHOKE ANA-ADVISE BHOKE TO SEEK DIVOCE LKN BHOKE YEYE NAKATAA NASEMA ATI NARIDHIKA NA YOTE KUMAR NATENDEA, ATI HIYO DIYO TRUE LOVE AND THAT DOES NOT CARE ABOUT ANYTHING WRONG, LOVE THAT TOLERATES BEYOND LIMIT/EXPECTATION. WAO NAISHI HUKO MWANZA MWAKA YA KUMI NA BILI SASA HAPANA TATIZO YOYOTE. NAJUA SOMJI YEYE HAPANA ONA SHIDA SABABU YEYE KULE INDIA NATOKA STATE MOJA ABAYO NAPATA INDEPENDENCE TOKA BRITISH AHEAD OF OTHER STATES YA INDIA.WAO NATUMIA BINU HII YA SOMJI YANI WAO ALITAPANYA NGAMA KWA STREETS YA COLONIAL MASTERS EVERY MORNING, COLONIALISTS NAZOA NGAMA KWA STREETS KILA SIKU PAKA NACHOKA,STREETS NANUKA SANA PAKA NAAMUA KUABIA QUEEN TO GRANT INDEPENDENCE TO THE FATEFUL STATE. SASA HAPANA SHAMBULIA SANA HIYO DAU NATOA MADA HAPO JUU MAANA NYIE HAWEZIJUWA WAO NAPATANA VIPI/NA-DEFINE VIPI DOA YAO? [HAWEZIJUWA NINI NAUNGURUMA KWA KIFUA YA PAKA]
    MIMI DAU YA MADRAS INDIA.

    ReplyDelete
  35. Mdau aliyoyasema hayo, yapo sana...lakini sio sifa zote hizo kwa mwanamke mmoja wa sasahivi.Na mwanaume anayetenda hayo yote, na akatendewa na mwanamke yote na akaona sawa, hiyo sio mwanaume kabisa duniani mpaka akhera,bali huyo ni shetani! Na mwanamke anayekubali yote hayo kwa kulinda ndoa, anamapungufu,ambayo anayajua Mola wake. Ila wanaume wengiwao hawana huruma na imani kwa wake zao ..."IF THEY ARE ABLE TO SEND A MAN TO THE MOON, THEY SHOULD BE ABLE TO SEND THEM ALL".

    ReplyDelete
  36. Wewe Mdau uliyeandika hayo, hukusifu wanawake MNAFIKI MKUBWA WEE!BALI UMEKASHIFU NA KUWATUKANA KIAINA. Maana hayo mambo yote ukiyasoma, ni mambo yanayochoma moyo na kuumiza ilifaa kuwaonya wanaume watendao mambo hayo yote kama ulivyoyataja(halafu kumbe mnajuaga mnavyofanyaa eeeh??!!!!)na kufikiria adhabu kali,ili kuwatia akili na kuleta akili nzuri yenye maendeleo na ubora katika jamii! Maana hizo sio sifa bali LAANA TUPU KWA MTENDAJI!

    ReplyDelete
  37. Mtenda yoote hayo, hafai kabisa kuwa duniani bali MWITUNI!

    ReplyDelete
  38. Ewe mama unayefanyiwa yote hayo, unauvimulivu mfano wa NABII!

    ReplyDelete
  39. Ewe baba mjaa wa laana unayetenda yote hayo, usijione bora,...umelaaniwa duniani mpaka akhera!

    ReplyDelete
  40. mke bwege!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...