ANKAL MICHU,
SISI WADAU TULIO KATIKA JENGO LA PPF TOWER TUNAOMBA UONGOZI WA JENGO HILI UTUSAIDIE KUTATUA KERO ZIFUATAZO:
· LIFT HAZIFANYI KAZI, TULIO GHOROFA KUANZIA YA 10 KWENDA JUU NI KIMBEMBE KUPANDA KWA MIGUU, YANI UTAWAHURUMIA KINAMAMA WAJAWAZITO WANATESEKA SANA
· USAFI UBORESHWE IKIJUMUISHA UWEPO WA MAJI NA KUUA WADUDU (FURMIGATION) AMBAO HADI SASA WANATUSUMBUA SANA KAMA MENDE NA WENGINE
· AIR CONDITION ZITENGENEZWE MAANA TUNAPATA SHIDA YA JOTO AMBALO LINAPUNGUZA UFANISI WA KAZI
SISI WADAU WA PPF TOWER, DSM
· LIFT HAZIFANYI KAZI, TULIO GHOROFA KUANZIA YA 10 KWENDA JUU NI KIMBEMBE KUPANDA KWA MIGUU, YANI UTAWAHURUMIA KINAMAMA WAJAWAZITO WANATESEKA SANA
· USAFI UBORESHWE IKIJUMUISHA UWEPO WA MAJI NA KUUA WADUDU (FURMIGATION) AMBAO HADI SASA WANATUSUMBUA SANA KAMA MENDE NA WENGINE
· AIR CONDITION ZITENGENEZWE MAANA TUNAPATA SHIDA YA JOTO AMBALO LINAPUNGUZA UFANISI WA KAZI
SISI WADAU WA PPF TOWER, DSM
NI AIBU KUBWA KWA JENGO ZURI NA KUBWA KAMA HILO KUWA NA MAPUNGUFU KAMA HAYO. WATANZANIA TUJIFUNZE KUWA NA DISCIPLINE KATIKA BASIC THINGS, VITU VYA MSINGI. UNAWEZAJE KUWA NA JENGO LENYE GHOROFA ZAIDI YA 10 HALAFU LIFT ZINAKUWA UNRELIABLE!, JENGO ZURI KAMA LILE LINAKUWA NA MENDE NA INZI NA PANYA!! WHAT A SHAME! NA MAJI JE, HAWANA RESERVE TANKS ZA KUTOSHA? KUNA WATUMIAJI WANGAPI KATIKA JENGO HILI, WAGENI KIBAO, UNAMPA PICHA GANI MGENI ANAPOKUTA NYUMBANI KWAKO CHOO KICHAFU, WHAT A SHAME!
ReplyDeleteTIA= This Is Africa
ReplyDeleteTIT= This Is Tanzania
TID= This Is Dar
Tehe, tehe, tehe .....!
mlalamikieni mwajiri wenu, ikishindikana muhame sio kama mnalitumia bure hilo jengo, na hamlazimishwi lada mwajiri wako naye anapata punguzo la kidi kwa hiyo anauchuna tu.
ReplyDeletehata kama mkataba haujaisha ila kisheria mna haki ya kuuvunja kama vitu muhimu havipo provided.
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteFurmigation ndiyo nini? Na mlalamikaji anaposema "Air Condition zitengenezwe" anamaanisha nini? Mimi sijaelewa.
ReplyDeleteMdau.
Wabongo bwana,hamjui nguvu ya media.Kila mtu anajua Michuzi blog inafuatiliwa na watu wa aina mbalimbali cha ajabu ni hawa wajinga wachache wanaowaambia watu wahame.Hawa watu ndo wanaondekeza ugonjwa,vitu vinapoletwa kwa michuzi ni kwa manufaa ya kila mtu.Leo unawapaka wenzako kesho utakuwa ww unayehitaji kwenda kupata huduma ktk jengo hili na hizi shida utakumbana nazo ndipo utakapoona uchungu wanaoupata wadau.Jamani fumbukeni.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeletelinchi la ajabu sana watu kutwa tunalilia maendeleo yakiletwa ndo kama hivyo yani ni aibu sana hivi kweli wahusika si mnasafirigi jamani si mnaona kwa wenzenu kulivyo bomba??? ni kujituma tuu na wala hawana mikono mitatu ni miwili tu kama sisi jengo tamu na safi ni kempiski bwana kwa vile tu halimilikiwi na mmbongo na hakika hiyo ppf tower akimiliki mzungu tu kila kitu kitakuwa shwari mazoea yana tabu tushazoea uzembe na uchafuuuuuu!!!!!
ReplyDeletejamani hayo malalamiko mm ningependa yaende kwa wahusika na kama wahusika wanasoma bsi fanyieni kazi kingine wekeni toiet paper za kutosha sio ikifika lunch time ndo mwisho wa usambazaji huo plspls mnataka watu wanuke jamani sio vizuri kama mmeshindwa achieni ngazi kuna watu wanaweza na nyie mnaoacha maji wazi tbia mbaya
ReplyDeletemdau
jamani yahitaji tubadilike sasa...tujue ya kwamba kuna mada wala hazihitaji kubezana wala kupondana kwa lugha nyengine...kama mtu huna la kumshauri mtu katika jambo kama hili ni bora ukanyamaza kimya na kutafakari mambo yako mengine muhimu! siwezi kusema kuwa unayocomment ni utombo au laa but ujiulize ni mahala pake hapo au ni wakati wake huu...mbona kuna hoja kibao jamani za kutoa pumba kama hzo...!! nasikitika sana kwa tabia kama hii kwan naamini fika kuwa watumiaji wa blog hii asilimia kubwa ni watu wazima ie above 18...na kwa lugha nyengine naweza kuwaita wasomi...lakin hu ku ndio kuelimika jamanii..mtu kutofaham jambo fulan kuwa wakati fulan na mahala fulan halipaswi kufanywa...!! TUBADILİKE WADAU...!!!
ReplyDeleteDah...
ReplyDeleteMdau wa Wed Mar 17, 02:49:00 PM
Umeniacha hoi kwelikweli na hizi lugha,ila mlalamikaji alimaanisha FUMIGATION na pia anadai kuwa AIR CONDITIONER zitengenezwe.
Yeye ameandika kibongo bongo zaidi cunajua kiswazi watu tulishamwelewa siku nyiiingi na wala hatukugundua kama amekosea.
hope umeelewa kimtindo au sio?
Mdau wa Mashariki ya Mbali.
Teh teh teh teh! uwiii! me nilifikiri ni jengo chakavu pekee na lililojichokea la POSTA HOUSE ndo linatatizo hilo pekee! kumbe hata majengo mazuri km haya! UPUUZI MTUPU!
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteooh ! hilo la 16th mi simo
ReplyDeletetumjadili huyu landlord wetu anayeitwa PPF
leo nimeona kibandiko kwenye lift kimeandikwa kuwa lift ni mbovu zitakuwa zinapona moja baada ya nyingine lets bear with zemu !
BOngo tambarareeeeeeeeeee