Hawa ni baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 54 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake, hutoka katika makundi mbalimbali ya jamii yakiwamo ya Asasi zisizo za kiserikali pamoja na Mashirika ya Dini.
Pichani ni washiriki kutoka Young Women's Christian Association-Kanisa la Anglican, ambao walifika Ubalozi wa Tanzania kwa lengo la kubadilishana mawazo, kuhusu masuala ya elimu kwa mtoto wa kike, ajira, umilikaji wa ardhi kwa wanawake, biashara ya binadamu hususani wanawake na watoto, masuala ya wakimbizi na masuala mengine yahusuyo haki na ustawi wa mwanamke na mtoto wa kike. ziara hiyo ilikuwa ni sehemu ya ratiba ya Mkutano wa 54.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...