Afisa habari wa Simba Cliford Ndimbo akizungumzia safari hiyo
Mabingwa wapya wa soka Tanzania Bara, Simba SC, inatarajia kuondoka alfajiri hii kwa shirika la ndege la Kenya Airways kuelekea nchini Zimbabwe ambako inatarajia kuwa na pambano kati yake na timu ya Legthens ya Zimbabwe katika mashindano ya Kombe la shirikisho katika mchezo utakaochezwa ijumaa jijini Harare.

Afisa habari wa Simba, Bw. Cliford Ndimbo amesema msafara huo utakuwa na watu 25 ambapo kiongozi wa msafara atakuwa mwenyekiti wa timu hiyo Hassan Dalali.
Amewataja wachezaji watakaoondoka kuwa ni Juma Kaseja, Haruna Shamte,Juma Jabu, Nico Nyagawa, Kelvin Yondan, Mohamed Banka, Hilary Eches,Ramadhan Chombo, Mussa Hassan Mgosi, mike Barasa, Ulimboka Mwakingwe, Ally Mustafa, Salum Kanoni, David Naftali, Uhuru Selemani, Jerry Santo, mohamed Kijuso, Jabir Aziz na Joseph Owino.
Katika safari hiyo pia ktakuwa na kocha mkuu wa timu hiyo mzambia Patrick Phiri, kocha msaidizi Amri Said, Daktari wa timu a Joseph Kapinga na meneja wa timu Innocent Njovu. Katika msafara huo pia atakuwepo mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Kassim Dewji na Mulamu Ghambi kutoka marafiki wa Simba (Friends of Simba).
Timu hiyo inatarajia kurejea mara baada ya mchezo huo ijumaa au jumapili kutegemea nafasi watakayopata kwenye ndege.
Simba funga hao watoto wa mzee wa mashamba, mrudi nyumbani na pointi tatu muhimu. Washibiki na wakeleketwa wa SIMBA 2nakutakmieni kila la kheri.
ReplyDeleteKigogo Boy
Wapi air Tanzania?
ReplyDelete