Tarehe 25/03/2010 ni siku inayoingia katika historia ya Chama cha Mapinduzi nchini Italy,baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa kwanza wa kuchagua viongozi wa tawi la CCM Napoli.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wakereketwa wanachama hai wa CCM ughaibuni ,ulimalizika kwa furaha na mafanikio makubwa. Katika uchaguzi wa viongozi wa tawi hilo, ndugu ABDULRAHAMAN A.ALLI alichaguliwa kuwa Mwenyekiti,Wana CCM pia walimchagua ndugu KAGUTTA N.MAULIDI kushika nafasi ya katibu wa tawi. Nafasi ya katibu siasa ilichukuwa na ndugu ALLAN BENDERA na mama FATUMA A.TANDIKA alichaguliwa kuwa katibu uchumi.
Pia katika uchaguzi huo Bi JUDITH JOSEPH, Bi ZENA HASSAN ,ndugu AWADH SALIM na Mzee HAMISI MNYAMANI walichagualiwa kuwa Wajumbe wa CCM tawi la Napoli.
aaagh! haha! haha! ha! ha! ha!...
ReplyDeletenikiiangalia hii ngozi yangu nyeusi nawaza sipati jibu na mwishoni naishia kucheka. wakati mwingine nawaza na ninadhani hata ubongo wa mtu mweusi ni mweusi ndio maana watz mbele hatuoni "NURU" giza limetanda; mara utasikia Uingereza mara U.S.A mara ... sasa Italy ni matawi tu ya CCM yanazidi kufunguliwa. wenzetu kama hao waingereza, wamarekani na hao wataliano wakija kwetu wanakuja kufungua viwanda, makampuni au utasikia wamewekeza kwenye madini sisi tukienda kwao tunawekeza kwenye siasa na kufungua matawi mapya kisha TUNAJIHAKIKI tunajipa MAKSI za kutosha na mwisho TUNAJIPONGEZA kama unavyowaona hao wanaCCM wa italia...
duh! Hii ni laana!
Mdau kutoka TARIME (a.k.a UKANDA WA GAZA)
Ujinga bado unaendelea.
ReplyDeletekumbe ccm hata kama sio mtanzania unaweza kuwa ccm? kweli hichi chama safi sana akina ubaguzi
ReplyDeletewabongo bwana!! mpo nchi za watu mnafungua matawi ya chama cha siasa ikiwa pale bongo kuna sehemu nyingi hayajafunguliwa matawi kulikoni? wacheni siasa fateni mlichokifata naona haina faida ni ufisadi mtupu
ReplyDeleteHAYA MAMBO YA KUENDESHA SIASA ZA CCM KATIKA NCHI ZA NJE YANA MAANA NA MANUFAA GANI KWA WATANZANIA WENZETU WALIO KULE NYUMBANI?
ReplyDeleteNASHINDWA KUELEWA WATU WANAOISHI NJE YA NCHI NA KUINGIA KWENYE MAMBO YA SIASA ZA CCM. SIJUI WANA MALENGO GANI.
ReplyDeleteKAMA MNATAKA KUFANYA SIASA ZA CCM SI MRUDI TANZANIA JAMANI. WENGI WENU HAMTAKI KURUDI KWA SABABU YA SHIDA ZA KULE TANZANIA, ULAYA KUNA MAISHA MAZURI NA MAMBO YANAFANYIKA KWA MSTIRI ZAIDI YA TANZANIA.
HIVI HAWA WATU WANASHINDWA KULINGANISHA MAENDELEO YA NCHI WANAZOISHI NA YA TANZANIA? WANASHINDWA KUELEWA KWANI NINI TANZANIA BADO HAIJAENDELEA WAKATI INA RESOURCES NYINGI TU?
TATIZO NI HIYO CCM MNAYOIPIGIA DEBE.
FIKIRIA VIZURI CHANZO CHA UMASIKINI WA TANZANIA YENU
mmmmmm sasa ccm mmezidi mpaka wataliano wanatumiwa kuongoza chama? inatisha
ReplyDeletehii poa sana hongereni.
ReplyDeleteCCM mna mpango wa kuanzisha vita nini? Matawi ya nje ya nchi huanzishwa na vyama vya wapigania uhuru tu. Ama hii ni milango ya kuingizia fedha za ufisadi? Tumewashtukia CCM Mshindwe na mlegee
ReplyDeleteITAFIKA KIPINDI haya MATAWI yatapanuka na KUTAKA yatoe na WABUNGE KABISA...MBUNGE WA CCM JIMBO LA UINGEREZA, ITALY, MAREKANI, etc..teh..teh..teh..
ReplyDeleteWizi mtupu hawa CCM wamekosa kazi za kufanya hadi wafungue matawi huko? Jamani tafuteni rizki ccm Wanachofanya ni kuchukua chao mapema sasa nyie mnachotakiwa mtafute maisha mje muwekeze huku mlikowacha familia zenu.
ReplyDeleteHebu wacheni hizi propaganda jamani fanyeni yanayo wahuuuuuuuuu ccm waachieni mafisadi.
CCM NOMA WANALOGA HADI UGAIBUNI
TUMECHOKA
bY MKEREKETWA - kISUTU
Mtoa Maoni wa kwanza nakupongeza kwa kuwa na akili inayotufaa. ni kweli kabisa watanzania hawa wanamatatizo fulani. Nilishawahi kumwomba kaka Michuzi awe na mwanasaikolojia kuwapatia wananchi hawa ushauri nasaha yeye naona hajalifanyia kazi suala hili. watu wanakwenda nchi za watu kutafuta maisha...pesa, elimu, teknolojia, maarifa ufundi nk kwa ajili ya maendeleo yao, ya familia zao na nchi kwa ujumla wao wanakimbilia siasa. Siasa haiona nafasi sasa Tanzania. Kweli wenzetu wanakuja Tanzania kufungua viwanda, makampuni nk. wanachota pesa wanapeleka kwao...sisis waaaa bize na politix....seriously kuna matatizo makubwa sana nchini.
ReplyDeleteSerikali iko katika big shake now...vitu kibao vimekwama, na nobody see it....oooh masikini Tanzania.
Upuuzi 1 : Maendeleo 0
ReplyDeleteKwa huzuni, sistushwi na upuuzi huu, ujinga tunao katika damu yetu.
HIVI JAMANI SIASA ZA NINI HUKU ULAYA? TENA ZA CCM? CCM INA MATAWI NA WANACHAMA KIBAO TANZANIA. NYIE WATU WA HUKU ULAYA FIKIRINI MAMBO MENGINE YA KULETA MAENDELEO YA WALE MLIWACHA KULE TANZANIA MAANA WANATESEKA SANA.
ReplyDeleteTANZANIA YA LEO BAADA YA MIAKA MINGI YA UHURU BADO HAKUNA UMEME, BARABARA, MAJI, DAWA HOSPITALI, MADAWATI SHULENI, WAFANYAKAZI HALI ZAO MBAYA SANA, CHAKULA CHA SHIDA SANA, WAKULIMA WANAJITAHIDI KULIMA LAKINI HAKUNA MASOKO YA MAZAO YAO NA YANAISHIA KUWAOZEA TU. KWA UJUMLA WATANZANIA WENGI WAMEPIGIKA SANA. WANAISHI TU ILIMRADI, MAISHA YA WATANZANIA WENGI NI YAKUBANGAIZA SANA TU.
NINYI MLIOPATA BAHATI YA KUTEMBELEA NA KUISHI KWENYE NCHI ZENYE MAENDELEO KWA NINI MSIFIKIRIE KUWAKOMBOA WATANZANIA WENZENU KATIKA UMASKINI?
SIKU MOJA NILIKUWA SUPERMARKET MOJA HAPA ULAYA NA RAFIKI YANGU, TUKAPITA SEHEMU WANAKOPANGA CHEESE (JIBINI) NA MAZIWA. HIZI BIDHAA ZINATOKANA NA MAZIWA YA NG'OMBE. BASI ZILIVYOKUWA NYINGI NA ZA AINA MBALI MBALI NILIFIKIRIA SANA NCHI YANGU YA TANZANIA, NCHI YENYE NG'OMBE WENGI NA MAZIWA MENGI SANA. NIKASEMA TANZANIA KULE WANAKUNYWA TU MAZIWA YA MGANDO NA FRESH BASI. KWANZA KUNA WATU WENGI TU HAWAJAHI KUONA ACHILIA MBALI KUNYWA MAZIWA KWA MUDA MREFU.
SASA SWALI LIKAJA KWANINI WATANZANIA WASIFANYE MBINU ZA KUTUMIA MAZIWA KUTENGENEZA HIZO CHEESE NA PAKETI ZA MAZIWA YA AINA MBALI MBALI KWA WENGI? JE HIVI KWELI VIONGOZI WETU WA KISIASA WANAOKUJA ULAYA KILA SIKU TENA LEO WENGINE WAKO LONDON HAWAJAONA HILO?
YULE RAKIFI YANGU KASEMA TATIZO NI VIONGOZI WETU WANASHINDWA KUWEKA MAZINGIRA NA KUWASAIDIA WANANCHI KUJENGA UWEZO.
VIONGOZI WETU NI AKINA NANI BASI? NI HAWA WALIOTAWALA NCHI MIAKA 50 NA BADO HAWAJAONA HILI.
BASI NILIONA HII PICHA YA KUFUNGUA TAWI LA CCM ULAYA NIKAAMUA KUSEMA HAYA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA. KIZAZI HIKI KITAPITA, ILA NAAMINI VIZAZI VIJAVYO VITEJENGA NCHI. IKO SIKU TU.
don't know what is wrong with these people. Naanza kuamini ni agenda ya chama chenyewe kuwa na foreign branches na kutumia pesa zake kufanya hivyo, sina uhakika ni kwa maslahi gani. Mtu mweusi ndio maana kamwe hatutaendelea maanake badala ya kufikiria maendeleo yetu na jamii zetu hata pale tunapokuwa na uwezo na uelewa kidogo huwa tunaishia kushabikia vitu kama hivi. Ulisikia lini mgeni akaja kama Bongo halafu akafungua matawi ya vyama vya nchi zao? Walipokuwa wapigania uhuru Yes. Shame on Us!
ReplyDeleteBado sijasikia tawi la CCM hapa US!! Kuna mambo mengi ya kufanya ambayo yatailetea nchi yetu maendeleo au angalau kusaidia wananchi maskini huko nyumbani. Hii mikutano na vikao vya CCM vinapoandaliwa ni hela inatumika na hata watu wanapokwenda kwenye hivyo vikao ni nauli(hela) zinatumika. Sasa kwa nini angalau wasichange hizo hela na kutuma nyumbani kwenye matatizo mengi kama watoto yatima, unyanyasaji wa maalbino, na sehemu ambazo ziko nyuma kimaendeleo hasa vijijini!! Itasaidia sana kwa watu wetu huko nyumbani na vile vile kwa watanzania tulioko nje tunaotaka kujijengea mazingira mazuri ya uongozi wa baadaye huko nyumbani. Kwa maoni yangu kushiriki kwenye matawi ya CCM nje ya nchi ni kujipotezea muda na hela kwa sababu bado nikirudi nyumbani na kutaka kuwa kiongozi itabidi nianze upya ku-kampeni kwa wananchi ambao walikuwa hawanifahamu. Kama ni kuanza kampeni nikiwa nje ya nchi inabidi nitumie muda wangu sasa na nianze kuyatatua matatizo ya nyumbani. Vikundi vya kusaidia nyumbani vikianzishwa nitajiunga haraka sana au labda hilo tawi la CCM liwe na malengo ya kusaidia nyumbani hapo ndio nitajiunga.
ReplyDeleteMdau!!!
Ni vizuri tuangalie historia, baadhi ya watu hapo juu, kipindi wanaondoka TZ hawakuwa wanachama wa CCM, sasa ni kwa nini wawe na mapenzi 'mazito' ya chama hicho baada ya kwenda nje? Nafikiri kuna kitu wanatafuta.
ReplyDeletePili, nafikiri kwa mlio nje mnajua nini kimewapeleka huko: kazi, masomo, kuoa, kuolewa, na mengineyo. Wosia wangu ni kuwa siasa is time consuming. Anyway, kila mtu ana malengo yake.
Tatu, mbona siwaoni wazee wakijiunga na CCM huko ughaibuni, au hakuna wazee huko?
Mdau, Bongo
Jamani naona sasa jumuiya za Watanzania Nje zinaanzishwa kwaajiri ya kufanikisha malengo ya CCM na kuliana hela tu! Hivi WANAWANE hao hapo juu si ndio wanaojiita viongozi wa Watanzania Italia au macho yangu yamekosea...sasa inakuwaje wanajipanga pia kuwa viongozi wa CCM?hivi huko Italy hakuna watanzania wengine? Ufisadi upo mpaka huko Italy jamani!!Kwa mwendo huu hatufiki!!Janja janja nyingi sana!!
ReplyDeleteNASHANGAA SANA KUONA SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI INAHANGAIKA KUFUNGUA MATAWI YA CHAMA CHA SIASA NJE YA NCHI BADALA YA KUFUNGUA MLANGO WA DUA CITIZENSHIP ILI HAO WALIOPO NJE WAWEKEZE HUKO NYUMBANI. HIZO NI SERA BUTU SANA ZISIZO NA MAKALI YO YOTE YA KULETA MAPUNDUZI YA MAENDELEO.
ReplyDeleteSERIKALI INASHABIKIA NA KUHANGAIKIA KUKARIBISHA WAWEKEZAJI WAKIGENI AMBAO KWA UPANDE MWINGINE WANAINGIA KUCHOTA MAPESA NA KUYAPELEKA KWAO TUNAFURAHIA HILO KWANI PIA WANACHANGIA UCHUMI WA NCHI. INATAKIWA KWA MWONDO HUO HUO RUHUSU DUAL CITIZENSHIP ILI WAZAWA NAO WANACHOCHOTA TOKA NCHI NYINGIE WAWEKEZE NYUMBANI ILI KUKUZA UCHUMI. NDO MWINGILIANO ULIVYO ULIMWENGUNI. TUNABAKI NYUMA KATIKA MENGI TUNAPOKUBALI FUNGUA MILANGO TUMECHELEWE WENZETU WAMESHATUACHA WAKO MBALI.
TUJIFUNZE WENZETU WEST AFRIKA, PHILLIPINE, INDIA NK WALIVYONUFAIKA NA DUAL CITIZENSHIP.
KUFUNGUA MATAWI YA CCM NJE YA NCHI NI UPUNGUFU WA UELEWA, TUNA MATAIFA YA KIGENI MAGNAPI HUKO TANZANIA NA NANI WAONA ANAENDESHA SIASA ZA VYAMA VYA SIASA? TUNA MACHO HATUONI, TUNA MASIKIO HATUSIKII JE TUTAFIKA KWA MTINDO HUU?
Kwi kwii kwiiiiiiii!!!!!! wewe anonymous wa frdy,26. 11.21am mbona unabana hao viongozi hapo wote si wa tanganyika pana mtaliano ,mnyarwanda,mwarabu lkini ccm tambarare ukiweza kulisha unapewa kura, mungu bariki danganyika.
ReplyDeletemdau CHANIKA
TUNAJUA KUWA WATANZANIA MLIOKO NJE YA NCHI NI WATOTO WA VIGOGO WA CCM NDIO MAANA KILA SIKU MNAFUNGUA MATAWI YA CCM MMETUACHIA BONGO VUMBI TUPU
ReplyDeleteANONY WA KWANZA I SALUTE YOU FOR HAVING A COMMENT THAT TELLS EVERYTHING.NI LAANA UKIWA MWEUSI,SERIOUSLY,NIMEKAA USA FOR 5 YRS AND I CAN TELL THERES SOMETHING WRONG WITH BEING BLACK.KUNA HAWA NDUGU ZETU WEUSI AMBAO WAMEKUWA HAPA FOR CENTURIES BUT OVER 50% MAISHA YAO YANASIKITISHA NI AIBU,NDUGU ZANGU MSIANGALIE BLACK AMERICANS AS YOU GUYS CALL THEM KWENYE MA-TV MKASEMA LA! WATU WEUSI USA NI BAB KUBWA MY DEAR INASIKITISHA,NI MANENO TU MENGI MDOMONI,NO CLASS AT ALL.HIVYO BASI HATA SISI TUNAOKUJA KWENYE NCHI ZILIZOENDELEA TUNASHINDWA KUJIFUNZA KWA HAWA WENZETU?NI KWELI NINYI MNA MDA HUKU UGHAIBUNI WAKUFANYA HIZO SIASA ZA CCM OR WHATEVER PARTY IT MIGHT BE?JE HIZI SIO BLA BLA ZA KUFANYA VITU AMBAVYO KAMWE WILL NOT HELP TZ AS A NATION? MDAU KASEMA KWAMBA SISI TUWEKEZA KWENYE POLITICS WHILE OTHERS INVESTS ON ECONOMICAL OUTGAINS.LAKINI SISHANGAI KWANI SIASA TZ NDO INALIPA BWANA THERE NDIKO MAFISADI WALIPO SOOO HAWA JAMAA WANATAKA NAO KUFIKA PAWALA PALE WAKIRUDI TZ.WANAJIANDAA KUFISADI NCHI YETU,PERIOD!
ReplyDeleteTunaishi katika ulimwengu-kijiji. Katika ulimwengu huu wa sasa umbali wa kijiografia hauwazuii watu kushirikiana katika masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi na wenzao popote walipo duniani. Mapinduzi katika teknolojia ya habari na mawasiliano, usafiri na usafirishaji yamewawezesha walimwengu kufika kila pembe ya ulimwengu wanayotaka na kufanya kile wanachokiona ni cha manufaa kwao. Ni kutokana na dhana hii ya utandawazi CCM ikaona ni vema ianzishe mashina na matawi nje ya nchi ili kuwafikia wanachama wake kwa urahisi. Mashina na matawi haya ya nje ambayo yameanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya CCM ibara 22.1(ii) na 31.1 (d) yamefunguliwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi husika za Tanzania na Uingereza. Hivyo basi ni mashina na matawi halali.
ReplyDeleteKuanzishwa kwa matawi ya nje kumepanda mbegu bora ya ukereketwa na kuhuisha uanachama wa wana-CCM walioko nje ya nchi. Lakini juu ya hayo matawi haya yanawawezesha watanzania waishio ughaibuni wanaotaka kuwa wanachama kupata kadi kwa urahisi kwani kabla ya utaratibu huu wa kufungua matawi nje ya nchi kila aliyetaka kuwa kujiunga na CCM ilimlazimu kurudi Tanzania ili kupata kadi. Matawi ya nje pamoja na mashina yake yanaanzishwa na wanachama kwa hiari bila kusukumwa na mtu au chombo chochote cha chama au serikali.
Uimara wa chama chochote cha kisiasa duniani kote siku zote uko mikononi mwa wanachama wake. Wanachama hai wenye elimu ya juu, ujuzi, uelewa wa mambo na vipawa katika fani mbalimbali hukiwezesha chama chao kufikia lengo lake kuu la kushika madaraka ya kuiongoza serikali. CCM inatambua kuwa uimara wake uko katika mikono ya wanachama wake hai kutoka katika umma wa watanzania ambao ndio hazina ya kweli ya uimara na uhai wa chama. Hivyo basi wanachama wa CCM walio nje ya nchi sawa na wenzao walioko Tanzania ni hazina ya kujivunia ya Chama Cha Mapinduzi. Nalisema hili na wala lisinukuliwe vibaya au vinginevyo, kwamba pamoja na kuwa wanachama hai wengi, chama chochote cha siasa huitaji wanachama wasomi na wanazuoni katika fani mbalimbali wenye uwezo mkubwa wa kuyachambua mambo. Wasomi na wanazuoni hawa hushirikiana na wanachama wengine kuunda sera ambazo hutumika kukinadi chama wakati wa uchaguzi. Sera nzuri huzaa ushindi wa kishindo. CCM inalitambua hili ndio maana ikafungua matawi ya nje ili kuwapata wanachama wengi zaidi na hasa vijana wasomi na wazalendo ambao wako tayari kulitumikia taifa kwa moyo wote na nguvu zote ili kushinda vita dhidi ya umaskini, magonjwa na ujinga na hatimaye kuliletea taifa maendeleo-endelevu.
Kufunguliwa kwa matawi ya CCM katika nchi mbalimbali kunabezwa na baadhi ya watu, wengi wao wanasema uanzishwaji matawi hayo unayafanya matawi ya nje ya CCM yawe sawa na matawi ya vyama vya wapigania uhuru kama PoLISARIO cha Sahara Magharibi au ZANI, ANC, FRELIMO, SWAPO, MPLA na PAC wakati wa harakati za ukombozi kusini mwa Afrika. Wanadai kwamba haipaswi CCM kuwa na matawi ya nje huku wakitoa mifano ya mataifa makubwa kama Marekani kuwa vyama vyake vikuu vya siasa vya Republican na Democrat havina matawi nje. Ukweli ni kwamba Republican na Democrat vina matawi yake na wawakilishi kwa mfano katika majiji ya London na Paris. Tukumbuke kuwa Tanzania ni nchi huru na mfumo wake wa siasa unavipa uhuru vyama vya siasa kuanzisha matawi nje ya nchi ili kuwafikia wanachama kwa urahisi na kuongeza idadi yao. Kwa mantiki hiyo hakuna kosa lolote kwa CCM kuazisha mashina na matawi ya nje. Hakuna chama cha siasa kilichozuiwa kuanzisha matawi ya nje. Hivi huu udikiteta wa kusema hakuna kufungua matawi nje unatoka wapi? Na haya mamlaka ya kuwazuia watu kuanzisha tawi la chama chao kwa hiari yao mmeyapata wapi? Kama hutaki kuwa CCM ni hiari. Halazimishwi mtu. Usijiunge. Hiyo ndiyo demokrasia. Hiyo ndiyo haki. Huo ndio utu. Kituo Kikubwa.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Unajua bwana, maafisa wa ubalozi wa Marekani pale Dar wana akili sana. Waliopatia visa za kwenda marekani wote hawana mawazo ya kijinga-kijinga namna hii. Huwezi kusikia watu wa US wakianzisha matawi ya vitu vya aina hii.
ReplyDeleteOngezeni scrutiny za applicants enyi watu wa ubalozi wa US hapo Dar. Tunaona matunda ya kazi yenu nzuri. Muendelee kuwanyima viza watu wa dizaini za namna hii ili waendelee kwenda UK, Malaysia, India na huko Napoli tuu. Ntawaletea chupa moja-moja za Margarita Mix nikija kutembea bongo. Hivi mko wangapi vile? LOL!!!!!
Kaka Michuzi acha kutubania. tumetuma maoni yetu kama koments mbona huweki.
ReplyDeleteNamuunga mkono mtoa maoni wa kwanza. Heko. Kwa kweli, ze mentality of a Tanzanian is logwa logwa by the wachawis x 4. Mi ningependa kuwauliza tu hawa watu wanaofungua matawi ya CCM nchi za nje suali moja: Ni nini hasa dhumuni na purposes ya haya matawi ya CCM?
ReplyDeleteI'm and feel ashamed to be a Tanzanian. Handshake to the first commenter.
ReplyDeleteyou misoup! bora nikuite wa kwa kiinglish sababu uko ulaya hivi unabana meseji wakati uko ulaya ili iweje narudia tena manafungua matawi ya ccm ulaya nati za kichwa zimelegea pigeni box someni mambo siasa ni hukohuko bongo ulaya haihuu!
ReplyDeleteusiulize nchi imekufanyia nini wewe utaifanyia nini sera za serikali ni nzuri sema wananchi wenyewe ,wadau wanakopa magari ya milioni arobaini bongo hi si sawa na trekta mbili angempelekea mama yake kijijini alime kwa kisasa na akodishe aingize pesa upeo wake wa elimu aanze kutafuta masoko nje na ndani kupitia mtandao anashindwa anaona prado akajioneshe town sirikali haiwezi ikafanya mambo yote kwa pato gani, halafu usitutusi wewe kama ni fala sio weusi wote weusi marekani wamegandamizwa ndio maana unawaona machizi wazungu wanajulikana mimi nimekaa zaidi ya nchi tano ulaya na pia nimekuwa marekani wazungu wanajulikana wabaguzi kwenye swala la maendeleo na kila kitu wakunyima elimu na ukisoma wanakuua waliwakata mainjinia wetu mikono wakati wa ukoloni maana tunasema made niggas au sio kuhusu matawi ya ccm ni haki yao kimsingi na chama kinachoimarisha undugu kuhusu ufisadi uko kila mahali mji cleveland ohio uko tahabani kwa sababu za ufisadi kama ukuweza kufanikiwa hapa basi popote pale matokeo yanaweza yasibadilike kuna watu walifikiri ulaya ndio maisha kufika mtoni mambo magumu wakaona wabadili uraia mambo bado magumu sasa wataka uraia wa nchi mbili babu if i made here A-town ninaweza popote cha muhimu usikimbie matatizo pambana kwa akili kama issa michuzi katoka mbali sasa anahema naye mdau A-town chagga boy ccm number 1 chama undugu maendeleo yako ni ya kujitafutia mwenyewe sio chama,sirikali au mzazi wako.
ReplyDeletemkae mkijiua kwamba haya makitu ya kufungua matawi ya sisiemu kune nchi za watu hayaruhusiwi kama raia wa kigeni kune nchi ya wenyewe.hawa jamaa ambao maisha ya mewashinda ugaibuni na kuamua kujistiri kune utapeli wa siasa wakae wakijua uhamiaji huko walipo wakinasa hizi picha wote wanakwea piapa hadi bongo africa kama una gwanda la europa au america unapokonywa mara mmoja uraudushwa home.so hizo njaa zenu boxi adimu sasa kwa sababu ya global economics crisis wengine hata ela ya kula hinhaa italy ukiwa huna kazi lazima ue kibaka maana hamna social money huko.so faza mithupu naomba usnibaniuu comenti yangu?
ReplyDeletemdau sverige
mdau A-town nimerudi tena jamaa ametutusi sana watu weusi kwanza michuzi kwa mapambano yako umetoka mbali vuta hewa hapa marekani number ya wazungu na wamerekani weusi watumia madawa ni sawa lakini namba ya weusi walio jela ni mara mbili ya wazungu na zaidi tena wakati wote wanajihushisha katika kitendo hivyo kwa usawa
ReplyDeleteMi nafungua Tawi hapa Vietnam, tena la CHADEMA maana hao CCM wameniwahi huko ITALY
ReplyDeleteMdau Vietnam
Nawapa pongezi kwa hatua hiyo. Pia natoa wito kwa wana-CCM wenzangu wote popote mlipo : tuendelee na ari hiyo hiyo ya umoja na amani. CCM NDICHO CHAMA PEKEE TANZANIA NZIMA KINACHOWAUNGANISHA WATANZANIA WA MAKABILA, DINI NA RANGI ZOTE. Wapinzani wetu wameanika tena chupi zao hadharani. They have absolutely nothing to offer but matusi, kejeli na ujinga. Tuko katika demokrasia. Waunde vyama vyao na wamwage sera zao hadharani. Matusi si sera. Mungu ibariki CCM. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa.
ReplyDeleteMzee michuzi mbona unatubania coments zetu. unataka na wewe kufungua tawi la CCM Bagdadi?
ReplyDeleteTe! te! te!
Mdau, milano italy.
Duh! Ni haibu, nasapoti maoni ya Anon wa kwanza.
ReplyDeleteKaka Michuzi, hii imekaaje? Mbona watu hawa hawa ndio tuliowaona huko nyuma kama viongozi wa Jumuiya ya watanzania Italia? Sasa mbona ni sura zile zile ndizo zinazokamata sasa uongozi wa CCM tawi la Italia? Hii ni kusema kuwa ile Jumuiya ya watanzania Italia imegeuka kuwa tawi la CCM au ndiyo kusema kuwa huko Italia watanzania ni watano tu?
ReplyDeleteMdau
NDUGU MICHUZI, NAOMBA KUULIZA KUWA NINI FAIDA YA KUANZISHA MATAWI YA VYAMA VYAMA VYA SIASA KATIKA NCHI ZA KIGENI? KUWA INAWAPA HAKI YA KUPIGA KURA KATIKA NCHI HIZO? HAPA UGIRIKI TUKO WATANZANIA WENGI SANA, JE TUNAWEZA KUANZISHA TAWI LA CHAMA FULANI NA MWAKA HUU TUKAPEWA HESHIMA YA KUPIGA KURA? VINGINEVYO FAIDA YA MATAWI YA VYAMA VYA SIASA NJE YA NCHI NI NINI? YAANI SISI WATANZANIA TUKO VIPI?
ReplyDeleteLORENZO, MZEE WA TERMINI
Jamani acheni mizengwe, kama mtataka siasa rudini bongo, tupambane kwenye majukwaa, siyo mnapiga madebe mkiwa mbagala wakati daladala yenyewe iko Ubungo, nyie vipi?
ReplyDeleteNAMUUNGA MKONO MTOA MAONI WA AWALI, NI WAZI KABISA KUWA SISI WEUSI SIJUI TUNA LAANA GANI? MBONA TUNASHINDWA KUWEKEZA KWENYE MAMBO YA MSINGI LAKINI TUNAKENUA MENO KWENYE SIASA, HIVI TUTAVUNA NINI. YAANI HATA KAMA KILA MTANZANIA ATAKUWA MWANA CCM, BADO KAMA HATUTATUMIA BONGO ZETU BADO TUTAANDAMWA TU NA UJINGA, MARADHI NA NJAA. JANI NI WAKATI WA KUBADILIKA SASA.. SIASA HUKO NJE ZA NINI??
ReplyDeleteYaani sisi walalahoi tutabaki na hali hii Milele. hatujui tulikotika, tulipo sasa na hatujui tuendako. yaani tulifikiria kuwa wenzetu mliofika nje mmefunga kidoga macho. Leo CCM, kesho CUF na keshokutwa... italia itajaa vyama wa wageni... ili iweje?
ReplyDeletemdau, toka Uturiki.