Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akilakiwa na Senator wa Bunge la Senate la nchi ambaye pia ni makamu wa raisi wa kamati ya mambo ya nje Mhe. Priyanandana Rangist mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Bangkok, nchini Thailand Jana. Spika yupo nchini Thailand kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mabunge Dunia (Inter- Parliamentary Union) unaonza leo na kumalizika tareh 1 April 2010 ambapo yeye ni mjumbe wa kamati tendaji ya IPU, inategemewa zaidi ya nchi 150 wanatarajia kushiriki Mkutano huo. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge.
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akipokewa kwa kuvishwa ua mkononi kama ishara ya ukarimu wa watu waThailand mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Bangkok, jana. Spika yupo nchini Thailand kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mabunge Dunia (Inter- Parliamentary Union – IPU ) unaonza leo na kumalizika tareh 1 April 2010 ambapo yeye ni mjumbe wa kamati tendaji ya IPU, inategemewa zaidi ya nchi 150 wanatarajia kushiriki Mkutano huo.
Mjumbe wa Tanzania katika Mkutano wa wabunge wanawake wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Suzani Lyimo, kulia akichangia mada kuhusu tatizo la usafirishaji haramu wa Binadamu katika mkutano wa 122 wa IPU unaofanyika Mjini Bangkok, Thailand. Kulia ni Mjumbe mwingine ambaye pia ni Mbunge wa Tanzania Mhe. Dr. Haji Mwita Haji. Mkutano wa IPU umeanza rasmi leo na unatarajia kumalizika April 1, 2010.
Wasanii wa ngoma ya utamaduni ya Thailand wakitumbuiza wakati wa ujio wa Spika Mh. Samwel Sitta jijini Bangkok




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Na hiyo mifuko ya rambo ya nini?

    ReplyDelete
  2. Mhe Spika 6, hiyo suti yako nzuri sana - suti ya kitanzania inapendeza na pia kudhihirisha kuwa tunaweza kujibainisha kama waTZ/WaBongo na tukafanya mambo kama ya 'wenzetu' badala ya kung'ang'ania suti ya 'wenzetu' lakini tukafanya madudu tunayoshuhudia kila kuchapo!

    mtaalamu wa social/political skin

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...