mkuu wa nanihii,vekesheni njema.
Kaka naomba tusaidie mawazo kuhusu hali ya usalama wa raia,vibaka wamezidi,maeneo ya jangwani darajani hapafai. Unakumbuka palikuwepo ulinzi baada ya mtu kukatwa shingo kwa waya aliyepita akiwa kwenye pikipiki.
Juzi tu nimepita hapo mnamo saa3 usiku nikakuta kijana kalala hoi analia baada ya kupigwa ngeta na kunyang'anywa kila kitu, na vibaka wanakimbia.
Sehemu nyingine ni mataa ya chang'ombe na batabara ya Nyerere road. Wananchi wanalizwa sana hapo. Je polisi na mgambo wa jiji hawawezi kusaidia?naomba kuwasilisha.
mdau -Dar.
DAWA YAO HAO NI MANYOYA TU!
ReplyDeleteHapo kesi ya nyani inapelekwa kwa ngedere. Unauliza polisi na mgambo mko wapi.?!! Wanajua wenyewe walipo.
ReplyDeleteKazi ya watu hii . Ni mtu mwenyewe kujichunga asiingie mitego yao.
Mi hata sielewi! viongozi nchi imewashinda au? Mbona ni rahisi sana kuwamaliza hawa vibaka.
ReplyDelete