Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi Afande Abdallah Mssika


JESHI LA POLISI HALINA TAARIFA ZA KUIBWA KWA SHILINGI BILIONI 300 KUTOKA KATIKA MABENKI MBALIMBALI HAPA NCHINI

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi nchini limesema halina taarifa za wizi wa shilingi Bilioni 300 zinazodaiwa kuibwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta kutoka katika mabenki mbalimbali yaliyounganishwa na mtandao huo hapa nchini.


Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, amesema leo kuwa taarifa zilizoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na wizi huo hazijafikishwa Polisi.

Kamanda Mssika amesema kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Ma
kosa ya Jinai Kamishna Robert Manumba, aliyedaiwa kukaririwa na chombo hicho cha habari, amesema kuwa hana taarifa ya tukio la wizi wa shilingi Bilioni 300.

Kamishna Manumba amesema kuwa mawasiliano kati yake yeye na Mwandishi wa taarifa hiyo kwa upande wake binafsi yalihusu tukio la wizi wa fedha katika benki ya NMB Tawi la Bank House Jijini Dar es Salaam ambapo mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu, ambapo Jeshi la Polisi lilibaini kuibwa kwa shilingi milioni 360 kwa njia ya mtandao wa kompyuta fedha ambazo zilihamishiwa katika tawi moja wapo la benki hiyo lililopo mkoani Shinyanga.
Kamanda Mssika amefafanua kuwa, mara baada ya fedha hizo kufika Mkoani Shinyanga, zilitawanywa kutoka katika tawi hilo na kupelekwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta kwenda katika akaunti mbalimbali za watu binafsi kwenye matawi mengine ya benki hiyo katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Kutokana na wizi huo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Benki ya NMB limeshafanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 319 kati ya shilingi milioni 360 zilizoibwa na kwamba tayari baadhi ya watuhumiwa waliohusika katika wizi huo wakiwemo watumishi watano wa benki wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu shitaka lao.
Hata hivyo Kamanda Mssika amesema kutokana na taarifa za kuibwa kwa shilingi bilioni 300, kama ilivyoandikwa, ametoa wito kwa Makampuni ama Taasisi za Kifedha zinazoweza kuwa zimefanyiwa hujuma hiyo ya wizi na iwapo rasimu zao za ndani kiuchunguzi zimekamilika, basi wawasiliane na Mkurugenzi wa makosa ya Jinai nchini Kamishna Robert Manumba, ili hatua za uchunguzi ipasavyo kwa kuvishirikisha vyombo vya dola ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. DUUUUUUUUUUUUUUUH CHANGA LA MACHO JENGINE MAFISADI WAMEKAA WAMEFIKIRIA TUDANGANYE VIPI PESA TULIZO IBA.

    WAMEONA NGOJA TUSINGIZIE VIJANA NA MAMBO YA COMPUTER WATAKAMATWA WATU HATA SIO. TUONGOPEENI TU.

    RUDISHENI PESA ZA WATU JAMANI. SEIF.

    ReplyDelete
  2. Internet Banking CustomerMarch 22, 2010

    MMh! Mbona tukio tajwa halikuwa covered na hata wahusika wajulikane au mimi ndio sikuwa hewani kufahamu?

    Maana wananchi tupaswa kuelezwa tujitahadhali na hawa wezi wa mitandaoni.

    ReplyDelete
  3. computer ExpertMarch 23, 2010

    Jamani TANZANIA, bado mnataka kuficha hata hilo, kubalini kama kweli mmeibiwa,sisi bado sana tuko nyuma na mambo ya mtandao,msijifanye mnajua, kama zimeibiwa kubalini tu, basi kila kitu nyinyi ni kukanusha tu!!!!!!!
    Kwani TZ ni ya kwanza kufanyiwa hivyo?mbona manchi mengi tu yameshafanyiziwa ila nyinyi mnataka kujifanya smart, kwamba kila kitu TZ ni bomba,Jamni tukubalini ukweli!

    ReplyDelete
  4. Bwana Michuzi vaa miwani..angalia isije ikwa kwa vile GLOBU yako inachangiwa saaana wakasema ilihusika katika upotevu huo kisha ukasikia tangazo rasmi toka SIRI KALINI imefungiwa toka leo,hao si ndio wanatuambia umeme wa mgao,ati chura wameingia katika jenereta,au maji hakuna wakti mafuriko yanazoa watu kilosa..wanazusha sana hao!KAA CHONJO SAA MBAYA!

    ReplyDelete
  5. Is man a man or a woman? Hebu angalia sura yake.

    ReplyDelete
  6. HAYA MAMBO YA WIZI WA FEDHA NI HATARI SANA CRDB WANAFAHAMU NI KIASI GANI WAMEPOTEZA NA MATUMIZI YA "TEMBO". NA MAMBO NDIO YAMEANZA HAO KUWENI MACHO SANA.

    ReplyDelete
  7. jamani hili siyo suala la mchezo. Kila mtu ake macho na akaunti yake. Hasa hao jamaa wanaofanya manunuzi na hizo kadi za tembo. Ila pia maoni ya mdau aliyesema labda wajanja wamejichotea kisha wakasingizia mitandao. Unajua uchaguzi unakaribia lazima wajanja watafute pesa kwa kila ujanja. Na kaka michuzi kama kweli pesa zimechotwa kimtandao tutaanza kufanya utaratibu tukuhoji maana wewe ni miongoni mwa wajanja wa hi fani ...
    Ila Ankal shukrani kwa kutustua na hii ishu siyo ya kupuuzia...be alert. huu wizi upo kila kona ya dunia...

    ReplyDelete
  8. Wewe Michuzi usipotoshe umma BILLION 300? Tz money or Zimbabwe dollar?

    ReplyDelete
  9. polisi wamesema hawana taarifa na huu wizi. Sasa kwa nini wametoa taarifa kwa vyombo vya habari. Mimi siwaelewi Polisi Tanzania. kama ni fununu mnatakiwa mzichunguze then mjue undani kisha ndo muingie k=hewani kwa Michuzi Blog. sasa mnasikia fununu tuu hamna uhakika na ishu tayari mko hewani. Nilidhani wangekaa kimya wakaanza uchunguzi wa haraka kupitia hizo benki na Benki kuu then in few days/minutes wangetoa taarifa ya uhakika wa walichokigundua vs fununu.
    Kaka Michuzi huu utaratibu wa hata mambo madogo kwenda hewani utatukosesha mengio na kuvuruga hata upelelezi. sasa kama wajanja wamevuta hela na wanaona habario kwenye blog kuwa eti polisi wanashangaa na hawana taarifa, si hawa jamaa wataingia mitini kama wako nchini bado....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...