Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano NMB Shy-Rose Bhanji, akiangalia wanafunzi wakiwa wameketi chini kabla ya kukabidhi msaada wa madawati ya darasa moja kwa Shule ya Msingi Jitegemee Bagamoyo. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki Gabriel Ole Loi Banguti na Kulia ni Meneja wa NMB tawi la Bagamoyo Elizabeth Chawinga. Makabidhiano hayo yalifanyika Mjini Bagamoyo .
Juu na chini anaonekana Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano NMB Shy-Rose Bhanji, akikabidhi msaada wa madawati ya darasa moja kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jitegemee Bagamoyo -Dina Mjema, ikiwa ni msaada wa NMB kwa shule hiyo. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki Gabriel Ole Loi Banguti na Kulia ni Meneja wa NMB tawi la Bagamoyo Elizabeth Chawinga. Makabidhiano hayo yalifanyika Mjini Bagamoyo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hii picha imenikumbusha mbali sana wakati nasoma iringa kabla sijahamishiwa dar ambako mambo ndio yalikuwa yale yale ya kukaa chini. wazazi wote walichangishwa mia nne ndio hapo tukaanza kupata madawati. yaani ingekuwa vizuri wangefuta mambo ya wanafunzi kwenda shule na kopo la maji na mfagio, vitu viwili hivi vinaniudhi sana, ningekuwa waziri ningefanya ajira hapo itokezee ya watu maalum wafanye hizo kazi lakini sio wanafunzi. wanafunzi wasome tu. naona inachanganya wanafunzi mara unasahau daftari mara kopo, kipi muhimu kisomo au hayo makopo ya maji na mifagio? na juu tena ya hapo kukaa chini? wadau jibuni.

    mrs baker

    ReplyDelete
  2. Brand shy-rose! The most photographed lady in Bongo

    ReplyDelete
  3. yani hadi leo mijini wanafunzi wanakaa chini!!wakati mafisadi wana chota ma bilioni kila siku!!chabuke kweli hakiji bure DONATED BY NBC !!!HAHAHA ADI KERO SASA!!

    ReplyDelete
  4. kwa kweli haipendezi kabisa karne hii kwa watoto wa shule kukaa chini...shime shime watanzania tuwasaidie watoto wetu wakae kwenye madawati. asanteni nmb kwa mchaango wenu

    ReplyDelete
  5. Hapa inasikitisha sana sana leo mwaka 2010 bado kuna wanafunzi wanakaa chini!!!!Ukiona Toyota VX zenye thamani ya milioni kama 400 kwa kila moja zilivyo nyingi serikalinihuwezi kuamini kama hii serikali ina shule ambazo wanafunzi wanakaa chini kipaumbele ni nini????ubabaishaji umepitiliza kila kitu kibovubovu tu utafikiri nchi haina mwenyewe hata madawati!!!!!vipande vya mbao vilivyouganishwa kwa misumari navyo vinakuwa tabu!!!Nchi haina mwenyewe hii!!!inasikitisha sana

    ReplyDelete
  6. kazi nzuri nmb

    ReplyDelete
  7. Asanteni benki ya NMB kwa msaada wa madawati. Kwa kweli msaada umetolewa shule ambayo inastahili kabisa. hivi mpaka leo watoto wanakaa chini? inasikitisha sana.

    ReplyDelete
  8. its true shyrose is arguably the most photographed lady in tz

    ReplyDelete
  9. this is what i call CSR, keep it up NMB

    ReplyDelete
  10. Hongereni NMB kwa kuchukua jukumu ambalo lilipaswa kufanya na serikali yetu ambayo kwa bahati mbaya inahangaikia kutumia mamilioni kukarabati nyumba za vigogo.
    Ila kuna kajikasoro kadogo wamefanya NMB,hamukuwa na haja ya kuangaza maandishi makubwa ya "DONATED BY NMB",nembo ndogo ya NMB ingeweza kubeba the same message bila ya kubadilisha maana ya huo msaada,tujaribuni kuwa wabunifu.
    Mdau Wa Istanbul

    ReplyDelete
  11. Nakumbuka wakati niko darasa la pili na tatu mwaka 1989 na 1990 kulikuwa kuna fomu za michango walimu walikuwa wanatupa tupeleke kwa wazazi,zilikuwa za kuchangia madawati sijui walikuwa wanaziita UPE.Leo ni 2010 hakuna mabadiliko kabisa yaani inasikitisha sana.

    mdau
    duniayetukubwa.blogspot.com

    ReplyDelete
  12. I agree with all those outcries about deprived children and families but I note a bit of exaggeration here. No VX will cost Tshs. 400m/=. Information is power, so let us be careful with what we say lest people thought we make up things. Indeed, in a law suit a defense counsel may pick up a flawed statement such as the one above and win the case...

    ReplyDelete
  13. asantenu nmb kwa msaada wenu bagamoyo na sehemu zingine ambazo mnaendelea kusaidia

    ReplyDelete
  14. al musoma, ongea kiswahili tu usijitie mzungu hapa. ni kweli vx haifiki 400m but ukweli ni kwamba it cost more than what we can really afford as a government. kununua vx wakati watoto wanakaa chini ni ushenzi, period. I think na wewe ni mmoja wao that why unatetea ufisadi. mungu atawalipia walala hoi hapa hapa duniani.

    ReplyDelete
  15. Al Musoma, kazi si kununua VX, kazi ni kulitunza. Afadhali hiyo gharama ya kulinunua. Ufisadi ni mkubwa katika kuyatunza (mafuta, matengenezo, nk) na kwa njia hii watu wamejenga maoghorofa. Kasome ripoti ya matumizi ya serikali ambayo juzi CAG amemkabidhi JK ndio utajua tunakoelekea!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...