Washindi wa NOKIA SHARE WEDDING COMPETITION,
Bw. Alex Ngasa na Bi. Johari Boniface, baada ya kumeremeta.

NOKIA waliandaa shindano la NOKIA SHARE WEDDING COMPETITION ambapo wachumba Tanzania nzima walitakiwa kutuma picha zao pamoja na love story ya jinsi walivyokutana, ili ziwekwe kwenye mtandao na kushindanishwa kwa kupigiwa kura na wananchi kwa muda wa takriban wiki nane, ambapo couple itakayo shinda NOKIA itawazadia mnuso wenye thamani ya milioni 25, kwa sharti la kwamba wawe wamefunga ndoa ya kihalali.
Waliobuka washindi wa NOKIA SHARE WEDDING COMPETITION ni Bw. Alex Ngasa na Bi. Johari Boniface wa Dar es salaam, ambao wamezawadiwa mnuso huo wa nguvu iliofanyika Golden Tulip Hotel jijini Dar.
GLAMOROUS Event Planners ndio walichaguliwa rasmi na NOKIA kuandaa THE NOKIA SHARE WEDDING EVENT.

Ushers wakipokea wageni waalikwa na kuwapa NOKIA giveaways

maharusi wakiwasili kwenye mnuso wao wa NOKIA

wageni waalikwa wakiduarika wakati wa mnuso huo
eneo la tukio Nancy Sayore (shoto) na Vumilia Kaaya, Wakurugenzi wa Glamorous Event Planners ndio walio andaa event hii kwa niaba ya NOKIA, walikuwepo kuhahikikisha shughuli inafana. Ukiwataka watafute kupitia:
Glamorous caters for any Organizational,
Personal, Leisure and Culture Events.
For more info please visit
Tel: +255 22 2772230/0784 410254





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. MSAADA TUTUNI, HII HAIHUSIANI NA HIZI PICHA ZILIZOTUNDIKWA, ninaswali linanitatiza. Hivi ugonjwa unaoitwa "Hypertensis" kwa kiswahili unaitwaje? aksateni wanajamii na mzeee wa maparachichi

    ReplyDelete
  2. Mdau "Hypertensis" kwa kiswahili inaitwa "Haitupatisisi" Huu ni ugonjwa unaowapata wazungu tu.

    ReplyDelete
  3. mimi naomba anauani ya hayo Gramorous event planners

    ReplyDelete
  4. Wachawi wa Tanzania, wanaongelea magonjwa wakati wa jambo jema la furaha na baraka.
    Mshindwe kwa jina la Yesu. Dini pinzani

    ReplyDelete
  5. Hahahahahaha mie mbavu zangu kuna watu wanaingia humu hawajui hata umuhimu mwenzio kauliza swali la maana ww unajibu utani eti "haitupatisisi" kweli kuna watu hamnazo mwenye kujua pls msaidieni mdau ankal picha umezibania sana mpe shamimu atutolee zote cos ni fani yake otherwise big up

    ReplyDelete
  6. jamani Vumilia aka mama nancy uko wapi? miss u sana!kaka michuzi naomba anuani ya glamorous event planners please.

    ReplyDelete
  7. jamani ankal unabana saana meseji sasa unatoa picha ya nini ka cinema si ili tutoe komenti? na kila mtu ana mtazamo wake alimradi mtu hatukani tunaomba uwanja uwe mpana yani hii blogu siku hizi imekuwa kimabavumabavu sana ankal acha hizo unatukera sana, tukirudi kwa maharusi kweli walipendeza saana ila bibi arusi mkorogo aachae awe natural mbona ana mvuto tuu

    ReplyDelete
  8. weee annon sio mkorogo ni mapouda yanaitwa "foundation"

    sijaelewa hii sentensi hapo juu "kwa sharti la kwamba wawe wamefunga ndoa ya kihalali"

    ReplyDelete
  9. GLAMOROUS EVENT PLANNERS CONTACTS:
    Email: info@glamorous.co.tz
    Tel: +255 22 2772230/0784 410254
    Web: www.glamorous.co.tz

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 03, 2010

    Nancy Sayore na Vumilia Kaaya, mnatisha kama njaa wanangu.. keep up the good work

    ReplyDelete
  11. mmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!i harusi ilikua ya ukweee jaman.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...