
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru(katikati)akiongea na waandishi wa habari wa magazeti mama ya Daily News na Habarileo katika ofisi zao kuhusu “habari ndiyo hii”ambapo mtandao wake ulivyoshusha gharama ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom,kulia ni Mkurugenzi wa mahusiano wa Vodacom Mwamvita Makamba na kushoto ni Kaimu Mhariri wa magazeti hayo Gabby Mgaya.

Baadhi ya waandishi wa habari wa Daily News na Habarileo wakiwa katika uzinduzi wa “HABARI NDIYO HII”

Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba wapili kutoka kushoto akiongea na waandishi wa habari wa Business Times katika ofisi zao kuhusu “habari ndiyo hii”ambapo mtandao wake ulivyoshusha gharama ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom,kushoto ni Mhariri wa Darleo Imma Mbugunili, Mkurugenzi wa masoko Ephraim Mafuru,Meneja husiano wa Vodacom Mwamvita Makamba na kushoto ni Kiumu wa mawasiliano wa Vodacom Nector Pendael Foya.

Baadhi ya wahariri wa habari wa Business Times wakishiriki katika uzinduzi wa “habari ndiyo hii”ofisini kwao.

Kaimu Mhariri wa ghazeti la Tanzania Daima Kulwa Karedia wapili kutoka kushoto akishiriki katika uzinduzi wa”habari ndiyo hii”ambapo wateja wote wa Vodacom Tanzania wataongea kwa shilingi 1 kwa sekunde kila siku ,kushoto Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru na kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Mwamvita Makamba.

Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba na Mkurugenzi wa masoko Ephraim Mafuru wakiongea na wahariri wa Africa Media Group Limited katika ofisi zao kuhusu “habari ndiyo hii”ambapo mtandao wake ulivyoshusha gharama ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom.

Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba na Mkurugenzi wa masoko Ephraim Mafuru wakiongea na wahariri wa New Habari 2006 Limite walipotembelea ofisi zao na kuwahabarisha kuhusu “habari ndiyo hii”ambapo mtandao wao ulivyoshusha gharama ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom.

Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru(katikati)akiongea na waandishi wa habari wa maghazeti New Habari 2006 Limite walipotembelea ofisi zao na kuwahabarisha kuhusu “habari ndiyo hii”ambapo mtandao wao ulivyoshusha gharama ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom.kulia ni Mkurugenzi wa mahusiano wa Vodacom Mwamvita Makama na kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa New habari Bw.Shaileen.

Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru(kushoto) Mhariri wa TBC1 Jane Shirima wakizindua rasmi “habari ndiyo hii”kwa wateja wa mtandao wa Vodacom ambapo mtandao huo umeshusha gharama za maongezi kwa wateja wake kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom.

Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru(katikati)akiongea na waandishi wa habari wa maghazeti ya IPP Media walipotembelea ofisi zao na kuwahabarisha kuhusu “habari ndiyo hii”ambapo mtandao wao ulivyoshusha gharama ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom.kulia ni Mkurugenzi wa mahusiano wa Vodacom Mwamvita Makama na kushoto ni Mhariri Mkuu wa ghazeti la The Guardian Wallace Mahugo.

Baadhi ya waandishi wa habari wa IPP Media wakiwa katika uzinduzi wa “HABARI NDIYO HII”

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communication Limited Sam Sollei wakifurahia jambo wakati Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba na Mkurugenzi wa masoko Ephraim Mafuru,Meneja Mawasiliano wa Vodacom walipotembelea ofisi zao na kuhabarisha kuhusu “habari ndiyo hii”ambapo mtandao wao ulivyoshusha gharama ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom.

Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communication Limited Sam Sollei(katikati)wakizindua rasmi “habari ndiyo hii”kwa wateja wa mtandao wa Vodacom ambapo mtandao huo umeshusha gharama za maongezi kwa wateja wake kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom.Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.

Baadhi ya wahariri wa habari wa Mwananchi Communication wakiwa katika uzinduzi wa “HABARI NDIYO HII”

Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Communication Mzee Buzohera akielezea jambo kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania. “habari ndiyo hii” ambapo mtandao wa Vodacom ulivyoshusha gharama ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom.

Hii ndiyo team nzima iliyofikisha”habari ndiyo hii”kwa vyombo vya habari ambapo mtandao wa Vodacom ulivyoshusha gharama ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom.
du walitembelea kila media office? na sio press confrennce moja
ReplyDeletehivi mbona vodacom siwaelewi nani hasa huwa ni meneja uhusiano wao mara dani kijo kesho asubuhi ukiamka unaambaiwa rukia mtingwa mkikaa kidogo mwamvita makamba au nyie waandishi ndo mnakosea mara mwamvitaa huyohuyo ukisoma gazeti mchana unaambiwa ni mkurugenzi wa voda foundation mmh! nyie kuweni waangalifu ni vitut vidogo lakini vinacost
ReplyDeletegood!
ReplyDeletehatimaye nasi tuna-onyonya.
safi sana. maana tulishaanza kutafuta laini za tigo. sijui tigo watuletee nini tuhame voda!
annon #2 juu
ReplyDeletenilitaka kuuliza ivo,ebu tufafanuliane apa
hamo makini kabisa,,,
mwavita umeota tako na hips
ReplyDeleteumependeza
picha ya mwisho
ReplyDeletewee kaka katikati ya mwavita na foya,,,duh mshkaji na wewe uko uko?kweli mmebebana na mwavita.
me mwezenu wa kuleeeee........!!
hahahahaaaa
hawana mpango wanatoa kwa mkono wa kulia wananyang'nya kwa wa kushoto. Tena wamebagua baadhi ya vyombo vya habari, mbona hutukuwaona kwenye magazeti ya CCM, au si wadau wao.
ReplyDeleteNawasikitia VODACOM, mmechelewa sana kupunguza, mnakuja wakati washindani wenu wamekomba wateja wote! Mnakumbuka shuku wakati kumekucha.
ReplyDeleteNext time you have to read the signs correctly and act promptly. I am MPESA customer bu can see you are not paying us in time. A good move but too late.
Hii ndio raha ya ushindani. Vita ya panzi furaha kwa kunguru. Tigo walikuwa washafanya maisha ya mitandao mingine yawe magumu sana. Sisi wengine laini zetu za voda zilikuwa zishaanza kupata kutu. Maana hata mabosi wetu walishahamia tigo. Hebu takazitafute tena zilipo.
ReplyDeleteHebu tusikilizie tiGO watakuja na nini. No wonder ukaambiwa ni nusu shilingi kwa sekunde.
Ha ha ha ha....
KILA MPENDA KULA VYA WATU NA YEYE ULIWA....SINA MAAANA HIYOOOO!
ReplyDeleteHabari ndio hii!
Hii globu ya jamii mnapenda sana kuripoti habari za VODACOM na huyu mama Makamba. Lakini kuna tatizo moja la kuchanganya cheo cha huyu mama Makamba kwa sababu mnasema mara ni mkurugenzi wa mahusiano, maneja husiano, mkurugenzi wa vodacom foundation. Sasa which is which here?
ReplyDeleteHUYU MWAVITA NI MKURUGENZI WA MAHUSIANO. MAHUSIANO GANI? ANKAL MIMI SIJUKUELEWA. LABDA KISWAHILI KIMENISHINDA?
ReplyDeleteSisi wateja wa vodacom tunapoke habari hii kwa furaha lakini bado tunaomba vodacom waendelee kuboresha huduma bora kwa wateja.Kwa ujumla makampuni ya simu yanapata faida kubwa sana na ndiyo yanaongoza kwenye udhamini matangazo ya biashara kwenye media.Sasa fanyeni utafiti ili mje na promosheni ya kila mwishoni mwa mwaka maalum kwa ajili ya kurudisha faida yenu kwa wateja wote.
ReplyDeleteHIVI NDIO MNAONA KUWA NI PUNGUZO KUBWA KWA NCHI MASIKINI KAMA BONGO??
ReplyDeleteMIMI NAONA NI BADO EXPENSIVE
UKILINGANISHA NA NCHI YA KIMASIKINI KAMA BONGO
HUKU UGHAIBUNI IKIWA MNATUMIA COMPANY MOJA MNAONGEA BURE BILA MALIPO
Ni habari nzuri lakini imekuja wakati kumeshakucha. Lakini kinachonishangaza VODACOM bado wanabagua muda wa kuwafurahisha wateja wao. Kwa nini huduma kama hizi saa 11 hadi saa 3 usiku huwa hazihusiki? Kwa nini wanatoa huu muda? Mitandao mingine huduma zao ni siku nzima. Hili pia litawacost VODACOM. Pia VODACOM wakitoa huduma kama hizi huwa ni tabu sana kupiga simu na kumpata unayempigia. Mara nyingi utaambiwa NETWORK BUSY. Waangalie na hili pia. Mdau
ReplyDeleteduh ankal, hii habari jinsi ulivyoishughulikia hadi inatia wasiwasi, au ni mshiko?????
ReplyDeleteanony wa 04:06:00 nimekukubali mnapiga bure ina maana hiyo kampuni haina cost incurred wala hawana return on busines....du kaaz kweli kweli....VODACOM YOU ARE THE STAR!
ReplyDeletejamaa linakula denda live kabisa. lakini siyo dalili ya ukware maana ni hazalani
ReplyDeleteUkisikia shilingi kwa sekunde unaweza kuchekelea lakini maana yake ni shilingi 60 kwa dakika, sio hela ndogo hiyo. Na bado JK atakutandika VAT 18%, jumla zinakutoka shilingi 70.80 kwa dakika!
ReplyDeleteNaunga mkono aliyeeleza jinsi utambulisho wa lejaleja unavyo weza ku- cost watu au kampuni.
ReplyDeleteSi tu katika kukosea cheo cha mtu bali hata kuwa mnamtaja yeye tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu wakati kuna wakuu wake na vichwa vingine vya intelligence, planning, marketing, sales n.k wanaowezesha maendeleo ya VODA.
Tukiandika tunabaniwa eti tumechafua hali ya hewa hili ni tatizo kubwa sana. Na sidhani kuwa Michiuzi na hii leo utaibana hii maana kwa kufanya hivyo hakika utawafanya watu wajenge hasira na chuki kwake bila sababu.
Dada Mwamvita....Holla!
ReplyDeleteMFA MAJI HAACHI KUTAPATAPA...
ReplyDeleteSIKU YA KIFO CHA NYANI MITI YOTE HUTELEZA
ReplyDeleteWatanzania kila kampuni ina style yake ya kazi.. Mkurugenzi wa Mahusiano (Corporate Affairs)= Mwamvita Makamba, Meneja Mawasiliano = Communications manager ni mtu mwingine, hakuna meneja wa Uhusiano Vodacom. Na pia muelewe sio lazima uwe meneja uhusiano ndio uongee na waandishi. Hata ukiuliza waandishi tutakuambia. Meneja Uhusiano anaweza kuandaa press conference na mzungumzaji akawa mwingine, anaweza andaa mahusiano na wadau na asionekane kwenye vyombo vya habari.
ReplyDeleteHapa meneja uhusiano atufundishe lugha ya Kiswahili.Unaposema siku nzima na baadae unasema isipokuwa saa 11-3 usiku,hiyo siku nzima ipo hapo tena au danganya toto?Huu siyo mfumo mzuri wa biashara na kujali wateja.Kwa tangazo hilo la vodacom walazimika kufuta hiyo kauli ya isipokuwa saa 11-3 usiku.Vinginevyo washitakiwe kwa mamlaka ya mawasiliano kwa kuwadanganya wateja kimakusudi kupitia vyombo vya habari.Naomba maoni ya mwanasheria wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania.
ReplyDeleteWamebagua CCM ehh, Hilo linaeleweka si unajua kule Ni NO - 10%
ReplyDeleteJamani picha ya pili kutoka juu ni Irene K kule mwisho? Mbona siielewi elewi?????????? Nanyorii A town.
ReplyDeleteNashukuru ankal kwa kuniminya kiaina.
ReplyDelete