TANZANIA STUDENTS ASSOCIATION IN BANGALORE – INDIA
Wanafunzi wawili ambao ni Ndugu. Hamis Mbelwa Fintan na Ndugu.Olais Alexendra Siarra, waliokuwa wanakaa Hennur Cross ambao walikutwa na mkasa wa kuchomewa moto nyumba yao wakiwa ndani umepatikna ufumbuzi baada ya Ubalozi wa Tanzania nchini India kuingilia kati sula hilo.

Tarehe 18/03/2010 Mh. A.M.R Mwamanenge kutoka ofisi za ubalozi wa Tanzania New delhi- India aliwasili jijini Bangalore. Majira ya 1:00pm siku hiyo hiyo tulifika katika kituo cha polisi cha Hennur Cross tukiongozana na Mh. A.M.R Mwamanenge na kuonana na Inspekta wa kituo hicho ambaye alitupa maafisa wawili wa polisi ambao tulifika nao sehemu ya tukio ili kujionea wenyewe kilichokuwa kimetokea na hatimaye kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha kituo cha polisi cha Hennur Cross.
Watuhumiwa walipohojiwa hawakuwa na sababu ya msingi ya kueleza kisa kilicho wapelekea kufanya kitendo walichokifanya zaidi ya kuomba msamaha na kudai kuwa walikuwa wamelewa siku hiyo. Walikiri kosa mbele ya Inspekta wa kituo hicho kimaandishi kuwa hawatarudia tena kosa hilo na pia kama itatokea tukio lingine kwa kipindi hiki basi wao ndio watakuwa watuhumiwa wa kwanza.
Ili kuweka hali ya amani na utulivu nikiwa kama mwenyeketi wa jumuiya ya waTanzania waishio Bangalore pamoja na wahanga wa tukio hilo tulimwomba Mh. A.M.R Mwamanenge tulimalize tatizo lile kwa njia ya diplomasia kwa kuwa kuwafungulia kesi na kuwapandisha mahakamani ingeweza kuleta mgogoro zaidi na wenyeji wa nchi hii pia ingechukua muda mwingi kushughulika na masuala ya mahakama wakati kesi ikiendelea hasa ukizingatia sisi ni wanafunzi .

Tulimwomba Mh. A.M.R Mwamanenge atusaidie kutafuta njia ya msingi amabayo itatufanya tuishi kwa amani na kupata msaada wa polisi kwa haraka mara tutoapo taarifa ambazo zinaitaji msaada wao.Watuhumiwa walikukubali kulipa fidia ya kiasi cha 18,000Rupees ambazo vijana hao walitozwa na mwenye nyumba kufidia uharibifu wa mlango.
Tarehe 19/03/2010 nikiwa kama Mwenyekiti wa jumuiya ya waTanzania waishio Bangalore (TASABA) niliongozana na Mh. A.M.R Mwamanenge mpaka ofisi za High Commissioner wa polisi Bangalore na kuonana na Msaidizi wa Commissioner wa polisi Bangalore na kumweleza juu ya suala hilo na hatua zilichokuliwa kwa malengo ya kuzidisha usalama wa waTanzania waishio Bangalore- India.

Yeye alitupa mikakati ya jinsi watakavyotusaidia kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini India. Tulifika pia kwa Inspector General of Police wa Bangalore na kumjulisha pia juu ya suala hili. Hivyo kwa sasa ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na jeshi la polisi watapanga mikakati ya kuhakikisha kuwa amani na haki inatendeka kwa wananchi wa kiTanzania waishio Bagalore- India.
Ushauri wangu kwa waTanzania wale wanaotaka kuja kusoma Bangalore-India katika fani mbalimbali, wakati wanapotuma maombi ya shule au wanapotafuta shule/ vyuo wawasiliane na Mwenyekiti wa jumuiya ya waTanznia waishio Bangalore- India (TASABA) ili wapate msaada wa kimaelezo juu ya vyuo wanavyotafuta.

Hii itasaidia kuwaweka waTanzania wasomao huku kwa pamoja na pia kuwatafutia makazi sehemu ambazo hazina fujo na za usalama zaidi kwao ili pale wapatapo matatizo wakiwa wanaishi sehemu moja kwa ukaribu zaidi wapate kusaidiana kwa njia moja au nyingine.Nawasihi pia wale wote waishio Bangalore na kwingine kote nchini India kuzingatia sheria na kanuni za nchi husika na kujiepusha na vyanzo vyote vinavyopelekea fujo kutokea.
kwa niaba ya waTanzania waishio Bangalore na uongozi wa TASABA, tunakushukuru sana Mh. Balozi kwa msaada tulioupata wa kuleta amani baina yetu na wenyeji wa eneo la Hennur Cross, na mikakati iliyowekwa kuhakikisha kuwa tunaishi kwa amani na kupata haki pale tutakapo pata matatizo.

Pia tunamshukuru Mh. A.M.R Mwamanenge kwa kushirikiana nasi bega kwa bega kuhakikisha haki inapatika na kuleta amani na ulewano baina yetu na wenyeji hao na kutujengea nafasi nzuri ya kusikilizwa matatizo yetu mara tufikapo katika kituo cha polisi, ni dhahiri kuwa kwa sasa waTanzania waishio Hennur Cross/ Bangalore wataishi kwa amani.
Naomba tuzidi kupata msaada kama huu au zaidi mara kwa mara pale tupatapo matatizo ambayo yatakuwa nje ya uwezo wetu kuyatatua.
Fidelis Msomekela
Mwenyekiti – TASABA
+919742176980
Mwenyekiti – TASABA
+919742176980
jamani acheni kuvizia mademu ya kidosi, mtauwawa bure
ReplyDeletenyie kwam si wasomi yani kelelezote ulizopiga humu ndo mmetulizwa kihivyo!! mnakuwa kama wakimbizi kwani uko mnasoma bure mimi nimesoma uko india na mwisho wa mambo ndo yanavyo kuwaga hivyo hila tatizo halija tatuliwa hilo wahindi awawapendi watu weusi (kalu) sasa kwa nini alitambuhi hilo. kwa nini msisome new delhi karibu na ubalozi na mjini uko mliko vijijini ndomana mnakatwa shingo na hampati msaada wowote. JAMANI WAZAZI HATA KWA DAWA MSIWAPELEKE WATOTO WENU INDIA NI BORA MUWASOMESHA AFRICA UKO UKO!! MIMI NIMEKOMA KWENDA INDIA. MWINDI UKIWA NA PESA HATAKUPENDA SANA HILA KAMA WEWE NJAA KAMA WAO UTAJUA MAHARAGE NI MBOGA!!!
ReplyDeleteNARUDIA TENA NA TENA WAZAZI MKITAKA WATOTO WENU WARUDISHE BILA SHINGO WAPELEKENI INDIA! NA MWENYE MASIKIO NA ASIKIE!! MUNGU ANATUPENDA WATANZANIA MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATANZANIA POPOTE PALE WALIPO DUNIANI !!
hivi nyie mmefelii kiasi gani hadi mnaenda kusoma india hao wadosi wenyewe wanakimbilia UK,US,Australia na canada kusoma kwelii kuna wabongo vilazaaa yaani unaenda kusoma indiaa nasikia kuna wengine wanaenda malaysia elimu ipo nzuri tu hapa nyumbani au ata uganda,kenya au south africa
ReplyDeleteMdau wa Korea Kusini ebu sema shida zako.
ReplyDeleteExcuse me for those who say waliofeli ndo wanakuja India, What facts do you have? Sio unaongea tu kuondoa harufu mdomoni. Hao wanaoenda US,UK na SA ndio hawajafeli au? Tunatafuta elimu huku just like hao wengine. Degree ndio zitaongea zaidi kama waliokuja India walifeli.
ReplyDeletenimesikitishwa na huyo mtu anaesema eti wadogo zetu wasomao india wamefeli.nijuavyo mimi na nina vithibitisho ni kwamba hawajafeli bali ni katika harakati za kutafuta elimu na vilevile ikumbukwe ili kupata experience ya maisha ni vizuri kubadilisha mazingira, wewe mtu huwezi kuanzia shule ya msingi umesoma mwanza,sekondari mwanza,hadi chuo mwanza,ni lazima kutoka nje na kujifunza watu wengine wanaishije.
ReplyDeleteAsanteni watanzania nawapenda wote na wadogo zangu mnaosoma india mungu awalinde.
WEwe anony wa Sat Mar 20, 02:30:00 AM umenifurahisha sana.... dah sikujua Kubeba BOX kunaharibu sana ubongo na uwezo wa kufikiri Kiasi hicho... sasa ndo nimeamini.
ReplyDeleteSat Mar 20, 02:30:00 AM, wewe ni mwehu.. jua india,malaysia watu huku wanakuja kwa lengo moja la kusoma si kutafuta fedha. Na huku wengi wameshindwa kusoma wamekimbilia hizo nchi ulizozitaja kufuata mkumbo. Engineer wa India na udsm ni sawa?!
ReplyDeletenakubaliana mia fill mia na mdau wa Sat Mar 20, 05:13:00 PM
ReplyDeleteok, nimesikia kama ulivyosema kwamba kulikuwa hakuna sababu, iliyofanya jamaa kuchoma nyumba.
ReplyDeleteHivyo sasa, wewe fidelis kulikuwa na sababu gani pia ya kuwahusisha hao wahindi wasio na sababu kuchoma nyumba huko India na wahindi waliopo hapa TZ, kama nayo pia sio sababu ya msingi.
Je hufikiri kutokana na maneno yako ya ubaguzi uliyoaandika awali, WATZ wasio na sababu wangeamua kweli kuchoma au kumuua mhindi hapa TZ ungesemaje sasa.
kumbuka watu kama wewe na wahindi kama hao huko INDIA ndo huwa wanachukua maneno ya mtaani na kusikia na kuyafanyia kweli.
Nakushauri uombe msamaha kwa WATZ wenye asili ya kihindi hapa Tanzania, kwa maneno yako uliyosema kwamba eti wanakaa hali mustarehe bila bugudha.
Pia kuomba eti mimi mzazi niwasiliane na wewe ili kuleta mwanangu INDIA ni upumbavu. Wewe baba yako aliwasiliana na Mwenyekiti gani wa WATZ india ili wewe ukaenda kusoma huko. Acha kuvuta watu ndani ya chama kwa kuwaogopesha, kwamba eti hawatasaidiwa ikitokea tatizo huko.
kama cheo ubalozini au serikali TZ hutapata hata ukujifanya mwenyekiti huko India.
Ila asante sana kwa kutekeleza yanayojiri na cheo ulichonacho, cha kusaidia na kufuatilia matatizo ya mTZ yeyote aliye India. Hiyo inakuja na kazi au cheo chako na ndio shuguli yako.